MTUNZI: Rulea Sanga
ONYO: Tafadhali usiangalie majibu kabla ya kujibu kwa kutumia akilia yako
MASWALI
MASWALI
- (a) Kwanini Mafarisayo walitaka
kumvizia Yesu katika Sinagogi kwa kutaka amponye mtu ambaye aliyepooza
mkono wake wa kuume siku ya sabato.
(b) Baada ya Yesu kuona mawazo ya Mafarisayo kuhusu kumponya mtu aliyepooza mkono wake wa kuume, alimwambia nini kwa huyo aliyepooza
(c) Yesu aliwaambiaje Mafarisayo kuhusiana na alivyomponya mtu aliyepooza mkono wake wa kuume katikaSinagogi?
(d) Je, Yesu alimponya yule mtu aliyepooza mkono wake wa kuume?
- Yesu aliporudi kutoka mlimani
ambako alikuwa akioomba na kukesha usiku kucha, ni kwanini makutano
walitaka kumgusa?
- Malizia misemo ya Bwana Yesu
aliyosema kwa wanafunzi wake:
(a) Heri ninyi mlio na njaa-------------------------------------
(b) heri ninyi mliao sasa----------------------------------------
(c) Heri ninyi watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu na kulitupa nje jina lenu kama neon ovu kwaajili ya Mwana wa Adam---------------------------------------------------
(d) Ole wenu mlio na mali, kwa kuwa--------------------------------------
(e) Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa kwa kuwa-------------------------
(f) Ole wenu ninyi mnaocheka kwa kuwa-------------------------------------
- Yesu alisemaje kwa wale ambao
wanaotuchukia au adui zetu?
- Yesu anasema tufanye nini kwa
wale
(a) Wanaotulaani
(b) Watupigao shavu moja
(c) Watunyang’anyao majoho yetu
(d) Watuombao
(e) Watunyang’anyao vitu vyetu
MAJIBU
- (a) Walitaka kumshitaki (Luka
6:7)
(b) Ondoka, simama katikati (Luka 6:8)
(c) Je, ni halali siku ya Sababto kutenda mema au kutenda mabaya; kuponya roho au kunyamaza? (Luka 6:9)
(d) Yesu aliwakaza macho, akawaambia, “Nyoosha mkono wako, akanyoosha mkono wake akawa mzima tena (Luka 6:10)
- Kwasababu uweza ulikuwa ukimtoka
ukiwaponya wote (Luka 6:19)
- (a) kwasababu mtashibishwa
(b) kwasababu mtacheka
(c)
(d) faraja yenu mmekwisha kuipata
(e) mtaona njaa
(f) mtabembelezwa
(Luka 6:20-26)
- Tuwapende (Luka 6:27)
- (a) Tuwabariki (Luka 6:28)
(b) Tuwageuzie shavu la pili (Luka 6:29)
(c) Tusiwazuilie (Luka 6:29)
(d) Tuwape kile watuombacho (Luka 6:30)
(e) Tusitake waturudishie (Luka 6:30)
Comments