Kundi machachari la gospel la nchini Nigeria linaloundwa na marafiki wanne liitwalo Midnight Crew linazidi kuchanja mbuga katika tour yao huko nchini Afrika ya kusini na kufanyika baraka kwa wakazi wa nchini humo na wale ambao wanaotokea Nigeria lakini makazi yao yapo Afrika ya kusini.
Kundi hilo ambalo kwasasa lina album mpya iitwayo King of Nations bado wimbo wa Igwe uliobeba album yao ya kwanza na kuwatambulisha vyema ikingali ikifanya vizuri mpaka leo hii nakufanyika kama wimbo wa taifa popote pale wanapohudumu hata kufikia waimbaji wengine kuurekodi pia akiwemo Pastor Uche double double. Ziara yao hiyo ya kihuduma nchini humo imefanikishwa na kanisa la Redeemed Christian Church of God (RCCG) ambalo makao makuu yake yapo nchini Nigeria na likiwa limesambaa takribani duniani kote.
Ziara yao ilianza mwezi uliopita na wanatarajia kuhitimisha mwezi huu kisha kurejea Nigeria ambako ndiko makazi yao makuu yaliyopo. Hii si mara ya kwanza kwa kundi hilo kualikwa nchini Afrika ya kusini kwa huduma, lakini pia limekuwa likialikwa takribani kila mwaka nchini Marekani, Uingereza na nchi nyingine barani Ulaya kwa ajili ya huduma.
Comments