Dotnata katika pozi. |
Mwigizaji na aliyewahi kuwa Mwanamuziki Dotnata Posh, amesema kwa sasa
ameaokoka kabisa na kuamua kufungua kanisa kubwa lengo likiwa
kuwashawishi wasanii wenzake kuachana na maasi na hatimaye kumrudia
Mungu.
Dotnata ambaye alianza kwa kufafanua jina lake, alisema watu wengi wamezoea kumwamwita jina hilo bila kujua msingi wake, kwamba yeye jina lake ni Doto na ameunganisha na jina lake la ubatizo Illuminate ambapo akachukuwa jina la kwanza la Dot na kuunganisha jina la mwisho na nate na kupata Dotnata.
Dotnata anasema aliamua kwenda Nigeria kwa Mtume T.B Joshua ambaye ni maarufu sana Afrika na Dunia nzima, ili kwenda kuchukua baraka kwaajili ya kuanzisha Kanisa hilo. Alisema baada ya kurudi kutoka Nigeria na kupata baraka hizo za kufungua kanisa, hivi sasa anasomea masomo ya Biblia ili baadae aje kuwa Mchungaji. Kwasasa yeye ni Mama wa Kanisa.

T.B Joshua wa Nigeria. |
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa, kwa sasa kanisa lake litakuwa na
wahubiri kutoka Nchi mbalimbali na baada ya hapo ataanza kutoa elimu kwa
wasanii waweze kuokoka ili kumrudia Mungu.
Dotnata pia amesema kwa sasa hawezi kumlaumu msanii ambaye anafanya
mambo ya ajabu ajabu kwakuwa anaamini ni ujana unamsumbua na ukifika
muda atabadilika.
Alizidi kusisitiza kuwa katika Kanisa lake anategemea pia kuwachukua wasanii Ray C na Asha Madinda, ambao nao wameokoka. Mwisho alimalizia kwa kusema Kanisa hilo kwa hivi sasa lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili, ingwa pia limeruhusiwa kuendelea na kazi zake za ibada
source--Bongo Unit. and Gospel Kitaa

Comments