RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ORIDA NJOLE APATA MWALIKO NA ASKOFU SYRIVESTA GAMANYWA

Askofu Syrivesta Gamanywa baada ya kuona mchungo alionao mtumishi wa Mungu Orida Njole wa uimbaji, ameamua kumualika katika ibada ya Jumapili ili aweze kumwimbia Mungu.

Orida Njole amekuwa akifanya kazi ya Mungu bila kuangalia ni mahali gani wala ni dhehebu gani. anachokiamini na kuzingatia ni kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele na jina la Yesu linajulikana kwa kila mtu. Ni wengi wanajua jina la Yesu lakini hawajui jinsi ya kulitumia ili liwe na manufaa katika maisha ya hapa dunia na baadae mbinguni. Orida ameliona hilo ndio maana anatumika na amekuwa akifaidika na huduma yake ya uimbaji, Mungu amekuwa akimwinua kila kukicha.

Unaweza kujiuliza Orida jina lake ni geni. Ni kweli, mwimbaji huyu ni mgeni kwa walio wengi kwa kazi ya uimbaji alianza muda mrefu sana kanisani na hakubahatika kutoa albamu. Mungu amesikia kilio chake na sasa ametoa albamu yake inayoitwa "Duniani Tuwapitaji", na inapatikana na ukitaka akuletee au akufikishie piga namba +255 718 9396.

Askofu Gamanywa wa kanisa la BCIC ameamua kumalika mwimbaji huyu Orida Njole kwa kuona karama aliyompa Mungu ambayo ni baraka kwa walio wengi.

Mungu azidi kumuinua Orida Njole

Orida Njole

Comments