Namshukuru sana Mungu wangu kwa kunipa chakula cha kiroho kupitia kwa
Mtume na Nabii Josephate Mwingia wa kanisa la Efatha Mwenge lililoko wilaya ya
Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam katika nchi ya
amani Tanzania.
Nimewahi kulishwa vyakula na watumishi wa Mungu katika makanisa mbalimbali lakini siku ya jana kwangu ilikuwa ya pekee. Nilifurahishwa na kubarikiwa sana na huduma inayotolewa katika kanisa lile. Chakula kilikuwa kitamu sana mpendwa na ningependa na wewe upate angalau kidogo ya kile nilichokula.
Namuomba Mungu akusaidie kuelewa kile ambacho nimekiandika kutoka madhabahu ya Nabii Josephate Mwingira. Pale ambapo hutaelewa naomba unisamehe na omba Roho Mtakatifu akufungue ili uelewe.
Chakula cha Jumapili hii ilikuwa ni mwendelezo wa chakula cha wiki iliyopita, Somo lilikuwa:
ROHO WA BWANA YU JUU YANGU.
Roho wa Bwana yu juu yangu kwa kuwa amenitia mafuta. Soma Zaburi 45:7.
Tusome pia Wakoritho 1:12:4 Basi pana tofauti za karama, bali Roho ni yeye yule, Tena pana tofauti ya huduma, na Bwana ni yeye yule, Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendae kazi zote katika wote.
Katika kitabu hicho cha Wakoritho tunaona kuna makundi matatu
KUJUA NENO
Tusome Yeremia 23:28- Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na Neno langu, na aseme Neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA.

- Karama
- Huduma
- Kazi
Na makundi haya yote
matatu, Bwana ni yeye yule. Katika dunia kuna watalaam wa hali ya hewa ambao
wanajua mambo ya mwezi, sayari, nyota n.k. Kuna watalamu wengine wa udongo
wanaojua undani wa maji, ardhi n.k na wengine ni watalaamu wa nguvu mbalimbali
kama vile nguvu za umeme, mabomu, kompyuta n.k na wote hawa tunawaita
wanasayansi.
KAZI
KAZI
Tunatakiwa kutambua
kuwa Roho wa Bwana yu juu yetu kwasababu ametutia mafuta kwaajili ya kazi yake.
Mafuta tuliyopakwa na Bwana ni kwaajili ya kufanya kazi yake na sio kwaajili ya
kuyahifadhi. Mungu anapenda kuona watoto wake wanafanya kazi na sio kuwa watu
wa kupokea tu baraka kutoka kwa watumishi wao bila ya kufanya kazi.
HUDUMA
Tusome Waefeso 4:12- Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe. Kubaini utendaji wa vitu Fulani. Ili uweze kuumba huduma kunahitaji watu ambao ni watenda kazi. Kuna watu Mungu amewapaka mafuta duniani na amewapa mafuta ya kufanya kazi ili huduma itokee na baadae karama itokee. Watu walio wengi wameishia kwenye karama na wachache kwenye huduma na wachache zaidi kwenye kazi. Tunatakiwa kuwa watu wa kufanya kazi ili baadae tuwe watu wa huduma na hatmaye kutumia karama zetu katika kazi ya Mungu. Walio wengi wanapenda kufanya huduma na wanakimbia kufanya kazi ya Mungu. Eliya aliambiwa na Mungu awapake mafuta watu ili wakafanye kazi. Kuna baadhi ya watu Mungu amewapaka mafuta ili wakafanye huduma.

Tusome Luka
4:18-Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini
habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu
kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa.
Makusudi ya kuwa na Roho wa Bwana ndani yetu ni ili:-
Makusudi ya kuwa na Roho wa Bwana ndani yetu ni ili:-
- Maskini wasikie habari njema
- Wafungwa wapate kufunguliwa
- Vipofu wapate kuona tena
VIPOFU WAPATE KUONA
TENA
Tunapozungumzia upofu
tunamaanisha dhambi. Dhambi inapofusha watu wanashindwa kuona yaliyo mema na
wanabakia kutenda maovu na machukizo mbele za Mungu. Unapokuwa na Roho wa
Munguanakuondoa ule upofu wa kutenda dhambi na kutamani kufanya kazi ya Mungu
Tusome Wakoritho 1:2:9- Lakini kama ilivyoandikwa. Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu), mambo ambayp Mungu aliwaandikia wampendao.
