NABII FLORA ATABIRI YAKUWA “WIKI HII NI YA MUNGU KUJITOKEZA NA KUPUKUTISHA MAADUI ZAKO” IBADA IMEAFANYIKA 29.01.2013 ASUBUHI
Bwana Yesu asifiwe..nawasalimu kwa jina lishindalo majina
yote la Yesu Kristo….Ameni
Ninakukaribisha wewe uliyefika mahali hapa kwa jina la Yesu
na Mungu atimize haja ya Moyo wako.
Ni kila sababu ya kusema asante kwa BWANA kwa kunipa siku nyingine hii. Ninasema siku ya leo Mungu ataenda kukutokea wewe, kama inavyosema Ufunuo 3:20 kwamba “Tazama BWANA amesimama mlangoni anabisha hodi".

Yupo Kristo asubuhi ya leo amesimama mlangoni akibisha hodi,
amesimama juu ya moyo wako anabisha hodi. Asubhi ya leo anasema Bwana,
ukifungua mlango wako tu, Bwana ataingia na kufanya makao ndani mwako, Bwana
ataingia katika nyumba zenu mama na uaskini unaenda kuondoka, mikosi inaenda
kutoka maana Bwana anasema tazama mimi nasimama mlangoni nabisha hodi na mtu
akisikia sauti Yangu na kufungua mlango mimi nitaingia na kukaa ndani
mwake..Haleluya…
Bwana anasema ukimruhusu kuingia ndani mwako atakula pamoja
na wewe, atabadilisha maisha yako, atabadilisha ndoa yako, atabadilisha uchumi
wako, atabadilisha kiroho chako, atabadilisha watoto wako,
Hakika Bwana akiingia ugonjwa unatoka, kansa inatoka, UKIMWI
unatoka, umaskini utatoweka mama,
kukoswakoswa kutatoweka, kukosa ajira
kutatoweka, hebu fungua mlango sasa.
Maana ya mlango ni fahamu zako. Yesu ni wa thamani, amezidi
kukupa uzima, afya, amekupa uponyaji, hebu fungua mlango wako asubuhi ya leo.
Nabii Flora Peter akiwa madhabahuni.
Bwana anaenda kugeuza majego ya adui zako, atawapindua maadui zako kama yalikuwa yanatazama mbele yatatazama nyuma, yaani kama ulikuwa hupati watoto sasa unaenda kupata. Ninachotaka kusema ni kwamba hapa maadui watapigwa kwa jina la Yesu Kristo.

Hata kama maadui zako wameandaa adui kama samba au nyati,
Mungu atawageuza hao maadui, na kama waliandaa mipango yako kuyumba ninasema
mipango yako itanyooka na kuwa na mafanikio makubwa, hata kama walikusudia
mwaka huu wakuondoe hapa duniani watashangaa unamaliza mwaka na kuona mwaka
mwingine kama ulivyouona mwaka huu 2013, mwambie jirani yako sifi tena, Bwana
amekusudia jambo kwangu mwaka huu kwani yeye ndiye aliyenitunza, aliyenipa
ajira.
Ninaona mema na Baraka, ninasema..pokeaaaaa Baraka zako kwa
jina la Yesu,
Nabii Flora akihubiri Neno la Mungu
UJUMBE WA LEO WA MUNGU KUTOKA KWA
NABII FLORA
Bwana anasema inua mioyo yenu na maana ya kuinua miyo yenu ni kujiachilia kwa BWANA, unakubali moyo wako kuvunjwa vunjwa, unakubali moyo wako kupondeka. Sio kuangalia haya mavazi uliyovaa, na mimi siko mahali hapa kumwambia mtu umevaa vibaya ila nipo kwaajili ya kumtangaza Yesu, nipo kwaajili ya kusema watu waokolewe, wewe njoo kama ulivyo kwani damu ya Yesu itakutakasa, noo kama ulivyo Yesu atakubadilisha, na usije kwa kujiona unaumbo zuri, una nywele nzuri, ninachofanya ni kuzungumzia Kristo ainuliwe juu, watu waokolewe.
