RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA PETER AKIWA KATIKA IBADA YA IJUMAA KUU 28.03.2013 KATIKA KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA UPONYAJI NA MAOMBEZI

SALAMU ZA NABII FLORA PETER

Ninawasalimu kwa jina la Yesu Kristo. Ninawapenda katika Bwana. Tupo katika siku hii ya Ijumaa Kuu, amabayo ilikuwa ni siku ya kutisha ambapo Bwana wetu alipitia misukosuko mingi sana kwaajili ya kutukomboa. Nilikuwa nikiongea nanyi toka asubuhi kwa habari za Pasaka, nikizungumza kipindi ambacho Yesu alikuwa amebeba msalaba kuelekea Goligotha, alipouweka msalaba akadondoka kwa mara ya kwanza, mara ya pili na mara ya tatu akatokea Simon ambaye alikuwa anatoka kwenye mashamba, alipokuwa akitokea Yule Mwaafrika akawa anamtazama Yesu alivyokuwa akidondoka, Wayahudi wakamuona huyu bwana kuwa anasikia huruma wakamsurubisha kuubeba ule msalaba pamoja na Yesu na ndipo wokovu ukaja kwetu barani Afrika.  Ndio maana watu wanapata Baraka hizo, watu weusi Waafrika kwa kupitia Simon aliyebeba msalaba na Yesu kwenda Goligotha. Ndio maana hata sisi tukiomba tukibeba mahitaji yako yakaisha, tukibeba UKIMWI unanyauka, kansa zinatoweka, kutoka na mwanaume ambaye ni Mwafrika Simon aliweza kubeba msalaba kuelekea Goligotha pamoja na Yesu. Alishika nyuma na Yesu akawa mbele, ndio maana hata sasa tukiomba mahitaji yako yanaisha, tunaweza kubeba tatizo  na kweli Goligotha likaisha.



Kama Nabii Flora, nitayapeleka matatizo yako Goligotha kama jinsi anavyokwenda kubeba matatizo yetu. Jioni ya leo amebeba matatizo yetu toka mchana na ilipofika saa kenda pazia la hekalu limepasuka, na kama una giza kubwa ni kwasababu ya maafa ya Bwana mkubwa. Yesu alikuwa wamekufa lakini siku ya tatu akaweza kufufuka. Na mimi jioni ya leo nitakwenda kufufua matatizo yako, ninaenda kuyahifadhi katika lile kaburi alilokuwa amelijenga Yusufu.

Nabii Flora akijianda kwenda kufanya kazi ya Mungu ya kuwwaombea na kuwatabiria

Na kabla ya yote ninaomba niombe...Ninaomba uinue mikono yako na mmoja uweke kifuani na mmoja inue juu. Una mtoto una mimba ninaomba ubebe vizuri maana ni wakati wa Bwana kwenda kuyabeba mateso yako...
 Nabii Flora kushoto na Mchungaji Jury

“Bwana Mtakatifu wewe ni Mungu, tazama natazama juu mbinguni jioni ya leo, nasimama mbele zako nikilia juu kwa uchungu. Tunahitaji nafsi zetu Bwana, unavyobeba matatizo na kuyapeleka kaburini, mimi Nabii Flora nimesimama kama Yusufu ambaye aliona mwili wa Yesu unakwenda kuhifadhiwa, name ninaenda kuomba kwaajili ya matatizo yenu na mateso yenu, nayeenda kuyahifadhi katika kaburi, ninahitaji mateso yak oleo niende kuyabeba katika viwanja hivi. 

