RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KIDATO CHA SITA

Samahani wadau wangu wa Ruma Africa, leo ningependa kutoa ushuhuda wangu juu ya matendo makuu ambayo Mungu ameyafanya kwangu tangia nimempokea Yesu Kristo.

Kuna siku moja nilikuwa naagalia hizi picha zangu kabla sijampokea Yesu na mwokozi wangu, na nikawa natafakari maisha yangu ya badaae yatakuwaje. Nikiwa shule nilikuwa kijana mmoja mkorofi sana, na niliadhirika na maisha ya watu wa Marekani. Nilipenda sana kuishi kama mastaa wa Marekani hasa hawa waimbaji wa muziki wa Hip Hop. Nilikuwa napenda sana mavazi yao na ile kujifanya wagumu wasiojali wakubwa wala walimu wao.

Nakumbuka nikiwa kidato cha pili nilijiunga na kikundi fulani cha vijana waliofukuzwa shule ya Tambaza kutokana na utukutu. Nilipenda sana vile walivyokuwa wanafanya mambo yao ya kuwa kama gangstars. sikupenda kujishughulisha na masomo kiufasaha. Namshukuru Mungu hata kama sikuwa nafuatilia sana masomo, lakini kuna baadhi ya masomo nilikuwa nayaweza vizuri sana. Na jambo lingine Mungu aliniepusha na uvutaji sigara na ulevi, sikuoenda kabisa kusikia vitu kama hivyo maishani mwangu. Pia katika kundi hilo la tambaza hakuna aliyekuwa anavuta sigara wala pombe.

Nimesoma shule ya serikali ya Njombe inayoitwa NJOSS (Njombe Secondary School) kipindi hicho Mwalimu Mkuu alikuwa anaitwa Mwanyigu. Nikiwa shuleni hapo nilikuwa natoroka shule na kwenda disko. Na kurudi usiku wa manane  shule na marafiki zangu. Kumbuka nilikuwa nasoma bweni. Mara nyingine nilikuwa nahonga pesa kwa viongozi wa bweni ili waweze kuniandika nilikuwepo bwenini wakati niko mjini-disko.

Nikiwa kidato cha nne nikaamua kumpokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wa maisha yangu. Nikiwa shule kulikuwa na vikundi vya UKWATA, nilijiunga navyo na kuwa mtumishi mzuri sana. Niliendelea na wokovu huo mpaka sasa. Nikiwa katika wakovu kuna majaribu mengi niliyapata kutoka kwa rafiki zangu niliokuwa nashinda nao disko, walinicheka sana na kuniambia nimepotea sana. wasichana nilikuwa nao walinidharau sana, na wakasema siwezi kufika mbali na wokovu wangu.

Ni kitu gani kilinitokea baadae...Endelea kuvuatilia katika blogu hii, uone matendo makuu ya Mungu

BAADHI YA PICHA NIKIWA O'LEVEL NJOSS
 Rulea wa pili kutoka kushoto nikiwa Mbeya kipindi cha likizo
 Rulea Sanga niliyevaa sandos nikisoma bwenini
 Rulea Sanga kushoto nikiwa na kikundi cha Tambaza. Kutoka kulia ni Allen Mwihava, wa tatu ni Nasoro, Tryphone na Embagise

 Rulea sanga kulia nikiwa na rafiki yangu niliyempenda sana shuleni
 Rulea sanga nikiwa na marafiki zangu, kulia ni Samy ambaye kwa sasa ameokoka, Yusuph
Nikiwa Disko

 Rulea sanga katikati katika mapozi..Mungu anisaidie
 Rulea sanga wa pili kutoka kushoto nikiwa na rafiki zangu Mbeya kipindi cha likizo
 Rulea Sanga wa pili kushoto nikiwa na rafiki zangu wa kidato cha pili
 Rulea Sanga wa tatu kutoka kushoto nikielekea mjini kuzurula wakati wenzangu wako darasani
 Rulea Sanga wa pili kutoka kulia nikionyesha mapozi ya mamtoni, na rafiki zangu wa Tambaza
 Kutoka kushoto ni Fikiri, Simon (niga), Deo ambaye alipata Division One, Rulea Sanga
 Rulea Sanga wa pili kutoka kulia nikiwa na class mate zangu. Kulia ni Samy Black
 Rulea Sanga kulia, nikiwa najisomea na rafiki yangu Fadhili Rwendo ambaye sasa hivi ni Mwanashera (Wakili)
 Rulea sanga wa pili kutoka kushoto, wakati wa gradution yangu kidato cha nne
 Rulea sanga nikiwa katika gari la Marehemu kaka yangu Amir Sanga maeneo ya Mafinga Iringa wakati wa likizo
 Nikipata chakula cha jioni katika Dinning Hall NJOSS
 Rulea Sanga wa tatu kutoka kushoto nikiwa na kundi la Tambaza
 Rulea Sanga, kulia nikiwa na wadogo zangu wa kidato cha pili, wakati mimi nikiwa kidato cha tatu
 Rafiki yangu Tryphone ambaye aliruka na Division One kidato cha nne wa kwanza kulia
Nikiwa katika bustani yangu-NJOSS
 Kikundi kutoka Tambaza
 Rulea sanga wa pili kutoka kushoto nikiwa kidato cha pili na classmate wangu
 Nikiwa kidato cha nne, niliyechuchumaa

ANGALIA PICH

 Rafiki yangu niliyempenda sana wa kitaa, anaitwa sebastian. Huyu jamaa alikuwa kichwa sana Chuo Kikuu ila watu walimchezea akawa chizi. Ila kiingereza usimguse
 Nikiwa kanisani Mafinga kipindi cha likizo, niliyechuchumaa
 Katikati ni Rulea sanga nikiwa na rafiki zangu, Tryphone (kushoto) na Sanjigwa
 Nikiwa katikati na classmate, kushoto ni Onesmo Mhewa ambaye aligonga Division One kidato cha nne
 Nikipiga Basketball


Comments