Kwa mujibu wa Sir Andy, ukiwa mwanachama wa Freemason hakuna kipato ama ongezeko la fedha lolote unalolipata. “There is no financial benefits, no no,” alisisitiza Sir Andy kwenye kipindi cha The Interview cha Clouds TV kilichoruka jana usiku.
Hiyo ndio ilikuwa ni pointi ya msingi kuifahamu kwakuwa watanzania wengi wameaminishwa kuwa baadhi ya watu wametajirika baada ya kujiunga na ufreemason, kitu ambacho kwa mujibu wa Sir Chande si kweli hata kidogo.
Katika kipindi hicho mzee huyo amesimulia mengi ya ndani kuhusiana na freemasonry na kuongeza kuwa hakuna kitu cha siri kwenye jamii hiyo.
“Hakuna kitu ambacho hujakisikia, ni kinyume kabisa ya mengi uliyokuwa ukiyasikia, kumbe mwisho wa siku kama alivyoelezea Mzee Chande, freemasonry ni kuhusiana na upendo, urafiki na ukarimu zaidi na kuitakia jamii mema na mambo ya aina hiyo,” alifafanua mtangazaji wa kipindi hicho, Gerald Hando.
There you have it!
Source: Vituko vya Mtaa
Comments