RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

IBADA YA UPAKO WA MAFUTA YAFANYIKA KATIKA KANISA LA NABII FLORA - [KANISA LA YESU LA HUDUMA YA MAOMBEZI]

Bwana Yesu Asifiwe…God is Good ... All the Time!!! Nawapenda kwa jina la Yesu..Amen..

Nabii Flora Peter akiombea mafuta ya upako kabla ya kuanza zoezi la kuwapaka waumini wake.

Tusome Yakobo 5:13. Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya, mtu wa kwenu amepatikana na mabaya na aombe na aombe akiwa na moyo wa kuchangamka, ana moyo wa kuchangamka na amwimbie Bwana Zaburi, mtu wa kwenu amekuwa hawezi na awaite wazee wa kanisa nao wakuombee na kupakwa mafuta kwa jina la Bwana. Na kwa kuomba kwa imani kutamuokoa mgonjwa yule.

Kuna watu wengine wanasema kupakwa mafuta sio mafundisho, wambie huo ni ushamba wa kiroho, wewe wambie “shughuli hii ya kupakwa mafuta inanihusu mimi na sio wewe”.  

Nawatabilia kuwa kuna watu wataenda kufanikiwa kutokana na mafuta ya leo, na kila kitu unachokiona kitasujudu siku ya leo katika ibada hii,  na hiyo miti itasujudu kwa jina la Yesu. Mungu leo ananambia kuwa kuna watu wenye kansa 300, UKIMWI 300 na hakuna watu wenye pesa ila kwa imani leo pesa zitadoka kwa jina la Yesu, kuna watu 300 hawana ajira na umetuma “Application letter”…naomba useme “Shughuli inanihusu mimi”  kwa jina la Yesu.

Bwana anasema kama unaugonjwa wowote ule na uchumi wako umeyumba, ndoa yako iko CO haina amani, Bwana anasema tutakutia mafuta na mambo yatakuwa sawasawa kama zamani na zaidi, kuwa na imani na mafuta ya nabii wako. Na ukitiwa mafuta ugonjwa wako utakuwa mbali na wewe, ukipakwa mafuta UKIMWI wako ni kwaheri tena, Una mikosi, hujaolewa, kila kitu ambacho ukifanya hufanikiwi, leo ni kwaheri. Naomba siku ya leo ubadilishe maisha yako ya kuteseka na njoo kwa Yesu. Kusudi la MUNGU lazima lifanikiwa kwa jina la Yesu.

Tusome Kutoka 30:31, Kama utanena na wana wa Israel, na kuwambia, Haya yatakuwa mafuta Matakatifu ya kutiwa kwaajili yangu mimi katika vizazi vyenu vyote. Hayatamiminwa katika kiwiliwili cha binadamu, wala msifanye mengine kwa mfano kama haya yaliyoungwa kwa viungo vyake, ni matakatifu, na kwenu ninyi yatakuwa matakatifu. Mtu awaye yote atayachanganya mafuta mfano wa haya, au mtu awaye yote atayatia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atakataliwa mbali na watu wake.

Watakatifu wa MUNGU tukae katika sifa, kwa maana hautakosa chakula na ujijue kuwa shughuli hii inakuhusu wewe…na sio mwenzako kwa jina la Yesu. Na hutaishi katika nchi ya ukame.

Baada ya uatbiri kuisha Nabii Flora alianza zoezi la kuwapaka mafuta waumini wake kama unavyoona katika picha hapo chini:


Ukiwa karibu na Nabii Flora Peter unapata raha ndani ya Yesu kutokana na jinsi Yesu anavyomtumia
Nabii Flora Peter akiwabariki waumini wake kanisani

Baadhi ya waumini wakifurahia ibada ya Jumapili yenye upako wa ajabu
Nabii Flora akiombea maji ili Mungu aachilie upako
Nabii Flora Peter akimbariki mtoto mdogo.
Nabii Flora ni mpenzi wa watoto kama unavyomuona
Mtoto huyu alifika kwa Nabii Flora Peter kupata uponyaji
Ukiwa na Yesu ni amani ndani ya moyo wako

Kanisani


Unaweza kufika kanisani kwa kupanda magari yanayoelekea Mbezi Beach na shuka katika kituo cha Salasala na uliza kanisa letu au piga simu. +255 716 310661 au unaweza tembelea blogu yetu www.nabiiflora.blogspot.com.

Comments