RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA YAFAIDIKA NA NENO LA MUNGU KATIKA IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA . SOMO LILIKUWA “ROHO WA BWANA YU JUU YANGU”



Mungu amekuwa mwema kwangu, Jumapili hii kama ilivyokawaida yangu, blogger wenu Rulea Sanga nilihudhuria Ibada ya Jumapili katika kanisa nilipendalo la Efatha liliooko Mwenge jijini Dar es Salaam. Nilibarikiwa sana na somo la Mtume na Nabii Josephate Mwingira kwa somo alilotufundisha watoto wake. Na hivi ndivyo alivyoaanza


Mtume na Nabii Josephate Mwingra (kushoto) akiwa na Nabii T.B. Joshua wa Sinagogi ya SCOAN Nigeria

Tusome Luka 4:18, Roho wa Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini. Roho wa Mungu anapatikana kwa kutiwa mafuta na kutangaza wafungwa kufunguliwa kwao ili wapate kuona tena kwa waliosetwa kuwaweka huru. Kifungo cha shetani kinatolewa kwa kusetwa baada ya kupata macho ya kuona mema na mabaya.

WAFUNGWA WAPATE KUONA TENA
Hapa ndipo tutakaposimamia katika somo letu la leo. Unaweza kuunguruma kwa rafiki yako na akakimbia kwaasababu umetiwa mafuta. Kipofu inaweza iakamaanisha yafuatayo:

Kipofu kwa lugha ya kawaida ni kutokuwa na macho ya kuona. Unaposhindwa kuona yale yanayokuzunguka tunasema huyu mtu ni kipofu.

Kipofu ni kukosa ufahamu, kama vile kushindwa kufundisha. Mtu anaposhindwa kujua baadhi ya mambo yanayomzunguka, tunasema mtu huyu ni kipofu wa ufahamu, kwa maana hiyo hajui mambo yanayompasa kuyajua.

Kipofu ni kukosa kuwa na elimu. Mtu anapokuwa ameshindwa kwenda darasani ili kujifunza yale yanayompasa kujifunza kwaajili ya maisha yake na kusaidia jamii, mtu huyu anakuwa ni kipofu wa elimu, tukimaanisha kuwa ana giza linalomzunguka katika suala la elimu. Pia mtu huyu anaweza akaitwa ni mjinga.

Kipofu ni kuwa mpumbabu. Mtu wa aina hii ambaye hajitambui la kufanya na kama anatambua la kufanya ili limsaidie au lisaidie jamiii, nay eye akalipuuzia na kufanya yasiyotakiwa tunasema ni mpumbavu.

Kipofu ni bumbuazi wa moyo

Leo tutazungumzia upofu kwa maana hii,
Tusome Zaburi 119:11 Upofu ni ile hali ya dhambi. Dambi yaweza kukupa upofu kwa kutojua yale unayoyatenda kuwa ni sahihi au sio sahihi mbele za Mungu. Dhambi inaweza kukutesa kwa kutoona njia ya uzima ambayo ndio Yesu anataka watu wake tupite kufika mbinguni kwa Baba.

Tusome Yohana 14, Dhambi hupofusha macho ya kiroho na kuwa kipofu wa kutotambua jema na baya, na mara nyingi ukawa ni mtu unayeona maovu kwako ni mema na kutoona mema kuwa ni mazuri mmbele za wanadamu na mbele za Mungu.


Kwaya ya kanisa la Efatha Mwenge

Katika nchi yetu ya Tanzania kuna bbadhi ya viongozi wamekuwa vipofu na kutoangalia maovu yanatokea katika nchi yetu. Kumekuwa na vurugu nyingi za kisiasa na za kidini zikiendelea hapa nchini na viongozi wamaekaa kimia. Viomgozi wamekuwa wala rushwa wakubwa sana, na vurugu hizi zote zinatokana na viongozi kuwa na dhambi.Viongozi wetu hawa wanahitaji kufanya toba ili kuungama dhambi ya rushwa inayoendelea nchini Tanzania. Viongozi wenye haki mara nyingi ni viongozi ambao wanachukia maovu kutokea katika nchi yao.
Kuna kipindi mabomu yalitokea Mbagala viongozi wetu walibaki kimia na wengine walidiriki kusema “Mbona waliokufa ni wachache sana” Kwahiyo inaonyesha viongozi hawa wangetamani watu wafe wengi ndipo wangeshtuka. Hii inaonyesha kuwa viongozi hawasikii maumivu ya wananchi wao.

Hatuwezi kupambana na mapepo ila tunaweza kufukuza mapepo, na sisi tumejipanga kufukuza vipofu wote madarakani na sio kukemea mapepo yao. Mwenye dhambi ni yule ambaye haoni makosa yakitendeka nah ii imeingia serikalini ambapo viongozi wamekuwa wala rushwa na hawaoni kuwa ni kosa wanafanya mbele za Mungu.

Kaman chi imejaa rushwa basi hata viongozi watakuwa wala rushwa wakubwa na rushwa hiyo inapotosha macho ya viongozi kuona mbele. Viongozi wamekuwa watu wakujifaidisha kwanza wao na kusahau wale waliowachagua na kuwaweka madarakani.

