Furaha, nderemo na vifijo vimeibuka katika mitaa ya taifa la Palestina,
baada ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa kupiga kura na kuipitisha
nchi hiyo hiyo kama taifa. Nchi mia moja thelathini na nane ziliunga
mkono hatua ya kuitambua Palestina kuwa nchi ambayo si mwanachama wa
Umoja wa mataifa lakini itaruhusiwa kushiriki katika shughuli za umoja
wa mataifa, kama mwangalizi, bila ya kuwa na uwezo wa kupiga kupigia
kura maamuzi.
Sherehe kila mtaa. ©The Independent |
Mataifa tisa yakijumuisha Isarael na Marekani yalipiga kura ya kupinga
mpango huo huku mataifa arobaini na moja yakikosesakana kwenye kura
Baraza la umoja wa mataifa limepitisha kwa kauli moja kwa wingi wa kura kupandisha hadhi ya eneo la Palestina.
Kura hiyo yenye umuhimu mkubwa sasa inaiwezesha Palestina kuwa na
ushirika na umoja wa mataifa na mashirika mengine kama vile mahakama ya
ICC.
© AP Photo/Majdi Mohammed |
Mwandishi wa BBC amesema kuwa wapelestina wanaweza kutumia nafasi hayo
kuishataki Israel kwa kusababisha visa vya dhulma dhidi ya ubinadamu
katika ngome yake.
Kutambuliwa kwa Palestina kama taifa, bado hakutabadili mambo haraja,
kwani eneo ambalo umoja wa mataifa unatambua kama sehemu ya Palestina,
'West Bank', Ukanda wa Gaza, na Jerusalem Mashariki vikingali katika
utawala wa Israel. Lakini hilo, halikuwazuia Wapalestina kusheherekea
maamuzi hayo ya umojwa wa mataifa, wakiuita wa manufaa sana kwao, kwa
kuwa wameulilia kwa muda mrefu sasa.
Shangwe hizo zimeambatana a kumsifu kiongozi wa Mamlaka ya Wapalestina,
Mahmoud Abbas, kwa kuongoza vizuri mamlaka hiyo mpaka kutambuliwa kama
taifa. Lakini kwa upande wao.
Israel kwa upande wao wamepokea taarifa hizi kwa masikitiko, wakiamini
kwamba itarudisha nyuma mpango wa mazungumzo ya amani, ulio na faida kwa
wananchi wa pande zote mbili - wale wa mamlaka ya Palestina, na wale wa
taifa la Israel. Je, nini kitatokea baada ya hapa? Maana mpoaka hivi
sasa inatabiriwa kuwa Palestina inaweza kutumia fursa hii kuishitaki
Israel kwa kusababisha visa vya dhulma ya ubinadamu katika ngome yake.
Comments