Nabii Flora Peter

Ninahitaji kubeba matatizo, ninaomba ulete watu mbele sasa...dada matatizo yako yanabebwa sasa, ninaona shida zinakusanywa jioni ya leo, jioni ya leo ni wakati wa kubebwa shida zako, magonjwa uliyonayo ninakuambia kama nilivyotangaza asubuhi ya kuwa maana ya kufufuka Yesu Jumapili mateso yako yanaenda kutoweka na Jumatatu nenda ukapime afya yako. Ninakusanya mateso, ninakusanya matatizo yako, ninakusanya magonjwa, magonjwa ya UKIMWI, kansa ninakwenda kuyazika kaburini leo. Kama jinsi Yule Baba alivyokuwa mchaji na mcha Mungu na Mtakatifu, alikuwa anaitwa Yusufu, na mimi ninayabeba matatizo kama Yusufu jioni ya leo. Nakwenda kubeba shida zako, ninakwenda kubeba matatizo yako, taabu yako naibeba katika jina la Yesu Kristo.
 Mchungaji Jury


Hakika ninasema hakuna mtu leo atakayezikwa kwa mateso yako yanazikwa. Jumapili anapofufuka hakika mateso yako yanazikwa, na utaenda ku-check afya yako kwa maombi ya eo.

Ninakuambia nenda kaangalie afyako baada ya Sikukuu na unilete vyeti hapa. Ninaapa mbele za Mungu hautakuta magonjwa, kwani Yesu alibeba shida zetu, alisumbuliwa kwaajili ya makosa yetu, alipigwa kwaajili ya dhmabi zetu, kwa kupigwa kwake sisi tulipata kupona.
 Nabii Flora akifundisha Neno la Mungu

Leo tatizo lako la utasa litaondoka, tatizo lako la uchumi litaondoka, tatizo lako la kansa na UKIMWI linaondoka. Jioni ya leo unabahati sana uliyefika hapa. Jione kama umekubalika, jione kama umekubaliwa, jione kwamba wewe ni mtu wa pekee, hakika utamwimbia Yesu hadi shetani ashangae, utashuhudia maajabu ya Yesu mpaka shetani atashangaa. 
 Nabii Flora Peter

Katika Biblia inasema akamtelemsha Bwana Yesu akamfungia sanda nzuri ya kitani safi yaani kuonyesha mtu huyo alikuwa safi, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani.

Nami jioni ya leo jinsi mwili wa Yesu unavyoviringishwa na kufunikwa katika katika kitani safi, ninakwenda kuyaviringisha mateso yak oleo, jinsi mwili unavyobebwa name ninakwenda kuyaviringisha, tunakwenda kuyahifadhi Yesu anapofufuka na mateso anayaache kuzimu. Ninasema lazima ufufuke na Yesu, laziima leo uchumi.
 Nabii Flora Peter akihubiri kwa mifano na ishara

Maana ya Pasaka ni ukombozi, upatanisho, mabadiliko, ninaona watu wanapokea. Pasaka ni ukombozi na ni lazima sasa ukombozi utokee kwako kati ya ndgu na ndugu, kati ya mume na mke, lazima damu zipatanishwe, lazima upatanishwe wewe na Baraka. Maana ya Pasaka ni Ukombozi, lazima utokee ukombozi katika familia yako, taifa.


Watu wengi sana wamemsaliti Yesu, wengi wamemkana Yesu kwenye madaladala. Anaambiwa mpendwa Bwana asifiwe, yeye anajibu Mambo! Na anajibu hivyo kwasababu amekaa na Bwana yake ambaye ni Shehe atapotza dola, anaona akisema Bwana asifiwe atamkosa Bwana na hapo tayari umemsaliti Yesu. Ninasema lazima Bwana atusamehe jioni ya leo, kwani yeye alielekea mslabani na kufia dhambi zetu

Mungu awabariki.

NABII FLORA AKIWAKARIBISHA WATU KUFIKA JUMAPILI SIKU YA PASAKA.
Wapendwa siku ya Jumapili si yakukosa, kama ulivyoona nilivyokuwa namtabiria mtu mmoja mmoja, nitakuambia maisha yako miaka 10, 15, 60 yatakuwaje. Nimekuwa nikiwatabiria watu kwa kutambua siri za mtu za ndani na kumwambia kuna nini mbele yake na huo  ndiyo maana ya kutabiri. Nimekuwa nikizungumza kwa wiki nzima. Nimelkuwa nikiona watu wakibarikiwa sana, watu kutoka Zanzibar na kutoka sehemu mbalimbali, na hata leo kuna watu wameshuka na ndege kutoka Mwanza na kesho wanapanda ndege kuelekea Mwanza kwasababu ya Easter, lakini wametua katika viwanja hivi na waliweza kutabiriwa, kwasababu Mungu anaonekana katika viwanja hivi. Kuna wageni wengine kutoka Lindi na songea wamekwisha kuingia katika viwanja hivi.