UJUMBE WA LEO WA MUNGU KUTOKA KWA
NABII FLORA
Yoeli 2:13-14 Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu,
mkamrudie Bwana, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye rehema, amejaa
huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi
wa rehema, naye hughahiri mabaya. N’nani ajuaye kwamba hata rudi, na kugeuka na
kutuachia Baraka nyuma yake, naam sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji kwa
Bwana, Mungu wenu?. Yoeli 2:18 Hapo
ndipo Bwana alipoona wivu kwaajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake.
Bwana anasema inua mioyo yenu na maana ya kuinua miyo yenu ni kujiachilia kwa BWANA, unakubali moyo wako kuvunjwa vunjwa, unakubali moyo wako kupondeka. Sio kuangalia haya mavazi uliyovaa, na mimi siko mahali hapa kumwambia mtu umevaa vibaya ila nipo kwaajili ya kumtangaza Yesu, nipo kwaajili ya kusema watu waokolewe, wewe njoo kama ulivyo kwani damu ya Yesu itakutakasa, noo kama ulivyo Yesu atakubadilisha, na usije kwa kujiona unaumbo zuri, una nywele nzuri, ninachofanya ni kuzungumzia Kristo ainuliwe juu, watu waokolewe.
Tusipoteze wasomi kwaajili ya kansa, tusipoteze wasomi
kwaajili ya kansa, tusipoteze watu kwa magonjwa. Nipo hapa kwaajili ya kumwita
Yesu aliponye taifa langu.
ninakumbia usijaribu kumkosa mtu kwani Mungu atankarabati, unachotakiwa kufanya ni kuomba na kumuombea mtu huyo anayefanya makosa. Unaona mtu kava suruali unaanza kumsema, kwahiyo ulitaka mtu huyo asisali, ninakuomba umuache na suruali yake amuombe Mungu wake.

Mungu wetu amejaa neema na si mwepesi wa hasira, Bwana wetu
hana ubaguzi anahitaji kuwabadilisha watu wote. Mungu wetu anawatazama
matajiri, anawatazama maskini, anatazama watu wanaojiweza na wasiojiweza ili
apate kuwainua..Haleluya!!... Mungu hahesabu makosa ya watu wanaomkosea.
Bwana anasema amewahurumia watu wake na kanisa lake. Mwaka
huu Bwana anenda kutuletea nafaka yaani tutakula tutashiba. Ataruhusu wingi wa Baraka,
Ataruhusu wingi wa mazao, Ataruhusu wingi wa utajiri, Ataruhusu wingi wa pesa.
Mungu anasema nanyi mtashiba mwaka huu, na Bwana ameahidi wiki hii kuleta Baraka
kwako, kuleta vyakula, kuleta watoto, kuleta maji, kuleta soda. Na mimi Nabii
Flora ninasema pokea motto wako sasa.
Nabii Flora akiwa madhabahuni kwa kazi ya Mungu
Bwana anasema leo hatawafanya nyinyi kuwa watu wa aibu tena, hata wakiwafanya ninyi kuwa kama watu wa mataifa, kwani watasema Yule mama hana kitu chochote. Lakini nataka kuwaambia kuwa Yesu hatawafanya kuwa watu wa shida, Yesu anaenda kuwabariki. Walio wadharau wataona BWANA akiwahudumia, waliowabeza wataona unaendesha magari mazuri, waliowabeza wataona unaishi katika nyumba nzuri, waliowabeza wataona mna makampuni, waliowabeza wataona masoma shule za International na nzuri kielimu. Mungu analeta Baraka, ninyi mtakula na kushiba, lazima Mungu ainue uchumi wako sasa.
