RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA KATIKA IBADA YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU YA JUMAPILI 24. 03.2013

Ninaomba uinue juu macho yako. Ninataka Bwana akutendee, ninataka Bwana akuonekanie. Viwanja vyote lazima visisme, leo ni siku ya kujazwa na Roho Mtakatifu. Utaona upepo unaingia, utaona utukufu unaingia, utaona Baraka zinaingia. Mama mwenye mtoto na unamzigo naomba uweke sawaswa, maana leo ni siku ya tofauti kabisa. Nitakapokwenda kuinua mkono wangu huu juu utaona watu wanasujudu chini.
 Nabii Flora Peter
KUOMBEA MIKONO WA NABII FLORA
Baba ninakutukuza kwa kupitia mikono hii, ninahitaji kibali kutoka kwako, ninapokwenda kunyoosha mikono yangu mbele za watu wako, watu wakapate kupokea na kuponywa kwa damu yako Yesu Kristo. Amen

 Nabii Flora akiombea mikono yake Mungu aweza kuitumia katika uponyaji na baraka


KIPINDI CHA MAOMBEZI
Ninazungusha mkono wangu huu sasa, ninaomba utukufu tembea, na watu wote wauone utukufu wa Bwana. Ninaona viwanja vyote nina-shake. Yesu tembea, watembelee watu wako, ninaachilia neema, ninaachilia Baraka juu ya viwanja hivi. Ninasema mchakamchaka sasa eeeh...touuuuuchhhh!!! kwa damu ya Yesu Kristo. Ninasema na watu leo, ni siku ya kubadilika, hata kwa wachungaji na wazee wa kanisa ni siku yenu ya kubadilishwa.
Yesu tembea kwa watu wako. Siku yako ya kuponywa ni leo, ninasema toooouuuuchhhhhh!! Leo unaponywa, wenye ugonjwa wa UKIMWI sikia, wenye kansa sikia, vilema sikia huu ni wakati wa kuponywa..Pokeeeeeaaaaa kwa damu ya Yesu kristo.

Wewe ni Baba unajyetembea, Mungu wetu mwenye neema, Mungu wetu unayetenda, ninatamka Baraka asubuhi ya leo. Ninaona tetemeko nadni ya kanisa, ninaona upako unapenya. Upako utembea kwa mtumishi wako Baba, tembea kwa watu wako leo, tembea kwa Rose Mbajo, tembea kwa Pastor ansilla, tembea kwa Pastor Jury, tembea kwa wababa na wamama, kutana na mama Rwegasila. Mama Rwegasilla pokea neema huko uliko ninasema toooouuuuchhhh!!!

Ninataka kuona watu wanakimbia na wanachangamkia madhabahu. Ninavungua moto, ninakata mapepo, ninakata majini, ninakata. Ninaachilia msumeno wa kukata. Ninasema pokea Baraka, watu wamekuwa watumwa, lakini leo Recho pokea Baraka,

Eeeehhh Yesu tembea, umetukuka Mungu, shuka Baba na nguvu yako, shuka Yesu sasa ukatendee, ukatendee Jehova, ninakuita Baba, ninakuita kwa uchungu.

Ninaziona mbingu zimeinama, mbingu zinasogezwa, ninaona utukufu wa ajabu, ninaona moto unapenya, ninaona mishale ya moto inapita. Ninakufyeka mshale wa moto, ninaona adui anakutesa na mimi kwa nguvu za Mungu namuondoa kwa damu ya Yesu Kristo.
Ninakutuza Baba, umetukuka Baba, ninaomba Yesu uwatembelee watu wako ili ijulikane kuwa uko Yesu. Ninaachilia uwepo wa Mungu. Mapepo majini ninasema fyata mikia yak oleo kwani yuko bwana amesimama, ninasema fyata mikia leo, ninasema achilia watu hawa. Ninasema na majini, ninasema na mapepo, ninasema na magonjwa nayakamata na ninayafunga matitamatita. Ninayalipua moto, Ninayalipua moto Ninayalipua moto Ninayalipua moto kwa jina la Yesu Kristo.

