RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SOWETO GOSPEL CHOIR YAFANYA SHEREHE NA WAANDISHI WA HABARI


Kundi la kwaya ambalo limejizolea tuzo nyingi za kimataifa duniani Soweto Gospel Choir wiki hii wameendelea kusherehekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ambapo safari hii wamefanya sherehe na waandishi wa habari wa nchini kwao Afrika ya kusini katika halfa fupi iliyoandaliwa na kundi hilo.

Kwaya hiyo ambayo inaundwa na waimbaji wenye uwezo wa juu katika uimbaji na uchezaji inajivunia mafanikio ya haraka waliyoyapita tangu kuanzishwa kwake ikiwa pamoja na kupata nafasi ya kuhudumu katika majukwaa ya kimataifa, sherehe za kimataifa kama ilivyokuwa hivi karibuni walipohudhuria katika sherehe za miaka 50 ya umoja wa nchi za Afika (AU) zilizofanyika huko Addis Ababa Ethiopia.

Lakini kama haitoshi kwaya hii imeshirikishwa katika album za waimbaji maarufu duniani pamoja na kuimba nao majukwaani. kwasasa kwaya hii baada ya kurejea kutoka barani Australia kwa ziara linatarajia kuelekea nchini Canada kwa ajili ya muendelezo wa tour yao ya kutimiza miaka 10.


SGC wakiimba katika hafla hiyo.



Mmoja wa viongozi wa SGC bwana Garreth akizungumza na wageni.




Waandishi kama kawaida.

Meneja wa kundi Jimmy Mulovhedzi, baba yake na kijana huyu ambaye kwasasa marehemu ndiye mwanzilishi wa kundi la SGC.

Tuzo za Soweto mezani.

Wadada wa SGC wakiwa wamepozi na tuzo za kundi hilo.

Kiongozi wa Joyous Celebration Lindelani Mkhize alihudhuria pia hapa akiwa na waimbaji wa Soweto, kushoto ni choirmaster wa Soweto Shimmy Jiyane ambaye zamani alianza kama mcheza shoo ndani ya Joyous Celebration

Mwanadada matata Sibongile Makgathe akipozi kwa picha, ni kati ya waimbaji wa kwanza wa Joyous Celebration.

Soweto Gospel Choir wakiimba pamoja na Judith Sephuma sherehe za AU Ethiopia. Picha kwa hisani ya page ya Facebook ya kundi hili.

Thanks GK

Comments