Leo hii Waislamu wanapigana na Wakristo na tunajiuliza na Wakeisto nao wakiamua kuyarudisha mashambulizi, je, Tanzania itakuwa wapi?

Mwenye dhambi na mla rushwa wote ni wapumbuvu. Watu wa siasa waliaanza kupiga makanisa na sasa suala hilo limeenda katika udini. Efatha tunapinga vita vya kidini kwani tunatambua ya kuwa kuna Waislamu ambao ni ndugu zetu na tunaishi nao mitaani na tunaazimiana vitu, leo hii tukianza vurugu hizi, basi tutauana ndugu kwa ndugu.

Efatha inawatangazi wale wote watakao kuja Efatha kupambana na sisi tutawacharaza bakuora kwani hao watakuwa wametumwa na watu kutoka serikalini ili kuanzisha vurugu. Tukiwajua wanaowatuma tutabanana nao.

Viongozi wa Tanzania wamezoea kuiburuza Tanzania kwa maovu, lakini sasa sisi tumelewa na hatutakubaliana kabisa. Amani ya Tanzania hailetqi na wanasiasa ila na Mungu mwenyewe. Wakati wa kukaa na majambazi umeisha na tuko macho kumpambana, uwezo tunao. Wanaoanzisha vita kwa njia ya majini tunatangaza vita.

Ukiwa na nguvu ya Mungu unatembea kifua mbele. Na sisi tuna nguvu ya Mungu ndio maana tunasema haya kwa kujiamini. Utawala wa wenye dhambi kwa sasa umekwisha na tunasema yatosha!!.

Mnakumbuka kipindi cha Kikombe Loliomdo na Sheikh Yahaya, nilisema kazi zao hazitadumu na leo mumeshuhudia, yote yaliyokuwa yakifanyika yamekwisha tena kwa aibu. Utawala wa kipepo umekwisha na sasa ni utawala wa Nabii Josephate Mwingira na Mungu.

Mwana akiwa mdogo huonekana kama mtumwa kwani amli yake imeshikiliwa na wakili wake, na mwana akikuwa huachiwa mali zake kwani anaufahamu na anaelewa jinsi ya kuitumia mali zake.

Tusome Zaburi 119:130, Ukiyafahamu maneno ya Mungu, yanakuondoa katika upofu. Unaposoma Neno la Mungu kila siku na kulielew vizuri na ukaamua kulifanyia kwa vitendo, utakuwa umeondolewa upofu kwasababu kwa kupitia Neno utajua jema na baya
Tusiwe na mawazo ya dhambi na kusema hufai kutokana na jyale mabaya yanayokuzunguka, kumbuka Mungu alisema wewe ni kiumbe chema

Tusome Yohana 1:1-5, Pasipo Mungu hakuna kitakachofanyika. Ukiona mtu hastawi, hana Neno la Mungu, achana na wezi au wala rushwa, ila kuwa na wale wenye hofu ya Mungu. Kama mtu wa Mungu, baraka unazopata inapasa ufurahie na sio zikuumize. Kuna watu wamebarikiwa na kuwa na kila aina ya vitu na wanauwezo wa kula chakula cha aina yoyote, alkini wameambiwa na baadhi ya vitu wasile, na matokeo yake hawafurahie utajiri walionao. Watu wamepewa masharti ya kula vyakula kutokana na matatizo yanayowasumbua>

Unapaswa kama muumini kuwaheshimu sana wapakwa mafuta lwani wanauwezo wa kukuanda madarakani na kuwa kiongozi mzuri na usiyependa rushwa.

Ziko mamalaka ambazo hazifungamani na tawala zingine ila zinatoa amri katika mamlaka zingine.

Neon likiwa ndani yako yafuatayo hufanyika:
  1. Kusaidia kuonyesha njia
  2. Chakula chako kinakuwa Neno la Mungu
  3. Kusababisha kujua cha kufanya katika maisha yako
  4. Huonyeshwa kizuri na kibaya na hivyo hupata mwanga
  5. Kujua mazingira halisi uliyonayo (utajitambua na kufahamu majukumu yako)
  6. Neno linakuongoza kujua nguvu ulizonazo
  7. Linakupa kupambanua mambo na kuyabaini

Tusome Isaya 9:9:2 watu waliokaa katika giza wameona Nuru.Ukitaka kuwa na nuru unapaswa kuokoka, kaa darsani ufunguliwe na mmbo ya rohoni. Unapaswa kubatizwa kwa maji ili uweze kufa na Kristo na baadae kufufuka na Kristo. Unapobatizwa unashurutishwa na mwili na kuunganishwa na Kristo

Tusome Wakoritho 2:5:17-9 Unapofika mahali na kuona mateso yaw engine, na ukiona hivyo chukua hatua ya kuwaleta watu kwa Yesu, kwani unawaleta kondoo waliopotea

OMBI: Nawaomba mkaniletee kondoo waliopotea!!!

MUNGU AWABARIKI

Comments