RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UJUMBE WA PASAKA KUTOKA KWA JOHN SHABANI


UJUMBE WA PASAKA Siyo siri, hakika umeumbika unavyo viungo vyote katika mwili wako, japo pamoja na uzuri huo bado hujaridhika, hupitwi na kila aina ya mapambo yanayojitokeza, kuonyesha kuwa hujajitosheleza. Kaka /Baba yangu ni kweli wewe ni mtanashati, namshukuru Mungu aliye kuumba. Swali Je wewe ni bora kuliko hao walilazwa, wenye shida na matatizo mazito, waliobadili historia ya maisha yao na majina yao kubadilishwa ghafla na kuitwa mgonjwa, mlemavu? Au wewe ni bora kuliko hao waliokufa? Unapotaza picha hizi, hebu jione kwamba wewe ni mtu aliyepungukiwa, ni mwitaji, ni mwenye dhambi, kisha chukua hatua ya kubadilika na kugeuka. Damu ya Yesu bado inaponya, inaokoa na kutakasa. Fuatisha sala hii: Bwana Yesu, mimi ni mwenye dhambi, nahitaji msamaha wako, namkataa shetani, na kazi zake zote, ninakukubali na kukupokea Yesu, uwe Bwana na mwakozi wa maisha yangu, Amen! Baada ya kukiri maneno hayo, litafute kanisa lolote la kiroho ili ujiunge. Pia waweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716560094, ili tukuombee na kukushauri zaidi. Mungu akubariki — ZINGATIA UJUMBE HUU WA PASAKA








Comments