Mchoro wa sura ya kiongozi wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, ukiwa Thokoza Park, Soweto, Jo'berg |
Hakuna taarifa raasmi iliyotolewa siju ya Jumatano kuhusiana na hali ya
kiafya ya Baba Madiba, Nelson Mandela, ambaye amelazwa kwenye hospitali
ya Pretoria, ambapo hapo awali hali yake ilikuwa mbaya zaidi.
Mzee Mandela, ambaye anatarajiwa kufikisha umri wa miaka 95 mnamo mwezi
ujao, amegusa mioyo ya taifa la Afrika Kusini ambapo maua mengi na kadi
za kumtakia kupona haraka zimeonekana kujaa nje ya hospitali ya
Pretoria, ambapo pia baadhi ya watu wamejawa na mtazamo tofauti
kuhusiana na ugonjwa wake.
Lucas Aedwaba, ambaye ni mwanausalama jijini huko, amezuungumzia mtazamo
wake, akisema kuwa taifa la Afrika Kusini halina budi kukubalinana na
hali halisi badala ya kulia, akimuelezea Mandela kama shujaa.
Kwa upande wake, Askofu mkuu wa Anglikan Cape Town, Thabo Makgoba
amesema kuwa ni muda wa kusheherekea kwamba mzee Mandela ameishi vema
na kuacha urithi wake. Maneno hayo yaliwekwa kwenye ukurasa wake wa
facebook mara baada ya kumtembelea siku ya Jumanne.
Jumbe kadhaa za kumtakia heri Nelson Mandela, kwenye lango la hospitali ya Pretoria. ©Daniel Born/Times Live |
Halikadhalika katika maombi yake hayo, Askofu Makgoba aliombea nguvu kwa
ajili ya mke wa Mandela, Graca Machel, na wengineo wote ambao
wanampenda kiongozi huyu aliye katika wakati mgumu, na pia kuomba Mungu
aiongoze timu ya madaktari ambayo inamtibu mpambanaji huyo wa ubaguzi wa
rangi ambaye alifanikiwa kuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo mara baada ya
kutoka jela alikokuwa kwa muda wa miaka 27.
Wanafamilia na viongozi wengine wa ukoo walikutana Qunu, mji wa
nyumbani wa Mandela, ulioko mashariki mwa Afrika Kusini, lakini hakuna
taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mjadala wa kikao hicho.
Mara ya mwisho Mandela kuwepo kwenye umma ilikuwa ni mwaka 2010 kwenye michuano ya kombe la dunia ambayo ilifanyika nchini humo.
Thanks:GK
Thanks:GK
Comments