RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAZNAT KUSHEREKEA MIAKA 10 YA HUDUMA KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE DAR ES SALAAM SIKU YA 5 MEI 2013

Kama kawaida ya Maznat Bridal Care Tanzania ambayo ni kama pilipili hapa jijini Dar es Salaam. Ukiuliza Maznat Bridal Care utakuwa unazungumzia maswala ya Maharusi, Kitchen Party na Send Off. Maznat Bridal Care imekuwa msaada mkubwa kuwarembesha wapendanao katika maswala mbalimbali ya urembo wa mahurusi.


Maznat Bridal Care ilianza shughuli zake miaka 10 iliyopita nikimaanisha ilianza mwaka 2003. Maznat ilianza ikiwa na wateja wachache sana kutokana na jina lake kutokuwa popular kwa miaka hiyo, lakini sasa ukitaja jina la Maznat Bridal Care ni kama vile unavyotaja jina la JK Kikwete nikimaanisha jina lake ni popular sana kutokana na huduma zake zilizo katika kiwango kingine kabisa katika swala zima la urembo wa maharusi. Maznat ambayo ni kampuni kubwa kwa sasa imekuwa ikifanya kazi zake kwa kujali mteja na kutoa ushauri ni jinsi gani mteja wake anaweza kuonekana bomba katika shughuli yake ya Harusi au Send Off au Kitchen Party.


Maznat Bridal Care inasifika sana kutokana na huduma zake na ukarimu wa wahuduma hasa pale unapofika ofisi kwao MIKOCHEN B  kwa lengo lakutaka kupata huduma zao.

Maznat Bridal Care imeweza kutoa ajira vijana wanaofanya katika kampuni hii. Kumekuwa na kilio kikubwa sana kwa jamii kutokana na watu kukosa ajira, lakini Maznat ili tambua hilo na kuona ni jinsi gani ya kuweza kufuata machozi ya watu wasio na ajira ndio maana ikaanzisha kampuni na kuajiri watu wengi wenye sifa bora za utendaji kazi.


Watu wengi wameweza kujifunza mambo mengi kutoka katika kampuni hii ya Maznat Bridal Care, kwani ku watu waliiona hii kampni ikianza ikiwa na wafanya kazi wachache na ikifanya kazi katika mazingira magumu sana. Lakini kutokana na juhudi na ushirikiano katika ya mwajiri, wafanyakazi na wateja wa Maznat, waliweza kufanya kazi kwa bidii na kutumia maarifa mbalimbali ili kuiinua Maznat. Na siri kubwa ya mafanikio ya Maznat Bridal Care ni juhudi katika kazi na kufanya SAVINGS (kuweka pesa Bank) kwa kile walichokuwa wakikipata kutoka kwa wateja wao na kutokuwa na dharau kwa watu. Kubwa zaidi ni katika maombi na kumtegemea Mungu kwa kila jambo walilokuwa wakifanya.


SIKU YA EVENT
Maznat kwa kutimiza miaka yao 10 katika zoezi zima la kupendezesha maharusi siku ya tarehe 5 Mei 2013 watakuwa wanasherekea siku yao maalumu ambayo kwa kizungu tunasema”10 YEARS ANNIVERSARY” katika ukumbi wa Diamond Jubilee hapa jijini Dar es Salaam. Kiingilio ni Tshs. 50,000 ambapo utaweza kupata kitenge cha sare na chakula.


Katika EVENT inatarajia kukusanaya akina mama na wadada 800 katika ukumbi wa Diamond Jubilee siku hiyo. Katika EVENT hii utaweza kuona watu wote waliowahi kupendezeshwa na Maznat katika Send Off, Harusi na Kitchen Party. Huu utakuwa na muda mzuri sana kwako wewe kujifunza mengi kutoka Maznat na kufahamiana na watu wengi katika shughuli za kibiashara na mambo mengine. Utaweza kupata historia fupi kutoka kwa mkurugenzi wa Maznat, wapi alianza. yuko wapi kwa sasa na nini amekipanga kwa miaka ijayo.


Pia kutakuwa na burudani, na zawaida mbalimbali zitatolewa ambapo Magauni Ya Harusi yenye Thamani ya Shilingi laki 9 kushindaniwa, Gharama za Kutengenezwa Bibi Harusi Kufidiwa siku ya Shughuli Iwapo Mtu atashiriki katika Mchakato Huo, Namna ya Kushiriki Nunua Tiketi Yako MAZNAT eneo la Mikocheni Pale Bajaj za Mikocheni B zinapoishia Kisha Utapewa Masharti Nafuu kabisa za Kujishindia Shela La Harusi na Mapambo ya Bi harusi na Matron wake.



JE UNAJUA HILI KUHUSU MAZNAT BRIDAL CARE?

Maznat Bridal Care inategemea kutoa huduma zingine za kimatafifa. Maznat Bridala Care inategemea kuwa na jingo lake kubwa litakalo kuwa likitoa huduamzifuatazo:

1. Floor nzima ambayo ina deal na wanaume, kutakuwa na nguo zao za maharusi

2. Floor ya wanawake tu ambayo itakuwa na vifaa vya maharusi tu.

3. Shule ya Urembo, watu watafundishwa mambo ya maharusi na urembo. Shule hiyo itakuwa kubwa sana kama vile chuo cha IFM au CBE cha hapa Dar es Salaam. Kutakuwa na masomo ya kutengeneza make up kama vile za kuonyesha watu waliopata jail na mambo mengi ya make up au urembo

4. Kutakuwa na gazeti ambalo litakuwa linatoka kwa mwaka mara mbili. Ndani ya gazeti kutakuwa na maada mbalimbali kama vil, Wedding Directory ambayo inahusisha watu wote kuhusiana wedding.

5. Floor kwaajili ya kanisa ambalo litakuwa lina deal na marriage tu (ndoa)

6. Kutakuwa na Maznat Bridal One Stop Center. Utaweza kupata kila kitu cha maharusi kama vile maua, Cake, mapambo, nguo za bibi harusi na bwana harusi

Kuna mambo mengi utapata kujua kuhusiana na kampuni hii katika ukumbi wa Daimond Jubilee.

USIKOSE DIAMOND JUBILEE 5 MEI 2013

MAWAILIANO
+255 752 444470 / +255 783 444470 / +255 718818999


Bloggers wakifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Maznat Bridal Care

Erick Brighton na Uncle Jimmy

Papaaa akitaka kujua jambo kutoka Maznat

Wafanyakazi wa Maznat Bridal Care iliyoko Mikoceni B Dar es Salaam

Blogger wakitupa maswali kwa Mkurugenzi wa Maznat Bridal Care

Mahojiano

Bloga wa RUMAFRICA, Rulea Sanga (kulia)


Maua mbalimbali

Wateja waliorembeshwa na Maznat Bridal Care wakitokelezea

Mfanyakazi wa Maznat Bridal akimhudumia mteja wake

MAPAMBO KUTOA MAZNAT BRIDAL CARE
























Comments