NABII FLORA: DVD, TSHIRTS NA VIPEPERUSHI VYA MAFUNDISHO NA MAHUBIRI YA JUMAPILI KUPATIKANA KANISANI KWA NABII FLORA JUMAPILI YA KESHO. USIKOSE
Watu wa Mungu nina kila sababu ya
kumshukuru Mungu kwa hatua tuliyofikia sasa. Mungu ametuwezesha kuwa na
DVD zetu ambazo zitakuwa zinatoa ujumbe wa MUNGU ninaohubiri
madhabahuni. Kama wewe ulikosa kufika kanisani siku za Jumapili na
katikati ya wiki, unaweza kupata Neno la Mungu kwa njia mbili. nazo ni
DVD au Vipeperushi.
Upande wa mbele wa DVD Cover
DVD yenyewe
Tumeona
tufanye hivyo ili wewe uweze kujifunza Neno la Mungu ukiwa nyumbani
kwako umetulia. Wengi wamekuwa wakifika kanisani kuombewa na wanapofika
kanisani wanapagawana mapepo na kukosa kusikia Neno la Mungu, kwahiyo
tukaona ni vizuri watu hawa wakawa na DVD na vipeperushi vitakavyo
wasaidia kujifunza Neno la Mungu.
Pia
kuna watu wengine kutokana na magonjwa au vizuizi mbalimbali vya
kutofika kanisani, nao tumeona kwa njia hii itawasadia kumjua Kristo na
kupokea uponyaji kwa kupitia njia hizi.
Leo tumeanza na mahubiri yaliyofanywa siku ya Jumapili 10.02.2013 na tutaendelea kutoa kadiri Mungu atakavyoweza kutuwezesha.
Mungu
pia katupa neema nyingine tena ya kuwa na Tshirts zetu ambazo wewe
unaweza ukavaa na kumtangaza Ysu Kristo na pia kulitangaza Kanisa letu
kwa watu wasiolifahamu. Kama mmumini wetu na mtu yeyote yule unaombwa
kuwa na hizi Tshirts.
Mungu wa nabii Flora akubariki.
KAZI ZOTE HIZI ZIMEFANYWA NA OFISI YA RUMAFRICA
www.rumaafrica.blogpot.com
+255 715851523
UONGOZI WA KANISA
Comments