RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UZINDUZI WA ALBAMU YA JANA IMEPITA YA MADAM RUTH NA CHRISS UMEFIKA SASA

Kama wewe ni mshabiki wa mambo ya MUNGU umefika wakati wa kushabikia kazi ya Mungu ambayo imefanywa kwa kupitia vinywa vya waimbaji wa injili Madam Ruth na Chriss. Kila siku tunasema ya kuwa Mungu ana njia nyingi za kuongea na walio wake, anaweza kuongea kwa kupitia watu au kiumbe chake chochote alichokiumba, leo hii anataka kuongea na wewe kwa njia ya uimbaji. Sasa ili uweze kumsikiliza huyu Mungu kwa kutokosa katika uzinduzi huu.

Watumishi wa Mungu wameamua kufanya uzinduzi huu bure ili ujumbe wa Mungu ukufikie hata wewe ambaye ungeshindwa kuwa na kiingilio, mtihani ulioko kwako ni kutafuta nauli yako ya kukuwezesha kufika katika kanisa la KKKT Ushirika wa Kariakoo hapa jijini Dar es Salaam.

Madam Ruth na Chriss wamenawa mikono mbele za Mungu wanasubiria kula chakula pamoja na wewe siku hiyo ya tarehe 28/10/2012 saa 7:00 mchana. Pia kuna waimbaji wengi sana watakuwepo kama unavyosoma katika tangazo hapo chini.




Tangazo hili limetengenezwa na

RumAfrica
Simu +255 715 851523
Blogu: www.rumafrica.blogspot.com
Barua Pepe: rumatz2011@yahoo.com

Comments