RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PASTOR PATRICK DUNCAN KUFANYA TAMASHA KUREJESHA VIJANA KANISANI


Baada ya kukaa kimya kwa muda tangu ajitoe katika kundi la Joyous, mchungaji Patrick Duncan anatarajia kufanya tamasha tarehe 26 mwezi huu katika ukumbi wa kanisa analoliongoza ikiwa maalumu kwa ajili ya kuinua vijana kwa upya na wale walioacha kwenda kanisani kurudi kwa upya katika nyumba za ibada.

Pastor Duncan anajulikana vyema kwa aina ya nyimbo alizokuwa akiimba ndani ya kundi la Joyous zikiwa ziko kwenye mlengo wa kutofanya vijana kuboreka kusikiliza au kuimba pamoja naye, album yake ya mwisho kuimba na kundi la Joyous ni ya 15 kisha akafanya live dvd recording yake akimshirikisha Pastor Jabu Hlongwane.

Ambapo dvd yake ilitoka mwezi wa pili mwaka huu sambamba na ya kundi la Dominion, pia unaweza kumpata vyema katika matoleo mengine ya Joyous kama ya 14,13,12 na mengineyo.Kwasasa Pastor Patrick Duncan anachunga kanisa la Mount Carmel Ministries discovery huko Johannesburg Afrika ya kusini ambako tamasha hilo litafanyika, ambapo mpaka sasa amekuwa akialikwa ndani na nje ya nchi yake kwa ajili ya huduma za uimbaji.

           MCHEKI HAPA KATIKA DVD YAKE MPYA "HALELUYA HOSANNA"

Comments