Katika hali inayoonekana kutovumilika, wakristo nchini Marekani wameijia
juu picha ya mchoro wa Rais Obama, anayeokana kama akisulubiwa, mfano
wa ilivyokuwa kwa Yesu msalabani.
Picha hiyo ambayo imechorwa mnamo miaka 4 iliyopita, na kushindwa
kuwekwa hadharani kutokana na hasira zilizoamshwa kwa baadhi ya waumini
wa dini ya Kikristo, imerejea tena, na sasa ikiwekwa hadharani kwa ajili
ya watu kuiona na kuitathmini jijini Boston kwenye chumba cha maonyesho
cha chuo cha jamii cha Bunker Hill hadi 15 december, ijapokuwa baadhi
ya watu kulalamika kudhalilishwa kwa dini ya kikristo.
Mchoro huo unamuonesha Rais Obama akiwa anavuta mapazia kufunika nembo
ya ikulu ya Marekani, huku akiwa amevishwa taji la miba, jambo lililozua
hasira kwa watu.
The Truth © Michael D'Antuono |
Licha ya hasira z\a watu kuonekana dhahiri, mchoraji wa picha hiyo,
Michael D'Antuono anaonekana kusikitika kwa kuwa mchoro huo umechelewa
kufika kwenye hadhira.
"Ninasikitika kwamba mchoro huu uliondolewa kwenye maonyesho mjini New
York, natamani usingeondolewa miaka minne iliyopita, nashangaa sana watu
wanaokasirika, hawajui kwamba mimi nimetumia haki yangu ya kikatiba
kuelezea maoni yangu, hata kama yanawakera wao" Anasema Michael.
Kufuatia kupata tangazo la kuwa picha hiyo itakuwa hadharani, mtangaza
nia ya kugombea urais mwaka 2012 kwa kupitia chama cha Republican,
Herman Cain, alionekana kuchukizwa na kusema ya kwake.
Hata hivyo kutokana na mfululizo wa mashambulizi kuwa makali, imemlazimu
msanii huyo kutoa picha nyingine (What I Meant)kama sehemu ya kutafsiri
kile alichomaanisha, na hapa ndipo alipoibua hasira za aina nyingine ya
watu, wakimtuhumu kuwa mbaguzi wa rangi kutokana na kuchora watu wengo,
akiwemo mtu mmoja mweusi.
What I Meant ©Michael D'Antuono |
Mwisho wa yote, msanii huyo aliishia kujitetea kuwa nia yake ni kutaka
kumilika uroho na unafiki, na kuwapa changamoto watu kuhusiana na namna
wanavyowazua mambo. Tazama baadhi ya kazi zake hapa
CP
thx GK
thx GK
Comments