Hakuna kitu kizuri duniani kama kujua kuna mtu yupo bega kwa bega nawewe wakati wa raha na pale unapokuwa katika shida. Ni kama biblia inavyosema kuhusiana na dini iliyosafi mbele za Mungu wetu kwa kuorodhesha mambo mbalimbali likiwemo suala la kuwatembelea yatima na wajane pia kuwasaidia katika dhiki zao.
Hii leo kuanzia majira ya saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika kanisa la Dar es salaam Pentecostal (DPC) ambalo lipo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam kunafanyika tukio la kugusa la kuwatia moyo na kuwapa ushauri wa namna ya kuinuka tena wanafunzi ambao wamepata majibu mabaya ya kidato cha nne kwa alama ya daraja la nne na sifuri.
Tukio hilo limeandaliwa na watumishi vijana kutoka jijini hapo, ambao wanajua na kuhisi hali ambayo wanajisikia kwasasa wanafunzi hao ambao matokeo yao yamelitikisa taifa na kuwa gumzo kubwa ambalo halijawahi kutokea kwa upande wa elimu nchini hata nchi jirani kuzungumzia matokeo yao.
Ambapo wanafunzi watakaofika na watumishi wengine watapata huduma ya chakula na vinywaji bure kutoka kwa waandaaji wa tukio hilo maalumu la kuwaambia vijana wa kidato cha nne kwamba kuna maisha baada ya matokeo yao.
Comments