MWIMBAJI MACHACHARI JIJINI DAR ES SALAAM NA ALIYEBAHATIKA KUZAWADIWA GARI AKIWA MTOTO MDOGO KUTOKA NA KUIMBA, JESSICA HONORE KUTOKA KANISA LA WORLDALIVE AFUNGUKA NA KUELEZEA ALIKOTOKA ALIPO NA ANAKOENDA…..
Rumafrica
ikiwa katika harakati zake za kutafuta maisha ilibahatika kukutana na Jessica
Honore maeneo ya Sinza Afrikasana akiwa katika harakati za maisha. Rumafrica
ilimuomba Jessica kufika katika ofisi za Rumafrica ili waweze kuongea machache
kuhusiana na huduma yake ya uimbaji. Na haya ndiyo mazungumzo yalivyokuwa:
Mwalimu na mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Jessica Honore
RUMAFRICA: Hello Jessica, Bwana Yesu asifiwe
JESSICA HONORE: Ameni Rumafrica…mzima wewe???!!!
RUMAFRICA: Rumaafica iko safi Mungu anaiwezesha. Jessica umekuwa kimia sana ila leo tuelezee ujio wa albamu yako mpya ambayo tumesikia baadhi ya nyimbo zikipigwa maredioni.
JESSICA
HONORE: Kwa muda mrefu nilikuwa kwenye mchakato wa kumalizia kufanya albamu
yangu ya kwanza, tangu Jessica mmemfahamu. Kiukweli nimechukua muda mrefu
ambapo albamu yangu ingekuwa tayari iko sokoni. Kwa sasa albamu yangu iko
mwishoni kumalizika na imebakia sehemu ndogo sana kui-release. Albamu yangu ina nyimbo
nane (8) imebeba jina la SITANYAMAZA. Mwezi wa Februari 2013 nategemea kufanya
tamasha la ku-Preview albamu yangu.
RUMAFRICA:
Kwanini albamu yako umeiita SITANYAMAZA?
JESSICA
HONORE: Nimeamua kutumia jina hilo
kwasababu nyimbo yangu ni ya kumsifu Mungu nikimaanisaha muda wote mimi
nitakuwa mtu wa kumsifu Mungu iwe asubuhi, mchana, usiku mimi sitanyamaza
kumsifu Mungu wangu. I just praise God all the time. Kwa upande mwingine
nimekuja Fully, kwahiyo sitanyamaza tena
RUMAFRICA: Maana ni muda mrefu sana umekuwa kimia sana, na watu wengi walikuwa wakijiuliza Jessica Honore yuko wapi?..Tuambie baada ya kutoka hii albamu yako ya kwanza, una mategemeo yoyote yakutoa albamu nyingine?
RUMAFRICA: Maana ni muda mrefu sana umekuwa kimia sana, na watu wengi walikuwa wakijiuliza Jessica Honore yuko wapi?..Tuambie baada ya kutoka hii albamu yako ya kwanza, una mategemeo yoyote yakutoa albamu nyingine?
JESSICA
HONORE: Baada ya albamu yangu hii ya SITANYAMAZA kuitoa, nategemea mwezi wa
nane (8) 2013 nategemea kufanya LIVE concert.
RUMAFRICA:
Albamu yako ina nyimbo ngapi:
JESSICA
HONORE: Ina nyimbo nane (8)
RUMAFRICA:
Kwanini albamu nyingi za injili hapa kwetu Tanzania, mara nyingi zinakuwa na
nyimbo kuanzia tisa (9) kushuka chini na kwanini isiwe zaidi ya tisa (9)?
JESSICA
HONORE: Mimi nadhani ni mfumo Fulani ambao wamimbaji wengi wanafuata, kwasababu
wanaona waimbaji wengi wanakuwa na nyimbo tisa kushuka chini. Lakini wenzetu wa
nje ya Tanzania
utakuwa wana nyimbo ishirini (20) na kuendelea mbele katika albamu moja. Sisi
tunakuwa na nyimbo kiasi hicho kutoka na mfumo wetu jinsi ulivyo, mwingine
utaona kuweka nyimbo nyingi ni kama anapunjika katika soko la kibiashara, kwani
anaweza kutunga nyimbo nyingi na akaweka zote katika albamu, mwisho wa siku
gharama za uuzaji zinakuwa kama yule mwenye
nyimbo tisa katika albamu yake. Utunzi na wenyewe ni kazi, unatumia muda mwingi
sana na
unaumiza kichwa kuuteneneza wimbo. Pia gharama za studio zinakuwa kubwa.
