RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TAMASHA LA WAKONGWE WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA MAANDALIZI YAPAMBA MOTO

Kampuni ya COME AND SEE PROMOTERS imeandaa Tamasha kubwa la wakongwe wa muziki wa injili Tanzania kwa lengo la kutambua mchango mkubwa ambao wameutoa waimbaji hawa wazamani wa muziki wa injili katika kuinua na kuendeleza mziki wa injili Tanzania. Akiongea kwa nyakati tofauti mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Come and see Promoters bwana Emmanuel Ezekiel ( Pastor Pepea ) Amesema hili ni tamasha la kihistori ambapo halijawahi kutokea katika nchi yetu ambapo waimbaji wote wakongwe wa mziki wa injili kukutana katika jukwaa moja.Tamasha hili limepewa jina la OLD IS GOLD DAY linatarajia kufanyika tarehe 17/3/2013 katika ukumbi mtulivu wa Diamond Jubilee kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni  na kukusanya wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikari,viongozi wa dini, waandishi wa habali nk.
Tamasha hili litaambatana na utoaji wa Tuzo za heshima kwa waimbaji hawa wakongwe ili kutambua mchago wao katika kuinua na kuendeleza wa injili Tanzania. Waimbaji wakongwe wa mziki wa injili watakaoshambulia jukwaa ni MZUNGU FOUR, JANGARASONI, MASAGA NYANDA,DAVIDI NKONE, NATHANIEL HINGI, MWASASU, MWASUMBI, ENCY MWALUKASA, AMON NA UPENDO KIRAHIRO, NEW LIFE BAND TOKA ARUSHA, na kwa upande wa kwa ya ni LULU KWAYA NAYOTH KWAYA ,VICTORY SINGERS , MSASANI KWAYA NK na kusindikizwa na JOSHUA MLERWA. 
ASKOFU JANGARASON
NEW LIFE BAND
MCHUNGAJI ENCY MWALUKACA
PASTOR SAFALI

JOSHUA MLERWA

MCHUNGAJI AMONI KIRAHILO

MCHUNGAJI MASAGA NYANDA
MZEE MAKASI
UPENDO KIRAHILO
MKURUGENZI COME AND SEE PROMOTERS

Comments