RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE


ONYO: Unaombwa kujibu maswali kabla ya kuangalia jibu, ikishindika unaweza kuangalia jibu na kufananisha na kile ulichokijibu.

Mwezi huu na mwezi uliopita tulikuwa katika kitabu cha Luka, na bado hatujamaliza,  kwahiyo na mwezi unaofuata tutaendela na kitabu cha Luka. Tunakuomba usome kwa makini ili uweze kujibu maswali yetu

MASWALI
  1. (a) Yesu alitumia njia gani kumponya mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu wa miaka kumi na nne ambaye alikuwa hajiwezi kujinyoosha kabisa?

    (b) Kwanini mkuu wa sinagogi alimkasirikia Yesu kutokana na kitendo cha kumponya mwanamke mwenye pepo?

  2. Yesu alipokuwa akielekea Yerusalem alikutana na mtu mmoja aliyemuuliza, Je, Bwana watu wanaokolewa ni wachache? Yesu alimjibu nini huyo mtu?

  3. Kwanini Mafarisayo walimwambia Yesu aondoke mahali alipokuwa anahubiri Yerusalemu kwenda mahali pengine?

  4. Yesu anasemaje kuhusiana na mtu kukaa vitivya mbele unapokuwa umealikwa katika harusi?

MAJIBU
  1. (a) Yesu alimwita akamwambia, mama umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake naye akanyooka mara hiyo akamtukuza Mungu (Luka 13:12-13)

    (b) Kwasababu Yesu alimponya siku ya Sabato (Luka 13:14)

  2. Jitahidi kuingia katika mlango ulio mwembamba maana nawaambia mtu wengi wataka kuingia wasiweze. Wakati wenye nyumba atakaposimama nje na kubisha mlango, mkisema, Ee Bwana tufungulie, yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako, ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika nia zetu (Luka 13:22-30)

  3. Kwasababu Herode alitaka kumuua (Luka 13:31)

  4. Ukialikwa na mtu harusini, usiketi katika kiti cha mbele, isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahimili kuliko wewe akaja yule aliwaalika wewe nay eye na kukuambia mpishe huyu! Ndipo utakapoanza haya kushika mahali pa nyuma, Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyumailia jae yule aliyekualika, akwambie rafiki yangu njoo mbele ya wote walioketi pamoja na nawe kwa maana kila ajikwezae atalisdhiwa, naye ajiadhiye atakwezwa.


Comments