Ninaomba uinue mikon-o yako juu. Ninaachilia upako, ninaachilia upako kwa wachungaji upenye sasa. Umekamatwa na mizimu ninasema kwa damu ya Yesu Kristo unaachiliwa sasa...Pooookeeeeaaaa! Uliyekamatwa na mateso ninayakusanya mateso yako ninayapeleka katika mikono ya Yesu na Yeye anayashika sasa.
Ninayashika mateso, magonjwa, shida, kulogwa, kukosa ajira, kutokuolewa na kuona, ninayashika mateso yako na ninaenda kuyahifadhi, ninayakusanya sasa... , ninayakusanya sasa... , ninayakusanya sasa... , ninayakusanya sasa, ninayakamata na kuyakusanya..ninayalipua moto. Mwachie baba Yule, mama Yule, kijana Yule, wewe uliyekufa mazingira ya kutatanisha onekana sasa. Ninasema viwanja vyote tikisikia.

Ninasema lazima leo watu wafiunguliwe, ninasema na watu, ninasema na hewa, ninasema na ardhi, ninasema na watu waliofika mahali hapa. Ninasema ardhi tikisika, shuka Bwana. Mwambie mwenzako kuwa leo lazima watu waokolewe.
Umekosa ajira yako kwa muda mrefu, leo ni siku yako ya kupata ajira, wewe ambaye huna ajira huu ni wakati wa kupata ajira. Ninasema na mabinti, mabinti pokea shela, wataenda kulipa mahali, ninasema pokeeeeaaaaa!!! Vaa shela sasa kwa jina la Yesu. Ninasema yupo Bwana mahali hapa, ninasema pokea. Ona kimbuga cha Yesu kinavyofanya kazi kwa watu hawa.
Moto unawake katika viwanja vya Salasala kwa nabii Flora, ninasema pokea kuolewa, binti yangu funga ndoa, ninasema pokeaaaa!! Utaishi maisha ya ukiwa mpaka lini?  Lazima umuone Bwana. Ninasema na mabinti na vijana, pokea mafanikio. Pokea kuolewa mabinti zangu, una mchumba anakuzingua leo amekamatwa namna hii kwa damu ya Yesu Kristo.

Operation inafanya kazi, upako uko nje nje, tembea Bwana Yesu, ninakuita Bwana Yesu kwani wewe ni Mungu unayetukuka. Ninaona malaika wameshuka mahali hapa, wamezunguka katika viwanja hivi kama mashahidi.
Ninasema pokeeaaa wewe, Bwana anakusudi na wewe, amekusudia jambo jipya leo, amekusudia kubadilisha maisha yako leo. Ninasema vilema wote tembea juu kwani kwa Mungu halkuna vilema, hakuna viwete. Ninasema leo lazima viwete watasimama.
Mapepo, vinyamkela, majini, mikosi, mapepo kutoka Zanzibar, mizimu kutoka Zanzibar mmekamatwa. Mapepo mmetoka Zanzibar upo moto hapa leo unakuunguza. Moto unakula adui zako.
Ewe jini mahaba uko wapi jini mahaba?  Ninasema lipuko huko uliko, tafuta njia, umekaa kwa watu hawa kwa muda mrefiu, ninasema leo achia

