RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFATHA LAFANYA MAMBO YA AJABU KATIKA IBADA YA JUMAPILI




Blogger wenu Rulea Sanga namshukuru Mungu sana kwa kunipa kibali cha kufika katika kanisa la Efatha Mwenge na kusikia ujumbe kutoka kwa Mungu kwa kupitia Mtume na Nabii Josephate Mwingira. Ngoja nikupe kile ambachonilikipata na kuandika katika Notebook yangu ili na wewe upate kubarikiwa.

Mtume na Nabii Josephate Mwingira aliyeshika mic wa makanisa la Efatha
UTANGULIZI
Kabla ya ibada ya kuanza kulikuwa na muda wa kusalimiana, kuimba nyimbo za tenzi, maombezi na baadae matangazo

MATANGAZO
Kulikuwa na matangazo mbalimbali kama ya ndoa, siku za madarasa ya kukulia wokovu, kambi ya vijana kufanyika kibaha, Wanakamati kukutana Kibaha, Workshop kwa wanavyuo kufanyika Kibaha, kubariki ndoa, wanakamati wa afya na mazingira kukutana Nuru Centre, wamama kukutana Nuru Centre, darasa la kukulia wokovu kuanza Jumatano, alhamisi na Ijumaa kanisani Efatha kuanzia saa 10;00 jioni na mwalimu ni Nabii Josephate Mwingira.

MUWAKILISHI WA BODY YA EFATHA SEMINARY
Mwakilishi wa body ya Shule ya Seminari ya Efatha Bagamoyo alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na Shule ya Efatha. Alisema Biblia inasema mkamate sana elimu usiache aende zake. Kusudi kuu la Nabii na mtume  Josephate Mwingira kuanzisha shule hii ni kumjenga mwanafunzi kiroho na maisha ya kawaida.

Sifa za Seminari ya Efatha ni kama zifuatazo:
  • Kuna shule nzuri sana Tanzania lakini ya Efatha ni nzuri zaidi
  • Kunatolewa elimu ya kawaida na mambo ya kiimani. Kitu unachofundishwa katika somo fulani linalinganishwa na Neno la Mungu katika Biblia. Kama unafundishwa jicho litalinganishwa na nini Mungu anasema kuhusu jicho.
  • Shule yetu iko Bagamoyo na ina eneo kubwa sana la ekari 45 na kuna viwanja vya michezo vya kutosha.
  • Kuna miundo mbinu bora kama maji, umeme, barabara n.k.
  • Tunafundisha kidato cha kwanza mpaka cha nne
  • Shule hii ni ya bweni, vijana wanalala na kula hapo hapo shuleni.
  • Tuna maktaba nzuri sana
  • Mahabara ni ya kiwango cha juu sana
  • Malezi yetu ni bora kwani tunaye mwalimu aliyeokoka na mwenye hofu ya Mungu anayesimamia wanafunzi kufanya yaliyomema machoni pa watu na machoni pa Mungu. Mwalimu huyu ni mchungaji na ni Professional Canceller
  • Walimu wanakibari cha Mungu
  • Ada yetu ni ya kawaida ukilinganisha na huduma wanayopata vijana wetu.
  • Mawasiliano yetu ni +255 595902 / + 255 754 271109  / + 255 689 3019142


UNABII KUTOKA KWA MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA KUHUSU SHULE YA SEMINARI YA EFATHA BAGAMOYO.

Unaweza kupeleka mwanao katika shule rahisi na inayolipa ada kidogo, lakini vijana wakaharibiwa. Mimi naogopa kuona wanao wanaharibikiwa. Watoto wangu kama nabii wanasoma katika shule hii. Usiogope gharama kwani hata kwenda mbinguni kuna gharama, Yesu alikufa kwaajili ya wewe kuokolewa kwahiyo wokovu ni gharama pia. Kama mtume na Nabii naamini waliofanya mtihani mwaka huu wamefanya vizuri kwa jina la Yesu, na wa mwakani watafanya vizuri zaidi ya mwaka huu.

