Hayawi hayawi sasa yamekuwa, hatimaye Sipho Makhabane na waimbaji wa
Kundi la Ambassadors wamewasili nchini tayari wka tamasha la kimataifa
la Pasaka kwa mwaka 2013
Mishale ya saa moja jioni katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa mwalimu
Julius Nyerere kundi hilo liliinga, likitambuliwa na waandishi wa
habari huku watu wakizubaa zubaa wasijue ni kina nani hadi pale
walipotoa acapella yao. Akizungumzia kuhusu ujio wao, Reuben Muvunyi,
Mwenyekiti wa kwaya hiyo akasema.
Shemu ya kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka nchini Rwanda. ©Umuseke |
"Tumekuja kuungana mkono na Watz, sisis tumekuja kuhubiri, kusema
neno la Mungu, kwa kuwa sisi ni mabalozi wa Yesu, kwa hiyo tumekuja
kusema jambo la Mungu tu hapa Tanzania."
Mwalimu wa kundi hilo, ambaye Kiswahili kinapanda vema, Sozi Joram, naye akamalizia kabla ya akapella.
"Kama kawaida sisi ndio wahubiri, lakini kupitia njia ya muziki, kuna
mapya kama kawaida kila mara tukija tuna mambo mazuri, hata awamu hii,
tarajieni mazuri kabisa."
Baada ya hapo, wakapiga akapella ya nyimbo inayobeba jina la album yao,
Kaeni Macho, ikiwa na nyimbo kumi. Hii ni album ya 8 kwa upande wa
Mishale ya saa nne usiku ndege ya shirika la ndege la South Africa
Airways, ilitua na kuwafikisha salama Sipho Makhabane pamoja na kundi
lake lenye takriban watu kumi, ambapo baada ya masuala ya visa
kukamilika mishale ya saa tano, hatimaye akaibuka kwa waandishi na
kupiga akapella, na pia akisema.
"Nashukuru kwa kufika hapa Tanzani kwa sababu ni mara yangu ya Kwanza
kufika hapa, pia nashukuru kwa mapokezi, na pia nimejipanga vilivyo kwa
ajili ya hili tamasha."
Sipho, almaarufu the Big Fish, alitunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake
katika nyimbo za dini na kugusa pamoja na kubadili maisha ya wengi
kupitia nyimbo zake, mnamo November mwaka 2012.
The Big Fish akiwa na tuzo ya kutambua mchango wake katika muziki wa injili Novemba 2012, Pastor Benjamin Dube ni mmojawapo wa washindi wa tuzo hii ya mara moja maishani. ©Gallo |
Ungana na Silas Mbise ndani ya Gospel Celebration kuanzia saa tano
asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki kusikia mahojiano ya moja kwa moja
na waimbaji hawa kupitia hapahapa Gospel Kitaa na pia tovuti ya WAPO Radio FM.
Comments