RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA STELA JOEL AFIWA TENA NA DADA YAKE AMBAYE NI TUMBO MOJA, GRACE JOEL USIKU WA KUAMKIA LEO

Hata wiki moja hajaisha Stella Joel alifiwa na mdogo wake Jessica Joel katika hospitali ya Mwananyamala na mazishi yalifanyika katika makaburi ya Ubungo Rombo.

Leo tena Stella Joel amefiwa na dada yake anayemfuata kuzaliwa Grace Joel amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko Bukoba alikoenda kwaajili ya matibabu. Na sasa wako katika maandalizi ya kujiandaa kusafiri kuelekea Bukoba kumzika ndugu yao.


Hili ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana katika familia ya Joel na hata kwetu sisi rafiki na ndugu. Unaweza kujiuliza ni nini hiki kinafanyika katika familia hii kwa kupotelewa na ndugu wa nyumba moja kwa kufuatana. Mungu ndiye aliyewaleta hapa duniani kwa makusudi yake na sasa ameaamua kuwachukua kwa makusudi yake.


Mkurugenzi wa Rumafrica na uongozi wa Rumafrica inawapa pole sana familia ya Joel na hasa Stella Joel ambaye amekuwa msaada mkubwa katika osisi yetu.

Ngoja tuone baadhi ya picha katika msiba wa mdgo wake stella Joel ambaye kwa sasa amefiwa tena na dada yake Grace Joel huko Bukoba usiku wa kuamkialeo

Marehemu Jessica Joel wakati wa uhai wake

Marehemu Jessica Joel akiwa amelala katika kitanda cha milele akisubiria kuwekwa katika nyumba ya milele

Kutoka kushoto ni Mchungaji Chriss na mfiwa Stella Joel akiwa na huzuni wa kupotelea wa mdogo wake Jessica Joel. Na sasa ameongezewa maumivu kwa kufiwa tena na dada yake Grace Joel
Kutoka kulia,wa pili ni mtoto wa marehemu na huyo mtoto aliyepakatwa
Stella Joel akiwa amemkumbatia mtoto wa marehemu mdogo wake Jessica Joel hivi juzijuzi na leo kafiwa tena dada yake Grace Joel
 Baadhi ya rafiki na jamaa waliofika kumsindikiza Jeesica Joel

Mkurugenzi wa Rumafrica Rulea sanga akiwa na camera anakupa pole sana stella Joel kwa kufiwa na dada yako Grace Joel. Hapa alikuwa akipiga picha ya mwili wa marehemu Jessica Joel ambaye ni mdogo wake na stella Joel. Msiba ulitokea hivi karibuni.

Mwili wa Jessica Joel ukielekea makaburini kupumzika katika mako ya milele.

Mkurugenzi wa Rumaafrica na wakazi wa Ubungo na maeneo mbalimbali wakimzika Jessica Joel Ubungo Rombo

Mkurugenzi wa Rumafrica aliyevali tshirt ya Kijani Rulea Sanga akiweka lens sawa kwaajili ya kuchukua matukio ya mazishi ili wewe upate kuona

MUNGU AKUTIE NGUVU STELLA JOEL

Comments