Kutabiri tutaendeleza baada ya Easter kwa kutabiria maisha ya kila mtu. Ninasema nikiwa na wingu la Bwana limenizunguka. Niliambia iko miezi 18 utukufu utashuka mahali hapa ambao sio wa kawaida, watu wataponywa hujawahi kuona, miezi 18 ijao wingu litatua mahali hapa. Ninasema miaka 18 ijayo hapa patakuwa na miujiza ya ajabu, ishara za kutisha zitatokea katika viwanja hivi, watu kuponywa, vipofu kuona, viwete kutembea, waliokufa kufufuka, waliopotea kupatikana. Amina

KUIOMBEA IBADA
Baba ninaiweka ibada hii mikononi mwako, ibada kuu ya kutisha na kuogopesha. Nimekuja mbele zako Bwana, ninaomba Neno hili ninaenda kulifundisha watu wakaweze kufunguliwa.AMINA




UJUMBE KUTOKA KWA NABII FLORA PETER

Nitakuwa na ujumbe wa Mungu, siku ya leo ya tarehe 28.03.2013 siku ya Ijumaa Kuu. Nitakuwa na ujumbe kutoka marko 15:37-44 kwa jioni ya leo halafu nitaingia katika maombi na maombezi. Hili ni kanisa la Yesu Kristo la Uponyaji. Mwambie mwenzako ni Huduma ya Uponyaji.


Nitasoma kwa jina la Yesu. Naye Yesu akatoa sauti akakataa Roho, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili. Lilipasuka toka juu hadi chini. Basi Yule akida aliyesimama hapo akimwelekea Yesu alipoona amekata roho jinsi hii akasema hakika mtu huyu alikuwa mwana wa Mungu. Palikuwapo na wanawake wakitazama kwa mbali na miongoni mwao alikuwapo Mariamu Magadalena na mama yake Yesu na mama yake Yakobo mdogo wa Yose Salome hao ndio waliofuatana naye huko Galilaya na wengine wengi waliopanda hadi Yerusalem. Hata ikiiisha kuwa jioni kwasababu ni maandalio ndio siku kabla ya sababto akaenda Yusufu Alimathaya mstahili mtu wa baraza ya mashauri na mwenyewe alitazamia wokovu, akafanya ujasiri akaingia na kuuomba mwili wake Yesu, lakini Pilato akastaajabu kwamba ameshakufa akamwita Yule akida akamuuliza kwamba amekufa kitambo, hata alipokwisha kupata hakika kwa Yule akida alimpa Yusufu Yule maiti, naye Yusufu akawa amenunua sanda akamtelemsha akamfungia ile sanda


Wanawake hawakushindwa waliendelea kufuatilia wakienda taratibu wakitazama mateso ya Yesu mpaka alivyokata roho. Ninasema wamama ni jeshi kubwa hawakuogopa kama akina Petro walijificha lakini wanawake walifuata tu. Wanawake ni jasiri. Mwanamke akiamua kufanya jambo anafanya jambo, mwanamke akiamua kusimama anasimaa. Wale wanawake walikuwa wakifuatilia kwa gari, lakini wanafunzi wa Yesu waliishia njiani, waliogopa misukosuko. Wanawake kwa macho yao walikuwa wakishuhudia kile kinachotendeka.


