Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedict wa 16, ameteua
makardinali wapya 6, kutoka nchi za Lebanon, Nigeria, Marekani,
Ufilipino, Colombia na India, huku makao makuu, Roma wakikosa mtu.
Uteuzi huu wa viongozi hawa wa ngazi ya juu ambao ndio wenye mamlaka ya
kuchagua mrithi wa papa, umefanyika leo Jumatano 24 Oktoba, ambapo Papa
alikuwa na hutubu katika mikutano yake ya kila wiki, ambapo alilitoa
tangazo hili kwa kustukiza bila watu kutarajia.
Tazama viongozi hawa ambao watapandishwa rasmi tarehe 24 Novemba 2012, kuwa makardinali.
|
Archbishop John Olorunfemi Onaiyekan wa Abuja, Nigeria |
|
Archbishop Luis Antonio Tagle wa Manilla, Ufilipino |
|
Archbishop Ruben Salazar Gomez wa Bogota, Colombia |
|
Archbishop James Harvey (kushoto) wa Mareani akiwa na Papa Benedict XVI |
|
Archbishop Bechara Boutros Rai, wa Lebanon |
|
Archbishop Baselios Cleemis Thottunkal, wa India |
|
Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedict XVI |
|
|
|
Uteuzi huu umefanya Ulaya kuwa na jumla ya makardinali 62, Latin America 21, North America 14, Asia 11, na Afrika 11.
Comments