RUMAFRICA: Rumafrica ingependa kujua baadhi ya nyimbo
zilizoko katika albamu yako ya SITANYAMZA
JESSICA
HONORE: Yah..kuna nyimbo moja ambayo nime-release sasa hivi na inaendelea
kupigwa katika vyombo vya habari, inaitwa NAPOKEA, nah ii nyimbo nimeifanyia
Video na Audio. Nyimbo zingine ni:
- juu yako nitaimba
- Sitanyamaza
- Mfariji
- Uwepo wako na nyingine nyingi
RUMAFRICA:
Wasomaji wangu wangetamani kujua style ya uimbaji umefanya katika albamu yako
na kwanini umefanya hivyo?
Jessica Honore
Jessica Honore
JESSICA
HONORE: Mhhh…nimechanganya kidogo, kwani kuna Southern beat, Kwaito, Chakacha
na slow. Mimi ni Mwafrika na Africa kuna vitu vingi, na hizo style hizo ziko
Africa, kwahiyo nimeamua kuchanganya ili kila mtu Africa aweze kuipenda kazi
yangu na pia ujumbe uweze kumfikia barabara
RUMAFRICA: Ni studio gani umefanya hii kazi yako?
RUMAFRICA: Ni studio gani umefanya hii kazi yako?
JESSICA
HONORE: Nimefanya katika studio za SHEKINAH STUDIO Sinza Afrikasana hapa jijini
Dar es Salaam.
Ila nategemea kufanyia mixing Kenya
kwasababu nataka kuweka utofauti kidogo na kuongeza radha kutoka nchi nyingine.
RUMAFRICA:
Ni matatizo gani umekumbana nayo katika zoezi zima la kutegeneza albamu yako?
JESSICA
HONORE: Matatizo ni mengi, lakini kuna hili na nenda rudi nenda rudi za studio
kutokana na umeme kukatika, kubadilisha ratiba, programa zangu nyingi
zimeharibika kutoka na ruti za kwenda
studio, na inafika wakati unachoka kabisa. Hali hii imeharibu sana
mipangilio yangu niliyoipanga,
Ukiangalia albamu yanugu imekuwa katika maandalizi ya miaka miwili sana na ndio maana nilikuwa kimia sana. Na kukaa muda mrefu kama huu nikutokana na mimi mwenyewe kutaka kuja na kitu bora. Kwahiyo utaona leo naenda studio naingiza sauti na ninarudi nyumbani, na nikirudi nyumani ninaanza kufanya mazoezi na kuiboresha nyimbo yangu, nah ii inanisaidia mimi ku-improve. Sasa nikirudi studio naona ile sauti niliyoingiza haiko katika kiwango kile nataka na kinachofanyika ni kufuta na kurudia tena. Mimi nilikuwa sijisikii vibaya kufuata nyimbo zangu ninapoona kuna udhaifu Fulani kwasbabu nilikuwa nataka ku-improve katika uimbaji wangu.
Ukiangalia albamu yanugu imekuwa katika maandalizi ya miaka miwili sana na ndio maana nilikuwa kimia sana. Na kukaa muda mrefu kama huu nikutokana na mimi mwenyewe kutaka kuja na kitu bora. Kwahiyo utaona leo naenda studio naingiza sauti na ninarudi nyumbani, na nikirudi nyumani ninaanza kufanya mazoezi na kuiboresha nyimbo yangu, nah ii inanisaidia mimi ku-improve. Sasa nikirudi studio naona ile sauti niliyoingiza haiko katika kiwango kile nataka na kinachofanyika ni kufuta na kurudia tena. Mimi nilikuwa sijisikii vibaya kufuata nyimbo zangu ninapoona kuna udhaifu Fulani kwasbabu nilikuwa nataka ku-improve katika uimbaji wangu.
Lakini sasa
wakati umefika, na nimeona huu mchezo wa kufutafuta nyimbo niuache na nitazame
kazi.
Na upande wa fedha, halijanisumbua sana na sio kama nina pesa sana na sina mtu aliyeweza kuni-sponsor ili niingie studio. Mimi ninasema ni Mungu tu aliyenisaidia kupata fedha na kuingia studio, ni kama vile Mungu alivyonisaidia kuishi ndivyo alivyonisaidia kupata pesa za studio.
RUMAFRICA Kwani wanamuziki wengi wanapokuwa wamealikwa kufanya huduma katika kanisani Fulani na wanapokuwa wamefanya huduma yao ya uimbaji wanaamua kutoka na kwenda kufanya mambo yao mengine wakati ibada bado inaendelea?
Na upande wa fedha, halijanisumbua sana na sio kama nina pesa sana na sina mtu aliyeweza kuni-sponsor ili niingie studio. Mimi ninasema ni Mungu tu aliyenisaidia kupata fedha na kuingia studio, ni kama vile Mungu alivyonisaidia kuishi ndivyo alivyonisaidia kupata pesa za studio.
