"Ni kama kanisa hapa, yaani ni kama kanisa humu. Kwanza kabisa, tumpe
heshima Mungu na Baba yetu, Mwokozi Barrack Obama, Barrack Obama"
alisema Foxx na kushangiliwa na umati wa watu uliokuwa ukimsikiliza
kwenye tukio hili la jumapili usiku.
Kufuatia tukio hilo na kuenea kwa habari, kimemfanya kiongozi wa
muunganiko wa Kanisa katoliki kwa ajili ya dini na haki za binadamu,
(Catholic League for Religious Civil Rights) ambaye amekuwa mpinzani wa
baadhi ya sera za Rais Barrack Obama, ikiwemo ile ya sera ya afya ya
kupandikizwa 'microchip' kuwa ni ya kushangaza.
"Licha ya kwamba Obama ameshindwa kuzuia bahari zisijae (kama
alivyoahidi mwaka 2008) bado amefanikiwa kumshawishi Jamie Foxx, na sina
shaka baadhi ya wafuasi pia, kuwa Mungu yupo. Ijapokuwa Mungu anaweza
kuchoropoka kesi ya ACLU (muunganiko wa vyama vya kiraia nchini Marekani
vinavyotetea haki za binadamu) dhidi yake kwa kumtuhumu kulitenda
kanisa ndivyo sivyo, na haki kutopatikana"
Kiongozi huyo (Bill Donohue) pia amekumbushia mwaka 2011 ambapo Foxx
aliulizwa katika mahojiano kuwa Mungu anamaanisha nini kwake, na yeye
akajibu kuwa hajui. Tazama video yake.
Mapema mwaka huu, uongozi huo wa kikatoliki ulimuandikia Rais Obama
barua, ikiainisha mambo mbalimbali ambayo Obama husita kufanya ama
kuzungumza kuhusu Mungu.
"Suala ni kwamba Obama hayuko sawasawa na urithi wa kikristo wa
Wamarekani, hata mwaka 2010 hakuweza kutamka wazi maneno 'In God We
Trust', wakati akizungumzia msemo wa taifa letu nchini Indonesia, badala
yake akasema 'E Pluribus Unum' yaani yeye anaridhika na upagani."
Donohue alisema.
"E Pluribus Unum = Kilatini. wamoja kutokana na wengi (One out of many) Maneno haya yapo kwenye fedha za Marekani yakimaanisha kuwa wao ni kitu kimoja kilichotokana na wengi."
Comments