WIZARA
ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema haiwezi kulumbana na maaskofu
kufuatia kauli zao kuwa Serikali haijachukua hatua za maana kudhibiti
vikundi vya kihalifu ambavyo vinatumia jina la waumini wa Dini ya
Kiislamu kuchochea vurugu za kidini nchini.
Akizungumza
na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Dk Emmanuel Nchimbi alisema hawezi kulumbana na maaskofu kwani
hatua zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa makundi
hayo kuwa na kesi mahakamani.
Kauli
hiyo ya Nchimbi inafuatia kauli ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki
na Pwani, Dk Alex Malasusa aliyoitoa wakati wa kufungua mkutano mkuu wa
kanisa hilo mjini Bagamoyo hivi karibuni.
Katika
hotuba yake hiyo ya ufunguzi, Malasusa alisema Serikali ina kigugumizi
katika kusema ukweli kuhusiana na ghasia hizo na zingine zinazotokana na
imani za kidini nchini na kudai kuwa Serikali haikupaswa kuishia tu
kuwakamata watuhumiwa bali pia kufuta vikundi vyao.
Kuanzia
katikati ya Oktoba mwaka huu, kulizuka ghasia katika Mji wa Zanzibar na
Dar es Salaam vilivyokwenda sambamba na kuchoma makanisa.Malasusa katika mkutano huo alitadharisha na kuitaka Serikali ipige marufuku vikundi hivyo hata kama ni ndani ya kanisa analoliongoza.
Hata
hivyo, kesi bado ziko mahakamani kwa viongozi wa wafuasi hao ambao kwa
Zanzibar ni Farid Hadi Ahmed na Dar es Salaam, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Kikristu Tanzania (CCT), Dk. Peter Kitula ilidai kuwa
ukimya wa Serikali katika kuzuia kashfa, uchochezi, matusi na uchokonozi
mwingine wa wazi dhidi ya waumini wa dini ya kikristu kunaonyesha wazi
kuwa serikali ina mkono wake.
“Jambo
hili la maaskofu mnallikuza bure, wangapi wapo mahakamani” alihoji
Nchimbi na kuongeza kuwa suala hilo lisikuzwe kwani linaweza kuwa na
athari mbaya.
Comments