NABII FLORA: BWANA ANAKWENDA KUREJESHA FIMBO ULIYONYANG"ANYWA NA ADUI. MAHUBIRI YA TAREHE 27.03.2013
UJUMBE WA LEO KUTOKA KWA NABII FLORA PETER
Maombolezo 3:19. Kumbuka sana mateso yangu na msiba wangu pakanga na nyongo. Nafsi yangu ni kali ikikukumbuka hayo, nayo ikiinama ndani yangu. Ninajikumbusha sana neno hili kwahiyo mimi ninayo matumaini. Ni huruma za bwana kwamba hatuwezi kuangamia kwa kuwa rehema zake kwetu sisi hazikomi, fadhili za Bwana ni mpya kila siku asubuhi na waminifu wako ni mkuu. Bwana ni fungu langu tena ni nguvu yangu kwahiyo mimi nitamtumainia Yeye. Jicho langu lilipokuwa likitoa machozi kila wakati na bila kukoma, lakini Bwana akanambia wakati wa kulia sasa umeisha. Walininyang’anya mavazi yangu na fimbo yangu
Sitaki kuona na mateso uliyonayo, moyo wangu unaumia ninapoona unapata shida na nia yangu ni kuhakikisha wewe unaokolewa. Makusudi yangu ni kuhakikisha wewe unafanikiwa, unaendesha gari yako nzuri, unafuraha katika maisha yako, ninasema pokea Baraka kwa jina la Yesu Kristo na Yesu akutendee kwa jina la Yesu Kristo, Bwana akupe neema kwa damu ya yesu Kristo. Ninasema zunguka kwa damu ya Yesu Kristo uone wema wa Bwana.
Mimi sitamtiumainia mwanadamu siku zote za maisha yangu bali nitamtumainia Mungu. Ninasema na mama uliopo hapa ya kwamba wakati wako wa kulia umekwisha. Umelia juu ya mchumba wako, na mimi ninasema hautalia tena na Mungu anakwenda kumfinyanga, kumpondaponda na kumbadilisha , pokeaaaaa...Mama mzungu hautakwenda kulia tena..Pokeeeaaaa neema ya kutolia tena. Bwana anakwenda kukomesha mateso ya ndoa yako, pokeeeeaaaa neema. Ninaona milango imefungua juu yako na unaenda kuinuliwa asema Bwana wa majeshi. Walikunyang’anya haki zako mama na sasa hutalia tena.
Walitunyang’anya mavazi na fimbo zetu lakini leo ninarudisha Baraka zangu. Kila alichokunyang’anya ninakirudisha. Nirudisha Baraka zangu, ninarudisha upako wote, ninawaacha kappa, ninarudisha mateka, ninarudisha mafanikio. Wamenyang’anya pesa yako, Baraka zako, nyota yako, kipato chako, leo ninakirudisha. Wamekuibia upako, wamekuibia mafanikio yako, leo ninarudisha fimbo yako, ninakwenda kurudisha mchumba wako, mume wako, palipobomoka lazima parekebishwe, ninawarudisha watu waliorudi nyuma. Ninarudisha mafanikio yako kwa Pastor Ansilla, ninaweka ulinzi pande zot kwako, ninarudisha sanduku la agano, lipo sanduku la agano mahali hapa limesindikwa asubuhi ya leo. Ninarudisha Baraka za maduka, makampuni, biashara yako, wateja wako, maongezeko.
Ninasema kila aliyekupiga amepigwa, aliyekugeuka amaegeukwa, aliyekuzunguka amezungukwa, aliyekujeruhi amejeruhiwa, asema Bwana wa majeshi, pokea Baraka sasa, ninaona watu wanapokea, ninaona watu wameshamalaizi wanatafuta mlango wapenye
Ninasema mimi ni Nabii ninayo mamlaka, ninamshusha chini adaui. Ninakuita Baba, ninakuita Jehova, ninakuita Yesu, shuka sasa Baba uwaokoe watu wako sasa.
Ninasema ninarudisha uridhi wako, pokea mfanikio, kwa damu ya Yesu Kristo. Na wewe unayesoma blogu, unayesoma katika facebook, unayetaza katika youtube nasema pokea kwa damu ya yesu Kristo. Ninaachilia neem, niaachilia Baraka, ninaachilia mafanikio. Ninakkuita Baba, ninakuita Makadeshi. Ninarejesha utajiri kwako kaka yangu, amaduka yanarejea, utajiri unarejea. Bwana anakwenda kutuzidisha kuliko tuliko sasa, Bwana anakwenda kushuka na nguvu zake, atashuka na uweza wake, atakwenda kurejesha mambo yako yaliyoharibika.
Bwana anasema aliyewakwangu nitamleta na kumbariki kwa jina la Yesu Kristo. Wewe ni Mungu unayetenda, wewe ni baba unayejibu, ninakutukuza mfalme, ninasema asante. Ninakuona dada unaenda kunyonyesha maana wewe ni tasa, Mungu anaenda kufungua utasa wako, na mimi nabii ninaona uzao katika tumbo lako na sio tasa, utazaa watoto wazuri wa kisura wakiume na wa kike, wanakwenda kuzaliwa kwa tumbo lako. Ninasema na wewe mama mwenye kilemba ninaona watoto wazuri wanakwenda kuzaliwa..Ooohh Baba..ooohhh Baba...oooohhh, ninakuita Baba kwaajili ya huyu mama.
Fimbo ni heshima yako inakwenda kurudi. Fimbo uliyoibiwa imerejeshwa katika kanisa la Yesu. Kanisa la Yesu ni huduma ya Uponyanji.
Amina. Karibu sana kwaajili ya Pasaka.
Unaweza kujua mengi kuhusu nabii Flora kwa kutembelea
Blogu: www.nabiiflora.blogpot.com
Facebook: Nabii Flora
Youtube: www.youtube.com/Nabii Flora Peter
Mwandishi
Rulea Sanga
Comments