RUMAFRICA Kwani wanamuziki wengi wanapokuwa wamealikwa kufanya huduma katika kanisani Fulani na wanapokuwa wamefanya huduma yao ya uimbaji wanaamua kutoka na kwenda kufanya mambo yao mengine wakati ibada bado inaendelea?
JESSICA
HONORE: Mimi naweza kusema kwamba, kuna matatu, yupo after money au hajui
kujisimamia (hajui kusema ndio au hapana) au mchanga kiroho. Pesa imekuwa
ikim-control. Kwahiyo haoni umuhimu wa kukaa chini na kusikia au kula Neno la
Mungu. Kwangu mimi nafanya hivi, Jumapili huwa najua siku ya ibada kwahiyo huwa
na kuwa nasehemu maalum ya kwenda kuabudu na ninaabudu, na kama nimealikwa
katika hilo
kanisa nitaimba na nitabaki maka ibada iishe. Na niwe nimeamua kuwa na hudumu
pale na ninakula neno pale na nikashamaliza ninaenda sehemu nyingine na kama ratiba zinaingiliana, itabidi niamue kuchukua kimoja
na sio vyote viwili kwa wakati mmoja.
RUMAFRICA:
Kuna baadhi ya waimbaji wanaalikwa katika kanisa Fulani na wanapewa hata pesa
ya nauli ila cha kushangazaa yule mwimbaji hafiki na anazima simu yake, wewe
unazungumziaje hili?
JESSICA
HONORE: Huyo ni mwizi kwasababu wewe utafanyaje kitu kama hicho kama mtumishi na kioo katika jamii. Unaweza kufanya kwa
mtu mmoja, ila habari zako zinasambaa, na hatma yake wewe kuchafua jina lako,
na unafungia watu mioyo yao
kupokea ile huduma yako. Kwahiyo the end of the time unakuwa hauna soko, huna
faida katika ufalme wa Mungu kwasababu huduma yako inakuwa ishanfungiwa.
Itafika mwishowa siku huduma yako itakuwa inasikika na familia yako tu na
utakuwa unajiimbia nyumbani kwako.
RUMAFRICA:
Hii albamu yako ya SITANYAMAZA ni albamu ya ngapi
JESSICA
HONORE: Ni albamu yangu ya kwanza.
RUMAFRICA:
Well !! ….Umeanza kuimba lini?
JESSICA
HONORE: Nimeanza kuimba muda mrefu sana,
ila rasmi nilianza kuimba mwaka 2005. Kukaa kwangu muda mrefu kuanzia 2005
mpaka 2012 nilikuwa nataka kwanza kukua katika muziki, na kusema ukweli siku
hadi siku nilikuwa naendelea kukua. Na nimekuwa chini ya watu kama
RUGE wa Clouds FM, na ukizingatia 2005 nilikuwa bado mdogo na ninasoma, na
nillikuwa chini ya mwongozo wa kiroho kutoka na umri wangu. Nafikiri Mungu
alikuwa ananiandaa ili kufikia hatua kwamba the time nikija kutoa kitu kiwe
kimeshiba. Ningeamua kuingia katika muziki kama
nilivyoamua sasa kwa kipindi kile, najua kungekuwa na hitilafu.
RUMAFRICA:
Kuna tetesi kuwa umeshawahi kuzawadiwa gari katika mashindano Fulani ya ya
uimbaji, naomba utuhakikishie?
JESSICA
HONORE: Habari hizo ni za ukweli kabisa. Yalikuwa ni mashindano ya Gospel star
search, na kipindi hicho nilikuwa nasoma nikiwa darasa la saba. Yalipotokea
mashindano hayo nikaenda kushiriki na mwisho wa mchakato nikashinda. Mashindano
haya yalikuwa yanahusisha watu wa mablimbali nimikimanisha watoto, vijana na
hata wazee, kulikuwa hakuna makundi ya umri. Kipindi hicho nilikuwa na umri wa
miaka kumi na tano (15). Namshukuru Mungu nilishinda lile gari na baada ya
kulipata lile gari likanisaidia katika harakati zamgu za kimasomo
RUMAFRICA:
Mbali na muziki ni kazi gani zingine unafanya?
JESSICA
HONORE: Ninafanya Jingles, na nishafanya matangazo mengi Radio ya watu Clouds
FM, Kampuni ya simu Vodacom. Pia mimi ni mwalimu muziki na nimejikita sana katika upande wa
sauti (vocal) . Kanisani kwangu WorldAlive huwa ninafundisha Praise Team na
kuna kanisa la Huduma ya Akuzam lililoko Posta hapa Dar es Salaam. Na pia
ninafundisha watu wengine binafsi.