Wakati huu ninaposema na wewe Mtanzania, unayenisikiliza hapa, unayenisoma katika blogu, unayenitazama kwenye facebook na kwenye Youtube



Tunapata habari kwamba mfupa wa Yesu haukuvunjwa ila mifupa ya wanyang’anyi ilivunjwa kwasababu Yesu ilipofika saa tisa ndipo aliposema maneno saba pale msalabani, Baba watu hawa wasamehe kwa maana hawajui walitendalo, na Yesu akakata Roho. Alipokufa Yesu pazia lilipasuka kutoka juu mpaka chini kuonyesha kwamba Yule alikuwa si mtu wa kawaida ni mtu wa ajabu, mtu alijaa uweza, alijaa uzima, alijaa uaminifu, . Kifo cha Yesu kilikuwa si cha kawaida.

 

 Mimi ninataremsha matatizo yako kama Yusufu alivyotelemsha mwili wa Yesu, kama Yesu alivyokuwa akishushwa msalabani na mimi ninaenda kushusha UKIMWI. Ninasema toooouuuuchhhhh!!! Bwana amewakumbuka, Bwana anawakumbuka nyinyi wanawake. Mwambie Bwana nikumbuke katika kilio chako. Nikumbuke Baba mimi na watumishi wote, ninaomba Bwana utukumbuka. Tumekuwa si waaminifu katika mafungu ya kumi tukipata milioni 10 tunatoa 100,000, Baba tumekuwa wanyang’anyi, tukumbuke na kutulehemu katika siku ya leo. Mwambie sasa Bwana akukumbuke, kumbuka maisha yangu kumbuka familia yangu, mume wangu, Baba yangu, mtoto wangu, mchumba wangu. Ninasema inawezekana leo kukumbukwa.


Baba mkumbuke Rose Mbajo, Lugano, wachungaji wote, watumishi wako, Katibu Molleli, wote wanaabudu hapa, Dani Mwaigomole, Eliya, Titus, Jonathan Masawe, Matroni, Mama Edward, walionivisha na kuninywesha, waliofika hapa wote, mama mdogo, Makinda, Rafa, Mwalimu Mose amekuwa akifanya kazi hata bila ya kulipwa shilingi, Octavian, Gideon Mutalemwa, kumbuka watu wanakutumikia katika roho na kweli wasioangalia vitu vya mwili, wanaofanyakazi yako kwa bisii na uaminifu, usimuache hata mmoja, Pastor Ansilla na nyumba yake, mdogo wangu Happy na mume wake, Bwana wamejitoa name toka mwaka 2010 wamepika na kutulisha Baba, unajua wanamahitaji mengi Baba, kumbuka Mawaziri, kanisa lako, Mchungaji Komba, rafiki yangu Salma ameshikamana na mimi toka mwaka 2010, ukawatendee makabeshi, ukawatedee wakaka, ukamtendee Katonda, wakumbuke wapiga vyombo, maana hivi ni viwanja vya ukombozi na uponyaji, kanisa la Yesu Kristo sehemu takatifu, kumbuka walio wema wote, mkumbuke mama Mzungu, Mama Lelo, mama Rwegasilla, rafiki yangu Tunda, mdogo wangu mama Witi.

Asante Mungu


Kulia ni Mama Lugano
Waimbaji wa kanisani
 
KIPINDI CHA SIFA NA KUABUDU
Kushoto ni Mch. Jury na Nabii Flora Peter wakimchezea Mungu wetu
 Maombezi yakiendelea
Ujenzi unaendelea katika kanisa la Nabii Flora

Huyu si mwanakwaya ila Nabii Flora alipendezewa na uimbaji wake mzuri na kumuomba aimbe
KIPINDI CHA KUTOA SADAKA

KIPINDI CHA KUOMBEA MAJI AMBAYO UKIYATUMIA UNAPATA KUTIMIZWA HAJA ZAKO


KIPINDI CHA SHUHUDA
MAMA KUTOKA IRINGA ALIYEPONA UTUMBO ULIOOZA
 
 Pia unaweza kutembelea www.nabiiflora.blogspot.com au Facebook Nabii Flora au Youtube www.youtube.com/Nabii Flora Peter


Mwandishi
Rulea Sanga wa www.rumaafrica.blogspot.com
Mpiga Picha na shooting: Rulea Sanga na Octavian



Comments