RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PAUL CLEMENT AACHA HISTORIA KATIKA KANISA LA VCCT MBEZI BEACH

Ulikuwa mwaka, Ukaja mwezi. Ikaka wiki, Ikafika siku, na hatimaye saa iliwadia na cha kushangaza dakika ikafika, na la ajabu kuliko yote ni sekunde iliweza kugonga ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Paul Clement kuweka historia katika kanisa la VCCT. MC Samsasali na Chavala walipoona sekunde imefika waliamua kupaza sauti zao na kumwita Paul Clement katika stage kwaajili ya kufanya kazi ya Mungu na kufungua tamasha lake la uzinduzi wa albamu yake ya kwanza ya "UMENIITA".



Watu walipiga nderemo na shangwe kuona kijana mdogo kufanya mambo makubwa ambayo yaliwasha masikio ya baadhi ya watu. Watu walionekana kutokwa na machozi na wengine kububujika kwa kumuombea kwani kijana huyu katoka mbali na huduma yake hii ya uimbaji. Ni mengi amepitia lakini Mungu amemuwezesha kufika mahali alipofika.

Mama yake alionekana mwenye fiuraha kumuona mwanae akizindua albamu yake na aliweza kumuahidi kumchangia mwanae Tshs. 200,000 ku-support kazi ya Mungu. Watu wengi walijitokeza kumchangia Paul Clement na wengine walionekana kutupa pesa zao wakati akiimba. Na hii ni kutokana na nyimbo zake kuwa na mguso wa ajabu katika maisha haya tuliyonayo na pia zinakuweka katika uwepo wa Mungu.



Mama Mchungaji wa kanisa la VCCT, Mrs. Huruma Nkone aliweza kuombea albamu hiyo ili Mungu aweze kuwa naye Paul katika huduma yake ya uimbaji na kumuomba Mungu amsaidie Paul asisikilize sauti zingine zenye kumkatisha tamaa katika huduma hii aliyonayo ya kumuimbia Mungu.

Paul Clement ambaye alisindikizwa na Mpelo Kapama pamoja na The Voice Of Acapella na Kisha kupanda Paul Clement kwenye Jukwaa. Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo Dr. Wandwi aliyekuwepo kwa Niaba ya Dr. Huruma Nkone Mchungaji Kiongozi wa VCCT alisema kuwa Mungu amempaka Mafuta Paul Clement kama Mtumishi wake kwa habari Ya Kuabudu katika Nchi ya Tanzania na Nje Ya Tanzania.
 JAEL GROUP
 VOCAPELA
 MIRIUM LUKINDO AKIIMBA NA JAEL
 BOMBI JOHNSON
 UMATI WA WATU

 COMEDIAN CHAVALA NA MC PILIPILI YA SHUGHULI
 PAUL CLEMENT AKIFANYA VITU VYAKE














Comments