RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAZISHI YA KARDINALI RUGAMBWA YAZUA JIPYA


Hayati Kardinali Laurean Rugambwa enzi za uhai wake.                         
Zikiwa zimebaki siku 10, kabla masalia ya mwili wa aliyekuwa Kardinali wa kwanza mweusi barani Afrika, Laurean Rugambwa, kuzikwa upya kwenye kanisa katoliki la kwanza mkoani Kagera, uongozi wa kanisa hilo umetoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioanza kunufaika na tukio hilo.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya wafanyabiashara katika manispaa ya Bukoba, kutengeneza fulana zenye nembo ya kanisa hilo na picha ya kardinali Rugambwa, ambazo zinauzwa kwa sh.12,000 bila ridhaa ya uongozi wa kanisa hilo.
Akizungumza na gazeti majira katibu wa kanisa katoliki jimbo la Bukoba, Padri Deodatus Rwehumbiza, alisema waumini ambao watanunua fulana zilizotengenezwa na wafanyabiashara hao bila baraka za kanisa hilo, watakuwa wamefanya makosa......
Limeandika Gazeti Majira.

Comments