Ili shule iweze kufanikiwa inahitaji hekima na mazingira mazuri kwa wanafunzi kufanya masomo yao kwa amani na furaha.

UTOAJI
Katika ibada hii ya Jumapili kulikuwa na utoaji wa sadaka katika bahasha, watu walimiminika katika kumtolea Mungu. Watu wamekuwa waaminifu sana katika suala la utoaji, kwani wanaamini kuwa ukimtolea Mungu utabarikiwa.

NENO KUU LA JUMAPILI KUTOKA KWA MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA.
Ujumbe wa Jumapili hii ulikuwa ni mwendelezo wa ujumbe wa jumapili iliyopita. Kanisa la Efatha kwa mwezi huu limesimamia katika Neno la Mungu linalosema, “ROHO WA BWANA YU JUU YANGU”

Roho wa Bwabna yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Kuna mabo muhimu ya kuangalia katika neon hili
  • Kuwafungua waliofungwa wapate kuona tena
  • Kutangaza mwaka wa Bwana
  • Kuwafungaua vipofu wapate kuwa huru
  • Kuondoa hali ya upofu unaoletwa na dhambi au mazingira mabaya
  • Kuhubiriwa habari njema zinazoleta tiba.

Tusome Ayubu22:21, Mjue sana Mungu na huwezi kumjua Mungu kama wewe mwenyewe humjui. Huwezi kumpata usiyemjua. Ili umjue Mungu unamtafuta yule anayemjua Mungu kwasababu atakutambulisha kwa Mungu ili umfahamu na mfamiane. Utajua umuhimu kwa yule aliyetumwa na Mungu kwaajili yako. Amani ya Mungu mara nyingi inakusaidia wewe kustawi.

Ukishamjua anayekujua Mungu itakuwa rahisi kwako kumjua Mungu. Ndio maana huwa nasema ya kuwa sio kila kitu naweza kukionyesha hapa kanisani bali tukikusanyika katika kambi yetu ya Kibaha utapata kuyasikia yote.

Kuna wengine wanamjua sana Mungu kuliko Mungu, nikimaanisha wanamjua sana Mungu na Mungu hawatambui kutokana na matendo yao mabaya. Mungu ndiye asili ya yote.

Tusome Ayubu 22:28, Ukimjua Mungu utaona mema yake. Ukifika mahali pa kumjua Mungu, hata kuazimia kununua gari, kujenga, kuoa utafanikiwa na hakuna atakayekuzuia.

Tusome Zaburi 1:1-3, Anayemjua Mungu atakusababishia na wewe kumuona Mungu. Kuna watu walimuomba Yesu awaonyeshe Baba yake. Na sisi Efatha tunaye Baba ambaye ni Nabii Josephate Mwingira, tunamwita Baba kwasababu yeye ni Baba yetu wa Kiroho.

Ukijitenga na waovu, wenye dhambi na mizaha utaanza kutafakari sheria ya Mungu na kupenda kufanya yaliyo ya Mungu kwani hakuna kipingamizi juu yako. Na ukifanya hivyo na Mungu atakufanyakatika ufalme wake na baraka zake zitakumiminikia. Utafikia kipindi ambacho jana yako haitanyauka tena. Ukisudia neon na Neno lako litadhibitika kwako. Pale unapoona leo una pesa na kesho huna hiyo ni dalili ya kunyauka. Ukitaka kuwa na fedha muda wote, ishi kwa kumwangalia Mungu. Watu wanaanza kufanikiwa katika kanisa la Efatha kwasababu wanaishi kama Mungu anavyotaka.

Tusome Mwanzo1:1-3, Kipindi hiki ni kipindi cha Mungu kuruhusu useme jambo na jambo litendeke. Mungu naye alisema jambo na dunia ikafanyika kuwa dunia na vitu vyake vyote. Ulipookoka bado wachawi na dhambi zilikusonga na kukuzunguka lakini hapo si mwisho wa wewe kushindwa na kuacha wokovu wako. Unatakiwa kutamka neon na neon linaenda kufanyika katika jina la Yesu.

