RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE


Mtunzi: Rulea Sanga

ONYO:
Ni dhambi kubwa sana kuona unaangalia majibu kabla ya kujibu kwa kutumia Bongo yako. Jitahidi kujibu kwa kutumia akilia yako kabla ya kuangalia jibu.

MASWALI
  1. (a) Yesu aliingia kwenye chombo cha nani cha kuvulia samaki wakati wavuvi wakiwa wametoka kuosha nyavu zao?

    (b) Je, Yesu alifundisha watu waliokuwa katika chombo cha wavuvi?

    (c) Ni kitu gani Simoni Petro alikifanya kwa Yesu baada ya kuona samaki aliokuwa anavua wamejaa katika vyombo vyao viwili?

    (d) Unafikiri Simoni Petro alishikwa na mshangao alipoona samaki ni wengi sana, yeye pamoja na Yakobo na Yohana?

    (e) Yesu aliwaambia nini, Simon baada ya kushangazwa na wingi wa samaki ambao hakutegemea kuwavua?

  2. (a) Mtu mwenye ukoma, alifanya nini ili alipomuona Yesu na aliomba nini kwa Yesu?

    (b) Yesu alifanyaje kumponya mtu mwenye ukoma?

    (c) Baada ya kutakasika mwenye ukoma, Yesu alimwambia nini cha kufanya kwa kuhani?

  3. (a) Baada ya watu waliomchukua mtu mwenye kupooza kukosa nafasi kutokana na wingi wa watu waliokuwa wakimsikiliza Yesu. Walitumia njia gani kumfikia Yesu ili amponye?

    (b) Yesu baada ya kuona imani ya waliombeba yule mwenye kupooza, aliwambia nini?

    (c) Waandishi walisema nini baada ya kuona Yesu ametoa msamaha wa dhambi kwa yule aliyepooza?

    (d) Yesu aliwaambia nini waadishi hao baada ya kuona mioyo yao?

    (e) Watu walipomuona yule mwenye kupooza akijitwika kile alichokilalia, Je, watu hao ni kitu gani walikifanya?

  4. (a) Taja jina la mtoza ushuru ambaye Yesu alikutana naye baada ya kumponya mwenye kupooza

    (b) Yesu aliambiwa nini na huyo mtoza ushuru baada ya kuonana naye?

    (c)  Kwanini Mafarisayo walinung’unika walipomuona Yesu anakula chakula na kunywa pamoja na watoza ushuru?

    (d) Karama ilifanywa na nani kuwakusanya mafarisayo, watoza ushuru na Yesu kula chakula na kunywa?

    (e) Yesu aliwajibuje wale Mafarisayo waliokuwa wanashangaa kuona Yesu anakula na watoza ushuru?

  5. Yesu alisema maneno haya baada ya kusikia nini kutoka kwa Mafarisayo, “Je, Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa harusini, akiwapo Bwana harusi pamoja nao?” Lakini siku itakuja  watakapoondolewa Bwana harusi ndipo watakapofunga siku zile

MAJIBU
  1. (a) Simoni (Luka 5:3)

    (b) Ndiyo (Luka 5:4)

    (c) Alianguka magotini pa Yesu akisema, “Ondoka kwangu kwa maana mimi ni mwenye dhambi, Bwana” (Luka 5:8)

    (d)  Ndiyo walishikwa na mshangao (Luka 5:9)

    (e) “Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu” (Luka 5:10)

  2. (a) Alianguka kifudifudi na akamuomba Yesu akisema, “Baba ukitaka waweza kunitakasa” (Luka 5:12)

    (b) Aliunyosha mkono wake akamgusa akisema “Nataka takasika” (Luka 5:13)

    (c) Nenda ukajionyeshe kwa kuhani ukatoe kwaajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao” (Luka 5:14)

  3. (a) Walipanda juu ya dari wakampitisha katika matofali ya juu wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu (Luka 5:19)

    (b) Ee, rafiki umesamehewa dhambi zako (Luka 5:20)

    (c) Walihojiana wakisema, “Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake? (Luka 5:21)

    (d) “Mnahojiana nini mioyoni mwenu? Kusema umesamehewa dhambi zako au kusema Ondoka, uende? Lakini mjue ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi. (Luka 5:22-23)

    (e) Walishikwa na mshangao, wakamtukuza Mungu, wakajaa hofu, wakisema leo tumemuona mambo ya ajabu (Luka 5:25)

  4. (a) Lawi (Luka 5:27)

    (b) “Nifuate” (Luka 5:27)

    (c) Kwasababu watoza ushuru walionekana kuwa wenye dhambi (Luka 5:30)

    (d) Lawi (Luka 5:29)

    (e) Wenye afya hawana haja ya tabibu, isipokuwa walio hawawezi, sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu (Luka 5:31)

  5.  Baada ya kuona wanafunzi kufunga mara nyingi, na kuomba dua, kadharika wanafunzi wa Mafarisayo, lakini wanafunza wa Yesu kunywa na kula (Luka 5:32)

Comments