Ibada hii ilifanyika katika kanisa lake kwa lengo la kuwakumbusha waumini kuwa Mungu anahitaji kuona ongezeko katika madhabahu yake. Na haya ndiyo aliyohubiri Nabii Flora Peter
Nabii Flora Peter akihubiri juu ya Ongezeko la Shekeli nyumbani mwa Bwana
Leo ni siku pekee ya kurejesha fedha na shekeli katika madhabahu ya Bwana. Ni siku ya maongezeko, yakuongezeka kila maeneo. Unaenda kuongezeka katika biashara zako, katika uchumi wako, uzao wa tumbo lako, unakwenda kuongezeka kila maeneo.
Leo ni siku pekee ya kurejesha fedha na shekeli katika madhabahu ya Bwana. Ni siku ya maongezeko, yakuongezeka kila maeneo. Unaenda kuongezeka katika biashara zako, katika uchumi wako, uzao wa tumbo lako, unakwenda kuongezeka kila maeneo.
Mbarikiwe
watumishi wote akiwemo Anna Makinda, mtumishi Kenesi na mtumishi Joshua. Wote
mliosimama hapa kusikia neno la Mungu, Mungu awabariki
Salama za
Nabii zinatoka katika kitabu cha Kutoka: 3:6, Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu
wa Ibrahimu , Mungu wa Yakobo, Mungu wa Isaka, . Musa akaficha uso wake,
aliogopa kumuangalia Mungu. Bwana akasema hakika nimeyaona mateso ya watoto
wangu, nami nimesikia kilio chao, kwahiyo kwasbabu hiyo nimeshuka nije
niwasaidie yale mateso wanayopata na kwa wasimamizi wao. Kwa maana nayajua
maumivu yao,
mimi nimeshuka ili niwaokoe, niwapandishe katika nchi njema. Nitakupeleka
katika nchi ijao maziwa na asali. Nitamhamisha, Mkanani, Mhiji, na Muamori…Tazama
kilio cha watu wangu Israel, kimenifikia na nimeona mateso walioteswa Wamisri,
haya basi ninakutuma sasa kwa Farao ukawatoe watu wangu wa Israel katika. Nitakutoa
katikati ya maadui, nitakuficha katika mbawa zangu, ili hayo mateso ya Wamisri
yasikupate tena katika nchi hakuna kuzaa mapooza, hakuna atakaeitwa tasa,
kwasbabu Bwana ndiye mchungaji wangu na sitapungukiwa na kitu, kwasababu katika
majani mabichi hunilaza na kando ya maji matulivu huniongoza, huniwisha nafsi
yangu na kuniongoza na hkatika haki huniongoza kwa jina lake. Naam nijapopita
katika bonde la mauti, hakika mimi sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja
nami, hakika Bwana ni gongo langu na fimbo ya kunifariji. Wanabeza mbele yangu
na machoni pa watesi wangu, ulinipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu
kinafurika, hakika wema na fadhili zitanifuata
Nabii Flora Peter akiwa na mtafsiri wake wakati wa ibada
Bwana
anasema, “Ukimjua Bwana utajengwa na ukiondoa udhalimu mbali na hema yake…Bwana
anasema asubuhi ya leo, mjue sana Mungu ili
upate kuwa na amani” Kumbe mtu anayemjua sana
Mungu ana amani ndani yake na hana la kumkwaza na ndivyo mema yatakavyokujia. Na
mimi nakuambia ya kuwa wale waliokudharau kuhusu fedha, Mungu atakubariki mno,
watu watakuogopa waliokudharau, wataona aibu, watatafuta wafiche nyuso zao,
wataogopa kukutazama kama Musa alivyoogopa
kutazama uso wa Mungu. Nakuambia utatisha kama
nini, maisha yako yatabadilika, utainuliwa asubuhi ya leo, utarudishiwa kibali
kile ulichonyang’anywa, kibali cha Yusufu, utajiri, utapewa baraka ya Bwana. Bwana
atakufanikisha wewe uliefika hapa kanisani, ataenda kukubariki, Yesu anaenda
kukusimamisha wewe upya, ataenda kukuinua Bwana.
Bwana
anasema nitaibariki Yerusalem na tena nitawabariki hata wateule wangu
walisikilizao neno langu. Bwana anasema asubuhi hii kuwa ameyaona mateso ya
watu wangu. Naye Bwana amesikia kilio chako mtu wa Mungu. Hata kama unaomba
huko unamadonda, Ukimwi, kansa na mateso mengi lakini Bwana anasema kwa kutumia
watesi wenu, nimeyaona mateso yenu. Ameshuka asubuhi ya leo ili atuponye,
atuokoe, watoto waliopotea wapate kupatikana. Mungu atakupeleaka katika nchi
njema upate kufurahi, kufanikiwa. Bwana anasema anakutoa katika UKIMWI, katika
magonjwa, nakutoa katika hali ya kansa, na katika hali ya ukame katika jina la
Yesu. Nakutoa katika mkono wa Kimungu katika mkono wa Farao. Ufukara ni Farao
amekalia maisha yako. Farao ni adui, magonjwa, umaskini, kukosa kazi. Farao
amekufanga, ninatuma Neno la Mungu likutoe katika kifungo hicho. Wat wnasema
hautanyonyesha, lakini utanyo.
Ndugu yangu
ukimwamini Yesu hautapungukiwa na kitu, utakapopita katika misukosuko mingi ya
ndoa, kazini, watu wanakutenga na kukukataa. Amini jina la yesu hutapungukiwa
na kitu, jina la Yesu ni jina pekee, ukiamini jina hili utabadilishwa na
kugeuzwa, mimi nimeamini nimebadilika, kuokoka ni kubadilika wapendwa
MUNGU AWABARIKI
MUNGU AWABARIKI
Mwandishi
Rulea Sanga
Rulea Sanga
RumAfrica
KAMA UNGEPENDA KUJUA MENGI KUHUSU MATENDO MAKUU YA MUNGU KWA KUPITIA NABII FLORA PETER INGIA KATIKA BLOGU YAKE ILIYOTENGENEZWA NA RumaAfrica...
www.nabiiflora.blogspot.com
KAMA UNGEPENDA KUJUA MENGI KUHUSU MATENDO MAKUU YA MUNGU KWA KUPITIA NABII FLORA PETER INGIA KATIKA BLOGU YAKE ILIYOTENGENEZWA NA RumaAfrica...
www.nabiiflora.blogspot.com
Comments