RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ASKOFU MWAKANG’ATA AZUNGUMZIA KUHUSIANA NA KUNDI LA GLORIOUS CELEBRATION KUMEGUKA NA KUWA MAKUNDI MAWILI, GLORIOUS CELEBRATION NA GLORIOUS WORSHIPERS TEAM.


Rumafrica na bloggers wa blogu za Kikristo Tanzania, ilibahatika kukaa na mmiliki wa Glorious Celebration, Askofu Mwakang’ata wa kanisa la Full Victory Church lililoko Chang’ombe hapa jijini Dar e s Salaam na kujaribu kutaka kujua ukweli kuhusiana na minong’ono inayotokea mitaani na kwa wapenzi wa Glorious Celebration kumeguka kwa kundi hilo. Askofu Mwakang’ata alizungumza mengi na kuweka wazi kuwa ni kweli kwa sasa Glorious Celebration imemeguka na kuwa na makundi mawili, lakini Glorious Celebration ambayo ilikuwa chini ya Askofu Mwakang’ata bado inazidi kuitwa  Glorious Celebration na hiyo nyingine itazidik kuitwa jina hilo la GWT.

Ameeleza amekuwa akilihudumia Kundi hilo kwa kutoa fedha za Kanisa na fedha binafsi lakini kundi hilo limekuwa haliingizi fedha kama ilivyokuwa ikitakikana na ndipo alipoamua kuuboresha mfumo huo uliokimbiza Wanamuziki hao "Waasi".

Askofu Mwakang’ta alisema anasikitika sana kwa kundi hili kugawanyika, na mbali ya hapo amesema kuna baadhi ya vifaa vya muziki havionekani kama vile base gitaa, pedal ya gitaa na vingine vingi. Aliomba kama wamejitoa wajaribu kurudisha hivyo vifaa na kama hawatafanya hivyo basi tumwachie Mungu ndiye ajuaye yote.

Askofu alipoulizwa swali na mmoja wa blogger kuhusiana na uhalali wa Glorious Worship Team kutumia nyimbo zilizotungwa wakati wakiwa katika Glorious Celebration katika matamasha mbalimbali au katika huduma mbalimbali, naye alijibu kwa kusema ‘hawana haki ya kuzitumia hizo nyimbo kwani ni mali ya Glorious Celebration na sio mali ya GWT, zilitungwa wakati wakiwa chini ya uongozi wa Glorious Celebration. Kama watazitumia sitawazuia wala kuwashtaki popote, nitamwachia Mungu kwani yeye ndiye mwenye mamlaka.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1UAMkdWh4_ksUf_ud7RacS2Of4QDxZPkUxpeoFScRwbukQc_geLMmX2o7gR1GFxskgOIgKOPtINzW2FOndb2k_u0CPnvFz32BnzFbmErP9gEEPiBh5rD4-uLO2oIzsNd1lOle79IrN8X5/s1600/DANIEL+380.JPG
Glorious Celebration kabla ya kugawanyika wakiwa katika kambi ya Askofu Mwakang'ata, Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakifanya mazoezi. Kutoka kulia ni Jessica Honore (alijitoa mapema kabla ya kugwanyika GC), Nice, Davina, Angel Benard (alijiengua mapema kabla ya kuwanyika na sasa yuko mbioni kurudi Glorious Celebration), Lister, Ester na Mercy.
Alizidi kulalamika, Askofu Mwakang’ata yakuwa kuna baadhi ya waimbaji wa Glorious Celebration hivi karibuni aliweza kuwasaidia mambo yao ya binafsi kama vile kuwatafutia Passport, na engine kurekodi nyimbo zao studio, na mbali na hapo wengine kuwapa sehemu ya kuishi, lakini sasa anashangaa wamemsaliti, Mungu ndiye mjuaji na muamuzi.

Aliwashukuru baadhi ya waimbaji waliobaki katika bendi ya Glorious Celebration kama David na Aron ya kuwa wana moyo wa ushujaa, na pia alisema mwimbaji alijiengua kipindi cha nyuma katika Glorious Celebration, yuko mbioni kurudi kundini kwa kazi ya Mungu.

Pia alizungumzia kuhusiana na mapato ambayo yanayosemekana kuwa yalikuwa yanaingizwa katika akaunti yake. Askofu Mwakang’ata alisema anachokumbuka  ni Tshs. 2,500,000 ndizo zilizoingizwa kipindi Gloious wamefanya tamasha la Morogoro na kuanzia hapo hakuna pesa ambayo iliingizwa. Na hiyo pesa ilikuja kuchukuliwa kwaajili ya malipo ya shooting ya albamu ya pili, na kuna pesa zingine kama milioni 5 Askofu Mwakang’ata alitoa katika mfuko wake ili kujazilizia kulipia hiyo shooting yao. Alisema, baada yakuona malalamiko hayo aliamua ku-print Bank Statement ili kuonyesha flow ya pesa ilivyokuwa. Alimuomba Kiongozi wa Band (jina tunamhifadhi) kukutana naye ili wwaongelee kuhusu malalamiko hayo naye hakuweza kutokea.
http://api.ning.com/files/R7xD32zz-xQn7Reh6kLvJx0-Hdlf2l3GryADvQJsYRQR*LPS2LDvDChyx97EvvM1tVulv38AgWByB7ocMgrhYjNwN9B5yMDa/GLORIOUSWORSHIPTEAM4.JPG
Glorious Worshipers Team
Kuna baadhi ya matangazo Glorious Worshipers Team hivi karibuni baada ya kujiengua walikuwa wakitumia kwa kutumia jina la Glorious Celebration, Askofu Mwakang’ata alipouliza kuhusiana na hilo, naye alisema si halali mbele za Mungu kwani watu hawa wameshaamua kutumia jina lao na ni kwanini tena wanatumia jina letu? Hapo watakuwa wanawachanganya wapenzi wa GWT na Glorious Celebration. Ni vema wakatumia jina lao la GWT. Kama wataendelea kutumia jina letu, basi Mungu ndiye mwamuzi.

Kwa sasa Glorious Celebration inayomilikiwa na Askofu Mwakang’ata wanajiaandaa leo Jumanne wana kwenda kambini kwao Chanika kwaajili ya mazoezi.

Story Nzima Ya Mahojiano ya Mmiliki na Waimbaji Walioamua kujitoa Itarushwa Katika Kipindi Kipya Cha Tv.....Chini Ya Ze Blogger na Uncle Jimmy Kupitia Kituo Chako Bora Kabisa Cha Clouds Tv.

Comments