RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MUNGU KANIEPUSHA NA BALAA LA JANA KARIAKOO

Mwandishi: Rulea Sanga

Nayasema haya kutokana na kile kilichotaka kunikuta jana Kariakoo katika vurugu za maaskari na Waislamu. Jana niliondoka nyumbani kwangu na kuelekea Kariakoo kununua tshirts kwaajili ya ofisi yangu. Nilifanya kazi yangu salama na baada ya kumaliza niliingia katika gari na kuelekea ofisini Sinza. Nilifika ofisini kwangu muda wa saa 5:00 asubuhi. Na baada ya kufika ofisini kwangu, mida ya saa 7:00 mchana nikapigiwa simu na Mtume na Nabii John Komanya kuwa nitoke huko Kariakoo hali sio nzuri, Waislamu wamepamba moto, nikamjibu kuwa mimi niko Sinza.

Kitu nilichojifunza na kumshukuru Mungu ni kwamba, ukiwa na Roho Mtakatifu atakuongoza na kukuepusha na majanga na wale maadui wako. Mungu kwa kupitia Roho Mtakatifu aliniepusha na hilo janga kwa kunisukuma kurudi nyumbani na kutobaki Kariakoo. Nilipokuwa Kariakoo sikuwa na amani kabisa na sikupenda kuhangaika kutafuta tshirts katika maduka tofauti. Nilipofika Kariakoo niliingia maduka mawili tu na kupata kile nilichokuwa nataka kununua na baada ya hapo nikafunga safari ya kurudi Sinza.

Kwangu huu ni ushuhuda tosha na ninaamini Mungu wangu atazidi kunionyesha wale wabaya wangu katika jina la Yesu. Nakushauri na wewe ndugu yangu, muda wote tamani kutembea katika uwepo wa Mungu na kuwa mtu wa maombi. Kila unapotaka kwenda omba kwanza ili Mungu akulinde na maadui. Ulimwengu umeharibika, hali ya udini inaanza kuingia nchini kwetu, tuwe macho watu wa Mungu.

Nikutakie siku njema na sema Neno Moja tu juu ya Amani ya Tanzania.

AHSANTENI:

Comments