Ukweli ni kwamba, Mungu kama Mungu haziakiwi, unachopanda ndicho unachovuna. Mpe Mungu uhai wako naye atadhibitisha uhai wako. Mungu anapotamka Neno nalo hufanyika.

Unapookoka unakuwa na nguvu za Mungu na Roho wa Bwana anakuwa juu yako. Mungu alitamka Neno na kitu kilitokea, na wewe tamka Neno utaona kitu kinatokea. Ukitamka neon haijalishi kama kuna giza bali utaona mwanga na nuru iking’ra mbele yako. Usiogope hilo giza lililopo kwani Roho wa Bwana yu juu yako. Biblia inasema, Mungu akasema Neno katika vurugu lakini Roho wa Bwana akatembea juu. Na wewe tamka Neno mpaka yanatokea yale unataka yakutokee. Mungu amesema Neno lake halitatoka bure mpaka limetimizwa. Neno la Mungu ni kweli.

Mungu awabariki tutaendelea wiki ijao. AMENI


WAFANYAKAZI WAPYA WA BENKI YA EFATHA WAWEKEWA WAKFU KANISANI.

Baada ya Neno la Mungu kumalizika kutoka kwa Mtume na Nabii Josephate Mwingira, wafanyakazi wapya wa benki ya kanisa la Efatha waliwekewa wakfu tayari kwa kufanya kazi katika benki hiyo. Nabii alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake katika benki ya Efatha ukilinganisha nn wanaume. Wafanyakazi waliowekewa wakfu ni
  1. Falasisia mzawa wa Malawi ambaye hajaolewa.
  2. Ester Ndungulu
  3. Juliet Muhangazo aliyemaliza IFM, ameolewa na ana mtoto mmoja
  4. Juliet Justine kutoka Dodoma hajaolewa
  5. Upendo shoo ameolewa na ana mtoto mmoja
  6. Gidian Mbilinyi hajaolewa
  7. Mbaula na
  8. Nuru

MAONO NA UTABIRI KUTOKA KWA MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA.
Mtume na Nabii Josephate Mwingira alifanya mambo ya ajabu sana kanisani hasa pale alipokuwa akiwaita watu kuokana na matatizo yao na kuwa tabiria. Na hivi ndivyo ilivyokuwa

  • Naona kuna mwanamke aliyota nyama ukeni. Aliposema hivyo alitokea dada mmoja akilia kama amepagawa mashetani na kufika madhabahuni akilia na alipoguswa na Nabii alianguka chini
  • Naona kuna mtu anahisi nyani anaruka juu ya kichwa chake. Alitokea mama mmoja akilia na baadae kupata utabiri wake.
  • Kuna mtuna najihisi yeye ni mbwa. Mwanamke mmoja alitokea na kupata faraja na kuombewa kwani alikuwa amelogwa.
  • Kuna mtu analala na mbwa akihisi ni mtoto wa kike au mwanamke. Alitokea kaka mmoja na alipofika madhabahuni alipota muujiza wake.
  • Naona kuna kijana alipata shida wakati yuko sekondari na alianguka kama mwenye kifafa, wakati yeye hana kifafa. Alitokea dada kama watatu na walipokea muujiza wao,kwani walilogwa wasifanikiwe kielimu.
  • Naona kuna dada aliona inge kama anamng’ata titi naomba aje mbele.

Mtume na Nabii Josephate Mwingira alisema jamii tunayoishi tunapita katika magumu mengi na watu wanateseka sana. Kwanini watu wanapitia katika hali hii? Mimi na wewe hatujui ila Mungu ndiye anayejua. Sio wote wanakuja kanisani ukadhani wana raha, hapana kuna wengine wana maumivu makali sana na wanapokuja kanisani wanafikiri watapata faraja na wachangamke.