RUMAFRICA: Ni kweli katika familia yenu ni waimbaji wote?
JESSICA HONORE: Ndiyo sisi sote ni waimbaji wa nyimbo za injili. Katika sisi kuna kaka zangu watatu wanapiga gitaa wa kwanza ni James Honore ambaye anafanya hizi tamasha za Holy Base Giter na anafanya vizuri sana kwangu mimi ni the best in Tanzania na niko so proud na yeye, wa pili ni anaitwa Jacksoni anapiga solo na Rhythm na pia ni mwimbaji, watatu ni John ambaye niko naye pale kanisani kwetu na yuko katika Praise Team, huwa tunapenda kumuita kilaka kwasababu anaweza drums, keyboard, Base gitaa, mwimbaji, ni music composer anaweza akamtengenezea mtu muziki.
RUMAFRICA: Ni kweli katika familia yenu ni waimbaji wote?
JESSICA HONORE: Ndiyo sisi sote ni waimbaji wa nyimbo za injili. Katika sisi kuna kaka zangu watatu wanapiga gitaa wa kwanza ni James Honore ambaye anafanya hizi tamasha za Holy Base Giter na anafanya vizuri sana kwangu mimi ni the best in Tanzania na niko so proud na yeye, wa pili ni anaitwa Jacksoni anapiga solo na Rhythm na pia ni mwimbaji, watatu ni John ambaye niko naye pale kanisani kwetu na yuko katika Praise Team, huwa tunapenda kumuita kilaka kwasababu anaweza drums, keyboard, Base gitaa, mwimbaji, ni music composer anaweza akamtengenezea mtu muziki.
Na wao
wattau, James, John na Jackson
wameshatoa albamu inayoitwa WACHA MUNGU BAND, lakini brother wangu wa mwisho
John ameshamaliza albamu yake..soon atai-release sokoni.
RUMAFRICA:
Umeshafikiria kuimba wote wane kama familia na
mkatoka na albamu yenu as family?
JESSICA
HONORE: Inwezekan na ni wazo zuri, lakini ni vizuri kwenda kwa Roho Mtakatifu
na sio kwa kuiga eti kwasababu mtu Fulani kafanya hivi au familia Fulani
imefanya hivi halafu na sisi tufanye. Wat mnaweza mkawa familia moja na
mnafanya kitu kimioja lakini mmeitiwa tofauti tofauti. Mimi ninavyotakiwa
kuimba inaweza kuwa tofauti na John alivyoitiwa na Mungu. Labda ifanyike kwasababu
tunataka kutengeneza ule umoja kama wait wa familia, ila kiukweli sijawahi
kuambiwa na Roho Mtakatifu kuwa tufanye kitu kama
hicho. Kwahiyo sitaki kukurupuka na kuunda vitu ambavyo sijaambiwa
RUMAFRICA:
Unaweza kufanya huduma yako ya uimbaji bila ya malipo?
JESSICA
HONORE: Kiukweli ninaweza, na nimeshafanya hizo nyingi sana, na sio kwasababu sasa hivi ndio naingia
kimuziki zaidi ndio sitafanya bure..hapana…Kuna wakati mwingine unafanya huduma
na unakarisikia ila hudumainasonga mbele. Ninamshukuru Mungu kwa yale
yanayotokea, wakati mwingine unaona hizi ni dharau, lakini unaamua kufanya
kwasababu nimefanya kwa Bwana.
Laniki
tunakuwa jamani, tunatoka utukufu mmoja na kwenda utukufu wingine. Na siku hizi
huduma yangu imekuwa sio kama zamani, Mungu
amenipa neema ya kuwa na Kikundi changu, ambapo binapoenda kuhudumu naenda nao.
Sasa hivi
nafanya LIVE Music, niko mimi na wapigaji wangu. Kwahiyo utakuwa unanionea,
ukinnita na kunifanyiza kazi bure. Na ujue ninapokuja kufanya kazi na wewe
ninakuwa nimebeba watu na siko mwenyewe…Kwa kiufupi haipendezi.
Dada Jessica Honore
RUMAFRICA:
Tupo jina la Band yako
JESSICA
HONORE:: sina jina, na sijaipa jina, kwasababu mimi ni solo artist, kwahiyo
nina watu permanent ambao ninafanya nao kazi, na wtu hawa wanatoka makanisa
tofauti na kanisa langu la WorldAlive. Na mahali amabpo tunakutana katika
mazoezi ni katika kanisa la WorldAlive Sinza Mori kwa Mchungaji Deo Lubala.
Tunafanya mazoezi kila Jumatatu, Ijumaa na Jumamosi
\RUMAFRICA
inakushukuru kwa kupoteza muda wako na kuwajuza wadau wa Rumafrica kili
ulichonacho.
Comments