Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.
Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi, dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.

Akizungumza na mtandao wa Global
Publishers baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema “Ushindi huu
niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na
Yesu na sasa amenijibu”.
Mara baada ya kushinda kesi hiyo lilizuka
timbwili lingine baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report
Book) akimtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa
viwanja. Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo
cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa
hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi
mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo
polisi alishindwa kumtia nguvuni.
source: Strictly Gospel
Comments