Yeyeyeyeyey!!!! Moto huo!!! Ninaomna moto usio wa kawaida, watu wanaponywa UKIMWI. Ninayakamata magonjwa ya UKIMWI, ninayalipua moto.
Mwambie mwenzako wakati umekaribia wa Yesu kubadilisha maisha yako, kubadilisha kiroho chako, kubadilisha mtazamo wako, wakati umewadia sasa, wakati umewadia wa wewe kuolewa, kuwa na gari, kuwa na yumba nzuri, kuwa na makampuni na viwanda, kuwa na mtoto mzuri, kuzaa. Wakati umewadia wa kuinuliwa Rulea Sanga, wakati umewadia wa kufanikiwa mambo yako. Bwana Mungu alitiuma Mwanae wa pekee ili aje ulimwenguni.
Ninasema wakati umewadia kwa wewe unayesoma katika blogu na facebook, wakati wako umewadia wa kubadilishwa na ku-change maisha yako kuwa bora. Yesu akuinue, wakati umewadia wa wewe kushamili.
Unasikia kelele hapa katika viwanja ni kwasababu nguvu ya Mungu inatembea. Viwanja vinashangaraizi, upako umemwagwa katika viwanja hiv.
Kuna watu kutoka songea, Mtwara, Dodoma, Morogoro, Moshi, Malangu, wamekuja kumuona Mungu, kwa kuwa wamesikia kwamba yuko Mungu katika viwanja hivi. Ninaomba Baba watu hawa wamuone Jehova (ninaomba uinue mikono yako). Ninauchungu juu ya watu hawa, ninasikia uchungu kuona watu wanapata shida, watu wanakufa kwa magonjwa,  watu wanakufa kwa UKIMWI, vijana wanakosa ajira (ninaomba uinue mikono yako juu). Ninaona huruma kuona unakufa na UKIMWI wewe. Ninasema Yesu yuko hapa anatenda. Kwanini upate shida, taabu yuko Bwana mahali hapa, yuko Yesu.
(Inua mikono yako juu). Baba tazama watu hawa, tazama mikono hii wameinua mbele zako, wamelekeza mioyo yao kwako Baba wa mbinguni, Baba tazama mioyo yao.Wapo wengine hapa wanahitaji ada ya shule, Yesu shuka, tunajitakaza Yesu. Baba gusa watu hawa. Tusamehe Baba makosa yetu. Samehe baba watu hawa. Ninahitaji kuona nguvu ya Mungu ikishuka.
Ninaomba uinue mikono yako juu sana, ninataka kuona mikono ikitikisika. Umekuwa na maneno ya umbea, umekuwa na majungu ndio maana huzai, umekuwa na vitiu vya chini chini, ume[kuwa ukisikiliza maneno. Yesu ansema ondoa usanii huo na kaa pamoja nami.  Kwanini hufanikiwi?
Baba nyesha mvua yako katika mikono hii iliyoinuliwa kwako. Kwanini upate taabu wakati Bwana yupo? Kwanini wachungaji mpate taabu? Yupo Yesu Mkombozi. Wewe unayeumwa UKIMWI, ninasema yuko Yesu.

Ninaona mikono inatikisika na upepo unavuma kama ishara ya kupokea Baraka kutoka kwa Mungu. Ninaona adui amechomwa moto sasa. Shuka Roho Mtakatifu, shuka Mungu wa Israel, uwaguse watu wako hawa Baba...

Sikiliza watu wa Mungu, ukiona mtu anakuita mcawi maana yake amekushindwa, amemuona Yesu na mambo yake hayaendi ndio maana anakuita mchawi, kwani una nguvu ya Mungu na yeye anashindwa kufamnya mambo yake kwako, na ndio maana anakuita mchawi. Ukiona mtu anazungumzia mambo yalko vibaya ujue huyo anakukubali.


KIPINDI CHA KUOMBEA MAFUNGU YA KUMI






GIDEON MUTALEMWA AKIMWIMBIA BWANA IKIWA NI MARA YAKE YA KWANZA TANGIA AZINDUE ALBAMU YAKE











KIPINDI CHA KUOMBEA MAJI
Waumini wakinyanyua maji kwaajili ya kuombewa na Nabii Flora

NABII FLORA AKIELEZEA SIKU YA PENTEKOSTE
Siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu alishuka. Roho Mtakatifu maana yake nini na anafanya kazi gani kwako na anafaida gani kwako? Roho Matakatifu akishuka kama una UKIMWI, UKIMWI wako unaisha, Roho Mtakatifu hakai sehemu chafu, Roho Mtakatifu akishuka kama una kisukari, kansa, aleji, umaskini, magonjwa yanaisha. Roho Mtakatifu ni moto tena moto ulao. Aliposhuka kwangu, mimi nimebadilika, maisha yangu yamebadilika na wewe ni shahidi. Roho Mtakatifiu aliposhuka alibadilisha maisha yangu, ukoo mzima unanikubali. Mimi ni mdogo, lakini hakifanyiki kitu mpaka waniulize mimi... Roho Mtakatifu akishuka kilicho chini kinainuliwa. Mume wako hatakusumbua tena, ukitoka hapa na Roho Mtakatifu utaitwa jina zuri kabisa na mumeo.

SOMO LINAENDELEA....

