Mwigizaji wa filamu Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ hivi
karibuni alidai kuwa siku za nyuma baada ya kuzongwa na matatizo
aliamua kumrudia Mungu wake kwa kuokoka katika kanisa moja maeneo ya
Mwenge akiamini kuwa anaenda kupata faraja lakini alichokutana nacho
huko ikibidi kurudi katika kanisa lake la awali.
“Unajua kuna wakati mtu
unapokabiliwa na mitihani unaangalia njia sahihi ya kutafuta utatuzi,
kwa wakati huo njia sahihi kwangu niliamua kuokoka na kujiunga na
kanisa moja Mwenge, sasa kilichonikimbiza ni pale Mchungaji aliposema
Mungu atakubariki ukitoa fedha nyingi kama sadaka,” alisema Kabula.
Jini Kabula kutokana na mahubiri hayo
ya kuhimiza sadaka kubwa kuwa ndio kigezo cha kupata Baraka aliona
kumbe maskini wanaosali katika kanisa lile wanapoteza muda kwani hawezi
kuokolewa kwa sababu ya sadaka zao kuwa ndongo, Kabula akaona ni bora
kurudi katika dhehebu lake la Sabato.
Source: Vituko vya Mtaa

Source: Vituko vya Mtaa
Comments