KIPINDI CHA MAOMBEZI MAOMBEZI
Ninasema magonjwa, UKIMWI, Kansa, TB, kuonewa teketea kwa
jina la Yesu. Ninasema leo ninakukurupusha umezoea kutesa watoto wa Mungu,
ninasema siku ya leo toooooka….moto ukulambe…moto wa Yesu ukuunguze…
Ninatangaza jina liletalo uzima..pokea jina hilo wewe unayehitaji likuokoe siku
ya leo. Ninasema wewe mama ulikaa hapo tikisa kichwa chako, Bwana anakuja
kukutembelea na kuondoa shida zako, ninasema tikisa na endelea kutikisa kichwa
chako, kwwa kutikisa kichwa chako unenda kupona ugonjwa wako na taabu zako
zinatoweka amini hivyo watu wa Mungu. Ninafichua mizimu inayokutesa siku ya
leo. Mizimu mnayesikia sauti hii nasema tokeani mlikojificha na muacheni huyu
mama awe huru .
Bwana anasema leo hatawafanya nyinyi kuwa watu wa aibu tena, hata wakiwafanya ninyi kuwa kama watu wa mataifa, kwani watasema Yule mama hana kitu chochote. Lakini nataka kuwaambia kuwa Yesu hatawafanya kuwa watu wa shida, Yesu anaenda kuwabariki. Walio wadharau wataona BWANA akiwahudumia, waliowabeza wataona unaendesha magari mazuri, waliowabeza wataona unaishi katika nyumba nzuri, waliowabeza wataona mna makampuni, waliowabeza wataona masoma shule za International na nzuri kielimu. Mungu analeta Baraka, ninyi mtakula na kushiba, lazima Mungu ainue uchumi wako sasa.
Watu wa Mungu wakimsikiliza Mungu.
Ninasema tumechoka sasa kuchekwa na kudharauliwa na
kutokufanikiwa. Ninasema Yesu lazima aguse mtu, kwa maana watu wamekaa muda
mrefu wakitarajia kufanikiwa. Na mimi kama Nabii Flora ninasema mwezi huu na
wiki hii mpaka kufikia Ijumaa Yesu anaenda
kutubariki na anenda kujifunua.
Jeshi la adui zenu wanaowaloga, wanaoingilia mipaka yenu Mungu anenda kuwafukuza. Na mimi nataka kuona
watu wanaotaka Mungu afukuze adui zao wakimtumikia Mungu wa kweli. Ninasema
maadui wanafukuzwa leo katika jina la Yesu. Ninasema inuka sasa njoo kwa Yesu
ndugu yangu.
Pokea Baraka zako kwa jina la Yesu Kristo. Nataka watu
wafurike wamrudie Mungu wao, na Mungu ataenda kupambana na wale walikokuwa
wanaiua ndoa yako, biashara yako, mipango yao. Na mimi Nabii Flora nakataa kwa
jina la Yesu..
Mungu akishughulika na watu walioamua maisha yao kuwa kwake
Watu wakishuhudia kwa macho yao matendo makuu ya Mingu yanayotokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Maombezi
Kwa Yesu kuna raha..kama unavyoona watu wa Mungu wakipokea baraka za Mungu na kutabiliwa na Nabii Flora
Nabii Flora akifafanua somo linalosomwa na msomaji katika kitabu kitakatifu
Nabii Flora akiwatabiria watu
Watu wakipokea baraka za Mungu kwa kupitia Nabii Flora
...dada akitafakari ..
UKITAKA KUJUA MENGI KUHUSU HUDUMA YA NABII FLORA PETER TEMBELEA
www.nabiiflora.blogspot.com
Mwandishi
UKITAKA KUJUA MENGI KUHUSU HUDUMA YA NABII FLORA PETER TEMBELEA
www.nabiiflora.blogspot.com
Mwandishi
Rulea Sanga
Rumafrica
creative Director and Graphic Designer
creative Director and Graphic Designer
MUNGU AWABARIKI.
SOMO LINAENDELEA...
Comments