RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SIPHO MAKHABANE, KWETU PAZURI WATUA DAR TAYARI KWA TAMASHA LA PASAKA

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, hatimaye Sipho Makhabane na waimbaji wa Kundi la Ambassadors wamewasili nchini tayari wka tamasha la kimataifa la Pasaka kwa mwaka 2013
Mishale ya saa moja jioni katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere kundi hilo liliinga, likitambuliwa na waandishi wa habari huku watu wakizubaa zubaa wasijue ni kina nani hadi pale walipotoa acapella yao. Akizungumzia kuhusu ujio wao, Reuben Muvunyi, Mwenyekiti wa kwaya hiyo akasema.
Shemu ya kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka nchini Rwanda. ©Umuseke
"Tumekuja kuungana mkono na Watz, sisis tumekuja kuhubiri, kusema neno la Mungu, kwa kuwa sisi ni mabalozi wa Yesu, kwa hiyo tumekuja kusema jambo la Mungu tu hapa Tanzania."
Mwalimu wa kundi hilo, ambaye Kiswahili kinapanda vema, Sozi Joram, naye akamalizia kabla ya akapella.
"Kama kawaida sisi ndio wahubiri, lakini kupitia njia ya muziki, kuna mapya kama kawaida kila mara tukija tuna mambo mazuri, hata awamu hii, tarajieni mazuri kabisa."
Baada ya hapo, wakapiga akapella ya nyimbo inayobeba jina la album yao, Kaeni Macho, ikiwa na nyimbo kumi. Hii ni album ya 8 kwa upande wa 
Mishale ya saa nne usiku ndege ya shirika la ndege la South Africa Airways, ilitua na kuwafikisha salama Sipho Makhabane pamoja na kundi lake lenye takriban watu kumi, ambapo baada ya masuala ya visa kukamilika mishale ya saa tano, hatimaye akaibuka kwa waandishi na kupiga akapella, na pia akisema.
"Nashukuru kwa kufika hapa Tanzani kwa sababu ni mara yangu ya Kwanza kufika hapa, pia nashukuru kwa mapokezi, na pia nimejipanga vilivyo kwa ajili ya hili tamasha."
Sipho, almaarufu the Big Fish, alitunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika nyimbo za dini na kugusa pamoja na kubadili maisha ya wengi kupitia nyimbo zake, mnamo November mwaka 2012.
The Big Fish akiwa na tuzo ya kutambua mchango wake katika muziki wa injili Novemba 2012,  Pastor Benjamin Dube  ni mmojawapo wa washindi wa tuzo hii ya mara moja maishani. ©Gallo
Ungana na Silas Mbise ndani ya Gospel Celebration kuanzia saa tano asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki kusikia mahojiano ya moja kwa moja na waimbaji hawa kupitia hapahapa Gospel Kitaa na pia tovuti ya WAPO Radio FM.

Comments