RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAMA ALIYEAMBIWA NA MADAKTARI KUWA MWANAE AMEFIA TUMBONI ASHANGAA NA KULIA BAADA YA NABII FLORA PETER KUMUOMBEA NA HATIMAYE MTOTO KUCHEZA TUMBONI MWA MAMAE

NABII FLORA PETER: "Ndugu msomaji wangu nina kila sababu ya kukusalimu kwa Jina la Yesu Kristo. Ninamshukuru Mungu mimi ni  mzima wa afya na Mungu anazidi kulinda huduma yetu hii ya uponyaji na maombezi hapa kanisani kwetu Mbezi Salasala. Mungu amekuwa mwema sana katika huduma yetu hii kwani kuna watu wengi wameweza kupona, kufarijiwa, kufundishwa Neno la Mungu, kubarikiwa, kurudishiwa watoto wao au ndugu zao waliokufa na kupotea katika  mazingira ya kutatanisha, vichaa wamepona, viziwi wamesikia, waliofiwa na watoto wao matumboni wamefufuliwa.
Kwa kweli ni mengi Mungu anafanya katika kanisa hili la Yesu Kristo"

 Leo kulikuwa na mama ambaye aliambiwa na madaktari kuwa mwanae aliye tumboni amekufa na ana siku tatu tumboni akiwa amekufa. mama huyu aliamua kuja hapa kanisani na alifika mida ya saa 9 mchana leo 25.04.2013 na alipoona na mimi Nabii Flora nilimuombea na baada ya muda mfupi mtoto aliweza kucheza tumboni mwa mama yake. Tunatawaletea ushuhuda huu katika facebook. Youtube na hata katika blogu yetu ya www.nabiiflora.blogspot.com.

MUNGU NI MWEMA KABISA

HUYU NDIYE MAMA ALIYEAMBIWA NA MADAKTARI KUWA MWANAE AMEFIA TUMBONI
 Mama akimweleza Nabii Flora tatizo lake
 Mama akilia wakati nabii Flora akimtabiria
 Mama akiwa na mume wake wakimsikiliza nabii Flora
 Mama akiombewa na Nabii Flora
Mume wake akiwa na Furaha baada ya mtoto kucheza tumboni mara tu nabii Flora alipomaliza kuomba na kumwambia azunguke kanisa mara ishirini

Unaweza kutupata katika blogu yetu www.nabiiflora.blogspot.com
Facebook: Nabii Flora Peter
Youtube: www.youtube.com/nabii Flora Peter

Comments