Mchungaji Robert Jeffress wa First Baptist Church Dalla, Texas. |
Moja ya habari iliyoongoza katika mtandao wa Christian Post mwaka huu ni
suala la mchungaji Robert Jeffress wa kanisa la First Baptist lililopo
Dallas nchini Marekani ambaye katika moja ya mahubiri yake siku moja
kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo alikaririwa akihubiri kanisani kwake
kwamba Rais wa sasa wa nchi hiyo Barack Obama anasafisha njia ya utawala
wa mpinga Kristo.
Mchungaji huyo ambaye huwa anatoa kauli zenye utata (kwa watu wengine
wasiofuatilia maandiko) alisema hayo akinukuu kitabu cha nabii Daniel
kuhusu siku za mwisho na kuwataka waumini wake kutomkariri vibaya kwamba
anasema Rais Obama ni mpinga Kristo la hasha ila rais ajaye atapata
kura nyingi sana ndiye huyo atakayekuwa mpinga Kristo na kuwataka
waumini wa dini ya Kikristo hususani wa nchi hiyo kumuomba sana Mungu
kuwaepushia janga hilo kwa kuchukua hatua ya kumpigia kura mtu sahihi.
Ukiacha jambo hilo pia Mchungaji huyo kiongozi aliwahi kukaririwa
akisema aliyekuwa mpinzani wa rais Obama bwana Mitt Romney kwamba licha
ya kutaja Yesu ni Bwana na Mwokozi si mkristo bali ni Momorn kwakuwa
ibada yao si ya Kikristo kwahiyo amesema Romney si Mkristo ni Momorn
kwahiyo wasidanganyike na misemo yake.
First Baptist Church Dallas, Texas. | x |
Comments