RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DON MOEN BEGA KWA BEGA NA ASKOFU KAKOBE NCHINI CANADA



Mwimbaji wa kimataifa wa injili duniani Don Moen pamoja na kundi la Krystaal wanatarajiwa kuwa kati ya waimbaji watakaoshusha uwepo wa Mungu katika mkutano mkubwa wa injili unaotarajiwa kuongozwa na askofu Zachary Kakobe wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship huko jijini Toronto nchini Canada katika viwanja vya Rexall Centre tennis  stadium kuaniza june 20 had 23 mwaka huu.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na askofu huyo kupitia huduma yake ya Bishop Zachary Kakobe International Ministries(BZKIM) utakuwa mkutano wa injili wa kwanza kufanywa katika uwanja huo mkubwa wa tennis nchini humo na askofu Kakobe ambaye kwa taarifa ambazo GK inazo ni kwamba makao makuu ya huduma yake yapo nchini Marekani kwasasa. Don Moen alizuru nchini Tanzania mwezi August mwaka jana na kubariki watu wengi kwa uimbaji wake huku kundi la wana ndugu wa Krystaal ambao walitamba na kibao cha Niguse tena wenyewe makao makuu yao yapo huko huko nchini Canada.

Unaweza kusoma zaidi katika habari iliyopita kuhusiana na uamuzi wa askofu Kakobe kufanya huduma yake kimataifa  soma
Krystaal Band wana wa Niguse ©nextlevel.blog
Rexall Centre mahali mkutano huo utakapofanyika ©toronto-unlimited.biz

Comments