Tusome Wakoritho 1:2:9- Lakini kama ilivyoandikwa. Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu), mambo ambayp Mungu aliwaandikia wampendao.
Tunaposema vipofu
wapate kuona tena tuna maanisha kuwa ni ile hali ya kumjua Mungu na kuwa katika
hali ya utakatifu.
Kuna mamabo ya kuzingatia katika kufunguliwa upofu:-
Kuna mamabo ya kuzingatia katika kufunguliwa upofu:-
- Mtu anapata kuona maovu.
Ili mtu aweze kuona maovu ni lazima
- Kulijua Neno
- Kujua ni wapi Neno lilipo
- Ni nani analo hilo Neno
KUJUA NENO
Tusome Yeremia 23:28- Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na Neno langu, na aseme Neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA.
Hapa tunaona ya kuwa
kuna wengine wana ndoto na wengine wana Neno. Sio kila mhubiri ana Neno bali
wana ndoto. Mhubiri alipooka alioteshwa ndoto ya kuwa mhubiri lakini hakupewa Neno
la Mungu kuwa mhubiri. Na hii inatoka na mtu kutamani kuhubiri wakati hana Neno
la Mungu na hajaitwa na Mungu kufanya kazi hiyo ila ametamani kuwa mhubiri kwa
kuona watu wengine wanahubiri. Wale wenye ndoto ni wale wanakurupushwa na Mungu
kufanya huduma kama vile Eliya
KUJUA NI WAPI NENO LILIKO.
Tunapataje Neno la Mungu? Neno la Mungu tunalijua kwa kufanya yafuatayo:
KUJUA NI WAPI NENO LILIKO.
Tunapataje Neno la Mungu? Neno la Mungu tunalijua kwa kufanya yafuatayo:
- Kusikia. Soma Warumi 10:14
- Kusoma. Soma Luka 1:3
Neno la Mungu
linapoingia ndani yetu linaumba pumzi ndani yetu ili kuleta uhai
Tusome Mwanzo 2: Mungu alipomuumba mwanadamu alichukua udongo
na kuupa pumzi na mwanadamu akawa hai. Pumzi inapoingia kwetu, siri ya Mungu
inafichuka. Uhai unasababisha kujua kuelewa siri.
Tusome Wakoritho
1:2:10- lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote,
hata mafumbo ya Mungu. Mungu hutufungulia mafumbo yaliyofichika na ya
sirini ambayo ni ya Mungu wetu. Kuna mambo mengine kwa akili au uwezo wa
binadamu ni ngumu kuyajua ila ukiwa na Roho wa Mungu utayajua hata
yaliyofichika na Mungu.
Tusome Ufunuo
10:10: Mungu pamoja na kuwa ameficha yaliyo yake bali hufungulia kwa Roho
wake. Kuna watu Mungu amewakirimia ya siri ili wapate kuona, kwahiyo wanapaswa
kusikiliza yule aliye na Neno lake
kwa kuwa na macho ya
kuona na baada ya hapo unapata yafuatayo:
- Pumzi
- Ya sirini
- Kuingizwa ufalme
- Unapokea ahadi zake
- Unaweza kutumia nguvu zake
Mungu anaruhusu ahadi
zake kutimiliza ahadi zako unapofikia hatua ya kujua siri. Tusome Wafilipi
4:13- Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Unayaweza mambo yote baada ya kuona siri za Mungu zimekuwa wazi kwako na hakuna kuning’inizwa tena na shetani. Ili kujua siri za Mungu unatakiwa kujikana na kujinyima
na usikosekane katika ibada za kanisani kwako. Unapotaka kuzitumia zile nguvu
za Mungu ili ziweze kufanya maajabu.
NANI ANALO HILO NENO AU NANI KABEBA
NENO LA ROHO
Unapata kujua kuwa
Roho wa Mungu ni zawadi na kazi yake ni:-
- Kukufanya uwe wa tofauti na wengine
MUNGU AWABARIKI
TUTAENDELEA WIKI
IJAO
Comments