Jacqui Hagler akiwa nyumbani kwake. ©First Coast News |
Wakinamama hao wakiwa nyumbani kwa Bi Hagler, walikua wakijiandaa
kucheza mchezo mmojawapo kati ya mingi waliyopanga. Na walikuwa wameketi
kila mmoja akiwa amepakata pochi yake, ndipo ghafla mvamizi akajitosa
ndani ya nyumba na kumuwekea bastola mmojawapo wa wakinamama
waliokuwepo, akiamrisha pochi, na vito vyao vya thamani kukusanywa.
Pamoja na kwamba hiyo ni bastola ya ukweli, bado wakinamama hao
hawakujua kinachoendelea, huku baadhi yao wakidhani kuwa ni sehemu ya
mchezo, kama ambavyo imeandaliwa na mwenyeji wao.
"Mi nilijua kuwa ni shemu ya mchezo, hivyo sikuwa na wasiwasi, lakini nilipomtazama mwenyeji wangu, ndipo nikagundua kuwa uso wake umejawa na wasiwasi, basi nikaju kuwa hali ni tete" anasema mwanamke mmojawapo.
Lakini ghafla, wakati kila mtu akwa ameduwa na asijue la kufanya, Bi
Hagler alijawa na ujasiri na kumuamuru mvamizi huyo kuondoka kwa jina la
Yesu. Jambo ambalo lilimfanya mvamizi huyo kwa muda huo kuchukia na
kurejea kauli ya kuwataka kinamama hao kutoa kila walichonacho.
Baada ya kuduwaa kwa ukimya kidogo hivi, ndipo wakinamama wote
wakaungana na mwenyeji wao kumkemea Jambazi huyo kwa jina la Yesu,
wakimuamuru atoke ndani ya nyumba.
Nguvu ya jina la Yesu ilipomzidia jambazi huyo, akaamua kutimka
akiliacha jeshi la kinamama 14 wakiendelea kumkemea kwa jina lipitalo
majina yote, jina la Yesu.
Kama mwanamke wa imani, ninajua jina la Yesu lina nguvu kubwa, na huwa
ninalitumia kwenye matatizo, lakini sijawahi kuitumia kama siku ya leo,
leo ni ajabu sana. Lakini sishangai sana kwa kuwa ninajua kuwa Biblia
imetuambia tuliitie jina lake wakati wa shida. Amesema bi Hagler wakati
wa mahojiano na vyombo vya habari.
Kwa upande wake afisa habari wa Lake City, ambaye pia ni mpakwa mafuta
mtumishi wa Mungu, Craig Strickland amesema kuwa, kitendo alichofanya bi
Hagler, ni mfano tosha wa nguvu ya jina la Yesu, lakini sio cha kuigwa
na kila mtu.
Hata hivyo jambazi huyo alikamtwa lisaa limoja baadae alipoamua kwenda
kufanya jaribio la kumuibia mtu aliyekuwa amekwenda kuchukua pesa kwenye
mashine ya ATM. Na hii pia ilitokana na utambuzi wa wanawake hao, ambao
katika kurupushani za kumkemea, jambazi huyo alihangaika kiasi cha nguo
aliyofichia uso wake kudondoka.
Pamoja na hayo, bi Hagler anamshukuru Mungu, kwa kuwa siku hiyo mambo
yangekuwa tofauti, ni mengine yangekuwa yanazungumzwa leo hii, kama sio
muujiza kutokea, hasahasa ikizingatiwa kuwa binti yake mwenye umri wa
miaka 14 alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
Comments