MAOMBI KUTOKA KWA MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA.
Wale wachawi waliotumwa kwako tunawang’oa na uchawi uende ulikotoka. Tunaruhusu amani ya Kristo na ingie ndani yako. Ameni.


MTUME NA NABII ALITOA FAIDA ZA DELIVERANCE
Yesu alisema pendeni aduizenu kama mimi nilivyowapenda. Unapoona ndugu yako anateseka msaidie. Kazi ya kuombea ni ya kusaidiana na sio kuachiana, kila mtu anahusika katika maombezi.

Katika huduma zote za kiroho, “Deliverance is the highest in the world” kwasababu inagharimu uhai wa mtu. Huwezi kufanya “Deliverance” kama hujawa mtu wa imani kali na huna roho wa Mungu. “Deliverance” ni zaidi ya uponyaji, muujiza au kuhubiri kwasababu ubaingia katika ufalme mwingine.

Unaweza kuona mtu ameokoka na yuko kiroho sana lakini bado anafanyiwa “Deliverance”, kwasababu “Deliverance” inafanya mtu kuwa kamili. Kama hujawa na upako wa “Deliverance” na ukaombea wengine wapate “Deliverance” utashanga unakuwa hoi na kuishiwa nguvu kutokana na wewe kutokuwa kamili katika huduma hiyo nap engine kufa. “Deliverance” iko juu sana na inahusika moja kwa moja na ufalme wa shetani.

Si kila mtumishi anafikia hiyo ‘level” ya “Deliverance”. Wanaofikia hiyo “level”  ni mitume na manabii. “Deliverance create creation” inaleta uumbaji na inakula maisha ya mtu. Huwezi kumuombea mtu aliyefanyiwa “Deliverance” kwasababu yeye anakuahirishia kifo chako. Hata kama kuzimu kulifanya ufe mapema utaahirishiwa na kuongezea siku.

Mheshimu sana Mungu anayekupa anayeweza kukupa mtu anayeweza kukufanyia “Deliverance”


MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA ALIWATABIRIA WAUMINI.
  1. Waliokatwa mapato yao wanaenda kulipwa
  2. Wafanyabiashara wanaenda kupata faida kubwa ambayo hawakutegemea

MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA ALIWAAGIZA WAUMINI.
Wale waliokoka katika kanisa la Efatha na wale wote waliokoka lakini hawakupata mafundisho ya kukulia wokovu wanaombwa kuja siku ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa katika masomo yatakayoanza kanisani na mwalimu ni MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA kuanzi saa 10:00 jioni.

Hakikisha mpaka inafika Desemba 2012 unaleta watu kwa Yesu ili waokoke na hakikisha unawalea kiroho mpaka wamekua.

Ukifika mwezi Desemba 2012 nitatamka jambo kwa wewe uliyeletya watu kwa Yesu.

MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA ALIOMBEA WAJAWAZITO
Nabii Josephate Mwingira alisema kuna baadhi ya wagonjwa hasa wenye ujauzito wana wadudu katika utumbo wa uzazi. Alitabiri kuwa kuna wengine watajifungua baada ya siku 2,4 na 6…

Nabii alisema, wakina mama Mungu amewapa upako wa ajabu sana katika kipindi cha kuzaaa, wamekomaa na ukiwaona wakati wanazaa hutatamani kuzaa tena, kwani ni mateso makubwa wanapata.

Kuna baadhi ya wagonjwa Nabii aliwasaidia pesa kwaajili ya taxi kwani baada ya maombezi walionekana kutaka kujifungua. Walikimbizwa mahospitalini.

Kuna baadhi yao aliwaombea wajifungue mida ya jioni kama saa 10 jioni ili waume zao wapate kuona wanapopata taabau wakati wa kujifungua na wawaheshimu.

Alimtabiria mama mmoja kuwa kuanzia sasa hataweza kugombana tena na mume wake, kwani wamekuwa wakiogombana sana.

Haya mdiyo yaliyotokea katikam kanisa la Efatha Mwenge.

Comments