Baada ya kuona umuhimu wa kazi ya
Mungu, Rumafrica iliamua kutengeneza kadi za mwaliko wa uzinduzi wa
albamu za ndungu yetu Lugano Mwiganege mwana wa Mbeya anayeishi hapa
jijini Dar es Salaam.
Lugano
akizungumza na mkurugenzi wa Rumafrica, Rulea Sanga ofisini kwake Sinza
Afrikasana jijini Dar es Salaam, alisema amejiandaa kikamilifu na
anamshukuru Mungu kwani maandalizi yamepamba moto, kila kukicha Mungu
anawapa vitu vya kuwaonyesha katika uzinduzi huo.
Lugano amesema sasa ameamua kupiga LIVE kwani anaamini kwa kufanya hivyo kutaonyesha utofauti ukifananisha na watu wengi kuogopa kufanya LIVE. Kuimba Live kunaonyesha jinsi gani unavyojiamini na uimbaji wako.

Mtumishi
wa Mungu huyu, alisikitika kuona watumishi wa Mungu wanakuwa ombaomba,
alisema utakuta mtumishi wa Mungu amefanya kazi ya Mungu na baada ya
kumaliza anakuwa mtu wa kuomba kwa watu wamsaidie nauli au pesa ya
chakula. Lugano alionekana kuchukizwa na tabia hiyo kwani ni
kumdharirisha Mungu tunayemwabudu. aliwashauri watumishi wa Mungu mbali
na kufanya kazi ya Mungu pia wawe na bidii ya kufanya kazi ya mikono
yao.
Katika uzinduzi huu kutakuwa na kuinuliwa kwa watu kiimani na pia watu watabarikiwa na huduma ya Lugano ya uimbaji wa kipekee utakaofanyika kanisani hapo.
Katika uzinduzi huu kutakuwa na kuinuliwa kwa watu kiimani na pia watu watabarikiwa na huduma ya Lugano ya uimbaji wa kipekee utakaofanyika kanisani hapo.
Lugano alimaliza na kuwaomba watu kufika katika tamasha hilo bila ya kukosa.
Unaweza kutembelea blogu yake www.mwiganege.blogspot.com kwa maelezo zaidi. Blogu hiyo imetengenezwa na RumAfrica.
Kaa katika uwepo wa Mungu.
Kaa katika uwepo wa Mungu.
Comments