RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI WA JOYOUS CELEBRATION KUANDIKA HISTORIA WIKI IJAYO

Khaya Mthethwa akiwa jukwaa la Joyous Celebration.
Kundi la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini linatarajia kuandika historia nchini mwao endapo mwimbaji wao kijana Khaya Mthethwa aliyeingia kwenye top 2 ya shindano la Idols nchini humo atashinda shindano hilo na kuwa mweusi wa kwanza kushinda tangu kuanzishwa kwa shindano hilo nchini humo.

Mwimbaji huyo kutoka jimbo la Durban amefanikiwa kuingia Top 2 akipambana na mpinzani mwenzake   mwenye asili ya kizungu aitwaye Melissa kutoka Port Elizabeth, ambapo upigaji kura kwa washindanaji hao walioweza kuwabwaga wenzao zaidi ya 30 hadi kufikia hapo, unaendelea kwa kuongezwa siku zaidi hadi jumatatu tarehe 1 mwezi 10, ambapo waimbaji hao watakuwa na nafasi ya kuimba hapo kesho katika ukumbi wa Mosaiek Teatro.

Kijana huyo ameonyesha kipaji kikubwa katika shindano hilo na kujikusanyia mashabiki wengi nchini humo ambao wamekuwa wakishirikiana na kundi la Joyous kufanya kampeni mbalimbali ili watu wapate kumpigia kura hatimaye kuibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho ambacho watu wengi(weusi) wanataka kumpigia kura Khaya ili ashinde na kuandika historia nchini humo.
Wakati huo huo kundi lake la Joyous Celebration siku ya Jumamosi na Jumapili katika ukumbi wa Teatro Montecasino, linatarajiwa kugawa zawadi kwa mashabiki wake kwa kuimba nyimbo mpya na zazamani ikiwa pamoja na kuwaalika waimbaji waliowahi kuimbia katika kundi hilo awali ambao watapata kuwakumbusha wapenzi wao nyimbo walizowahi kuimba wakiwa na kundi hilo. Kati ya waimbaji ambao kuna uwezekano wakawepo katika onyesho hilo lililopewa jina la MTN Joyous Celebration Rewind, kuna Keke, Kgotso, Swazi,Pastor Patric Duncan, William Sejake, Nqubeko na mkewe Ntokozo na waimbaji wengine wengi.

Source:Gospel Kitaa

Comments