Mchungaji Jury akimuwekea muumini aliyekuwa akinena kwa lugha
Waumini wakinena kwa lugha baada ya kushushiwa Roho Mtakatifu

Nabii Flora akipita kwa watu kuwawekea mikono kupokea Roho Mtakatifu




Watu wakipokea Roho Mtakatifu






Mwimbaji wa kwaya ashushiwa Roho Mtakatifu madhabahuni
Nabii Flora alimuona huyu dada ndiye muombaji wa kweli na aliweza kunena kama nabii anavyonena. Nabii akaamua kumuwekea mkono

Kaka huyu ni mfanyakazi wa shirika la TANESCO. Baada ya kurudi kutoka Marekani alipata ugonjwa wa kutoweza kutmbea. Hapa akiombewa na Nabii Flora
Akijaribu kutembea baada ya maombezi




KIPINDI CHA MATANGAZO

KIPINDI CHA UGAWAJI WA BAHASHA KWAAJILI YA PASAKA


KIPINDI CHA KUOMBEA SADAKA YA UJENZI

Hapo chini ni Mchungaji Ansila ambaye alishuhudia siri ya urembo wake na jinsi Mungu anavyomtunza na kuonekana kijana wakati yeye ni mzee wa miaka 65. Mchungaji alimshukuru Mungu kwa kumponya figo. Watu walifurahishwa sana na ucheshi wake kama utakavyoona hapo chini:
Mchungaji Ansilla
Waislamu wakisikiliza Neno la Mungu









KIPINDI CHA SIFA KUTOKA KWA WAIMBAJI MBALIMBALI

Mwimbaji wa nyimbo za injili Sarah Mvungi
Sarah Mvungi akimkabidhi albamu yake kwa Nabii Flora Peter kabla ya uimbaji
Sara Mvungi akisalimia waumini
Kulia ni mtoto wa Saraha Mvungi


Saraha Mvungi akicheza na Nabii Flora Peter
Nabii Flora akienda sawa na mwimbaji wa nu=yimbo za Injili na MC Saraha Mvungi

Nabii Flora na Sarah Mvungi
Sara Mvungi akitafakari baada ya kumaliza kuimba

Saraha Mvungi wa pili kutoka kulia nyuma akiomba baada ya kumaliza kuimba

KIPINDI CHA SHUHUDA
Tutawaletea shuhuda muda si mrefu
APATA KAZI
APATA KAZI




MAMA AMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA SAFARI YA KWENDA MAREKANI


DADA AMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUPONA TATIZO LA KULA MCHANGA, NA HII ILITOKEA TU BAADA YA KUTUMIA DAWA YA MENO NA MISWAKI ILIYOOMBEWA JUMAPILI ILIYOPITA

BWANA PANGALASI AMSHUKURU MUNGU KWA KUJENGA NYUMBA MBILI KWA MPIGO NA KUMPONYA MWANAE ALIYEKUWA HAONGEI

MTOTO WA PANGALISI ALIYKUWA HAONGEI NA SASA ANAONGEA AKIWA NA NABII FLORA
\


MAMA LUGANO AKIMSHUKURU MUNGU KWA KUPONYA AJALI ILIYOTAKA KUMKUMBA

MAMA RWEGASILAA ASHUHUDIA JINSI ALIVYOPATA TAABU KUPATA KIATU CHA NABII FLORA . KIATU HIKI NDICHO ALICHOVAA LEO NABII FLORA

MAMA AMSHUKURU MUNGU KWA KURUDI KUTOKA ULAYA

MAMA AMSHUKURU MUNGU KWA KUMPATA MWANAE ALIYEKUWA AMEPOTEA


MAMA MWISLAMU AMSHUKURU MUNGU KWA KUPONA UGONJWA WA KUPANUKA MOYO NA SASA AMEAMUA KUWA MKRISTO


VYETI NA XRAY YA MAMA ALIYEPONA MOYO


DADA AOTA JINO BAADA YA KUTUMIA MISWAKI NA DWA ZA MENO ZILIZOOMBEWA NA NABII FLORA

KIPINDI CHA SIFA
Baadhi ya waimbaji wa kanisa la Nabii Flora wakimuimbia Mungu siku hii ya Jumapili


 
Mama Lugano akijaribu kuigiza na kuonyesha matendo makuu ya Mungu




KIPINDI CHA KUKARIBISHA WAGENI







Comments