Katika maonyesho hayo waliyoanza toka siku ya ijumaa kuu hadi jumapili, mashabiki wa kundi hilo waliweza kupata kile walichotarajia kutoka katika kundi hilo ingawa pia wengi wao waliondoka kwa majonzi baada ya kugundua baadhi ya waimbaji wameachana na kundi hilo akiwemo mwanadada Mahalia Buchanan ambaye alirekodi dvd ya 17 lakini kwasasa amemaliza mkataba wake, wengine ni Sipho Manqele, Ntombizodwa Mahlangu ambaye hata hivyo haijawekwa hadharani kama ni kweli amejitoa rasmi kutokana na kuwepo fununu za kujiondoa kwake mapema mwaka jana, wengine ni Philile Chonko pamoja na Tabello.
Pamoja na majonzi hayo lakini furaha kubwa ilikuwa kwa mashabiki wa mwimbaji aliyejitoa kundini humo toka mwaka juzi Brenda Mtambo ambaye alikaribishwa kuimba katika jukwaa la Joyous ikiwa ni kutambulisha album yake aliyorekodi binafsi huku mashabiki wakilitaka kundi hilo kuendelea kumbakiza mwimbaji huyo, lakini pia mpiga drum mpya Irebolaji Arowolo aliweza kufanya vyema ingawa mashabiki wengi wa kundi hilo wameonyesha kusikitishwa na kuondoka kwa Sabu na kujaribu kuonyesha wasiwasi wao kuhusu uwezo wa kijana huyo na wengine kufikia kuuliza kwanini JC wamemchukua kijana huyo wa Nigeria wakati Afrika ya kusini wana vipaji vingi.
Mashabiki waliohudhuria shoo siku ya ijumaa wameonyesha kusikitishwa baada ya kusikia waimbaji wengine wameimba siku ya jumamosi na jumapili akiwemo Brenda Mtambo, Mkhululi Bhebhe(ambaye alikuwa amerejea kutoka visiwa vya Trinidad na Tobago kwa mwaliko) na mshindi wa SA Idols 2012 Khaya Mthethwa lakini funga kazi katika maonyesho yote alikuwa mwanamama Nobathembu Mabeka na wimbo wake Baleka ambao ndio umefungia kazi katika maonyesho yote kwa siku tatu na kumaliza huzuni ya mashabiki walioshindwa kuwaona waimbaji wawapendao.
Irebolaji mpiga drum mpya akiwa kazini na tabasamu kubwa. |
Siyanqoba Mthethwa music director wa JC akiwa kazini. |
Mwanamama Nobathembu Mabeka wimbo wake uitwao Baleke ni gumzo kwasasa. |
Viongozi wa JC katika wimbo wa pamoja. |
Duduzile Tsobane aendelea kuwabariki wengi. |
Charisma Hanekam azidi kupewa nafasi |
Brenda Mtambo akipaza sifa kwa Mungu ndani ya jc. |
Khaya Mthethwa bado yupo na JC kama kawaida sauti yake inakubalika sana. |
Mwanadada Sphumelele Mbambo au mwite Ntokozo kama kawaida na nyimbo zake za Zion. |
Mercy Ndhlovu Manqele katikati akiwakilisha wimbo kwa kabila lake. |
Hapa ni wimbo wa Baleka lazima ujirushe sana pekupeku, mwe HIZI NI NYIMBO ZILIZOMO KATIKA ALBUM MPYA YA JC 17 |
1. Umbhedesho (Jc choir)
2. Izobongo zenkosi (Mbuso khoza)
3. Uyangihola (choir)
4. Nguye inkosi (founders)
5. Mthunzi wam (Hlengiwe N)
6. Hay' inyweba (Siya Kobese)
7. Prayer (Nthabi)
8. Akukho okungenzeki (Xolile Mncwango)
9. Ulithemba lam (Phelo
10. Lona ba ratang (Palesa M)
11. Yebo ngiyazi ( Nomthi)
12. Xikwembu xayina (Mercy)
13. Thethelela (Sphumelele)
Disc 2
1. Intando emnandi (Given)
2. Even me (Ncebakazi)
3. Ndizokulandela (Unathi)
4. Motho mang le mang (Puleng)
5. Amasotsha (Ps Namba)
6. Sweet Jesus (Ps Namba)
7. Unkulunkulu uyangithanda (Sbu M)
8. Kubo bonke oThixo (choir)
9. Muphi umhlobo (Nolwazi)
10. Dumisani (Nomandla)
11. Thrz no 1 like u (Mahalia)
Disc 3
1.Simakade baba(Khaya)
2.Tshepo yaka (Nhlanhla)
3. Njengendluzela (Xolani M)
4. Mthembe njalo (Dudu)
5. Sebebuthwa (Ps J)
6. Ke ngwana hao (Sbongiseni T)
7. Zulu worship (Hlengiwe N)
8. Ingxangxasi (Sylvester)
9. Lekker smakie (Charisma)
10. Na Ma Ta (MK)
11. Baleka (Nobathembu)
12. Jerusalem (Ayanda Shange)
Comments