Huu ni wakati wa kufanya kazi ya Mungu. Kama wewe unavyopenda mtu akufanyie kazi nzuri, ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, naye anapenda kuona wewe unafanya kazi yake kwa uaminifu na kwa bidii. Tuache tabia ya kuwa wavivu katika kufanya kazi ya Mungu. Unaweza kujiiuliza ni kazi gani hizo? Kazi kubwa kuliko zote ni kuwaleta watu kwa Yesu kwa kuwapeleka kanisani na kuwafundisha iliwaweze kufanya mema na kuachana na maovu. Pia kusaidia wenye uhitaji katika maisha yao.
Mungu amekuwa mwema katika maisha yako na wewe ni shahidi, amekuepusha na mengi na bado anakulinda mpaka sasa. Pale unapokuwa na njaa Mungu anahangaika kukutafutia chakula na mwisho wa siku tumbo lako linapata hitaji lake. Kuna kipindi unahitaji faraja wakati wa mapito yako magumu, Mungu anakupa faraja. Na ni mengi Mungu anafanya kwako na mengine huyaoni kwa macho, ila yanafanyika.
Kuna kipindi huwa nafikiria sana, leo hii Mungu aamue kutunyima hewa kwa muda wa dakika 15, unafikiri utakuwaje?. La msingi kwako ninakuomba sana ujitahidi kufanya kazi ya Mungu kwa kutumia karama ambayo Mungu amekupa kufanya kazi yake. Huu ni muda wa kufanya kazi ya Mungu, utafika muda utashindwa hata kutoa sauti na kuwa tegemezi. Usipende kuchangua ni akzi gani ya kufanya katika nyumba ya Bwana kwani kuna kazi nyiingi sana ambazo zipo kanisani ambazo unapaswa kufanya. Tuache tabia ya kutaka kazi nzuri za kanisani na zile mbaya kuawaachia wengine. Yesu hakuchagua kazi ya kufanya ila alifanya ile ambayo aliona inambariki Baba yake.
Wachungaji tunawaombeni msipende kushindana wenyewe kwa wenyewe na kusemezana mabaya, wote tunamtafuta Mungu mmoja. Kumekuwa na maneno ambayo hata sisi waumini wenu mnatushangaaza na kufikiri kuwa labda mnagombeneana waumini. Tuwalishe watoto chakula chema kutoka kwa Mungu na tuache kugombeana watu. Kuna watu wengi sana vijijini hawamjui Mungu na wanaamini miungu yao. Kama mchungaji unawajibu wa kukimbilia huko kijijini na kuwaokoa watu wa Mungu, na tuache kubanana mjini na kugombeana waumini ambao mwenzako kafanya juhudi kuwapata. Naomba mniwie radhi kama nimeenda kinyume na maadili yenu.
Nikutakie kazi njema

Comments