Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu maswali ya papo kwa papo kwenye picha iliyopigwa mwaka 2012. © Global Publishers
Ifuatayo ni nukuu ya majibu ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda alipoulizwa swali kipindi cha maswali ya papo kwa papo Alhamisi tarehe 30 mei 2013 bungeni kuhusu kuchelewa kwa uchunguzi wa kesi ya mauaji ya Padri Mushi visiwani Zanzibar licha ya FBI kushiriki kwenye upelelezi huo
Ninachoweza kusema tu kwa sasa ni kwamba; uchunguzi ule umechukua muda mrefu kwa sababu ya hali halisi ya tatizo lenyewe lilivyotokea, na maelezo yaliyopatikana ni maelezo ambayo bado yanahitaji kuthibitishwa vizuri zaidi kwa mujibu wa taratibu.
Kwa hiyo hata pale ambapo mtu amekamatwa, amepelekwa mahakamani, bado uchunguzi lazima ukamilike kikamilifu ili tuwe na uhakika kwamba mwisho wa yote ataweza kutiwa hatiani.
Kwa hiyo kwa kweli mambo mengine yanakuwa na ugumu wenyewe tu kwa namna yanavyojitokeza, lakini imani yangu ni kwamba tutafika pazuri, inshallah na mambo mengine tutafikisha inapotakiwa.
Padri Mushi aliuwawa kwa kupigwa risasi tarehe 17 Februari 2013 wakati akielekea ibadani Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili. Tazama picha za maazishi yake hapa.
Comments